- Ni nini maana ya digital marketing na kwa nini ni muhimu katika biashara ?
-Chukulia muuliza swali ni mklima, na hajui chochote zaidi ya kusikia sikia kwa watu.
- Je! Ni njia gani za kawaida za digital marketing na ni ipi inafaa kwa biashara ya matunda na mboga mboga?
- Hapa chukulia muuliza swali ni mfanya biashara mdogo wa matunda na mboga mboga katika soko ilala, mkoani Dar.
- Je! Kuna changamoto gani za digital marketing na jinsi ya kuzitatua?
==
My take
- Uzi ni mzuri, tuendelee kupeana elimu,
Shukrani kwa maswali mazuri. Naomba kujibu kama ifuatavyo:-
SWALI LA 1.
Ni nini maana ya digital marketing na kwa nini ni muhimu katika biashara ?
-Chukulia muuliza swali ni mklima, na hajui chochote zaidi ya kusikia sikia kwa watu.
MAJIBU:
Kwanza kiswahili cha neno Digital Marketing ni Utafutaji wa Masoko kwa njia ya kidigitali (mtandao).
Hivyo Digital Marketing ni ile hali ya kutumia majukwaa mbalimbali ya mtandaoni kutafuta masoko.
Na majukwaa haya yanaweza kuwa mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Jamii Forums, Twitter na aina nyingine ya mitandao ya kijamii na pia matumizi ya Tovuti (Websites).
Faida za Digital Marketing:
A. Ni njia rahisi ya kufikia wateja wengi kwa gharama ndogo.
B. Ni njia rahisi ya kujenga brand (Jina lako au biashara yako) na kujenga uaminifu mkubwa kwa wateja.
C. Ni njia rahisi ya kutambulisha biashara yako na kufahamika na wengi.
D. Inaongeza mauzo zaidi katika biashara yako ukilinganisha na kukaa tu hapo sokoni ukitegemea wateja wa hapo tu.
E. Inarahisisha ukuaji wa biashara yako.
SWALI LA 2:
Je! Ni njia gani za kawaida za digital marketing na ni ipi inafaa kwa biashara ya matunda na mboga mboga?
- Hapa chukulia muuliza swali ni mfanya biashara mdogo wa matunda na mboga mboga katika soko ilala, mkoani Dar.
MAJIBU.
Moja kati ya kitu muhimu sana kwa mteja linapokuja kwenye kufanikisha biashara Yake mtandaoni ni kufahamu kundi la wateja anao walenga.
Hapa ni kuanzia kipato, umri, sehemu walipo wateja anao walenga, Jinsia, Kiwango cha Elimu, Changamoto zao na Vitu ambavyo wanapendelea zaidi.
Kwa mfanya biashara mdogo wa matunda na mboga mboga pale Soko la Ilala mkoa wa Dar-es-Salaam anaweza kutumia njia ifuatayo kufikia wateja wengi mtandaoni:
Huyu anapaswa kutumia mitandao ya kijamii tu.
Kwasababu haina gharama kubwa na pia ni rahisi kwake yeye kuisimamia baada ya kueleweshwa vitu vichache kama vile, Jinsi Ya kupost picha za bidhaa yake, wakati gani apost, post zake azipangilie katika utaratibu gani mzuri ili kuepuka kuwachosha wafuasi wake, na namna nzuri ya kupangilia ukurusa wake (settings nzuri za Bio & Profile).
Mitandao ya kijamii ambayo inaweza kumfaa ni kama vile WhatsApp, Instagram, Twitter na Facebook.
Ambayo atapendelea yeye kutegemeana na aina ya watu anao walenga basi ataitumia.
Na wakati wa kuanza ni muhimu kuchagua mtandao mmoja kwanza kisha unaweza kuongeza mtandao mwingine hii ni kwasababu ukitumia mitandao mingi mwanzoni itakuwa ngumu kwako kuzikuza na kuzisimamia inavyotakiwa.
Pia anaweza kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram (Hapa anapaswa kupata muongozo ili kukamilisha vizuri). Ina matokeo mazuri sana ukiandaliwa tangazo na mwenye uzoefu.
SWALI LA 3.
Je! Kuna changamoto gani za digital marketing na jinsi ya kuzitatua?
Changamoto zipo, pamoja na kwamba faida ni nyingi.
A. Inahitaji kuwa na ujuzi wa kidigitali katika kuendesha na kusimamia majukwaa yako ya biashara mtandaoni.
Hapa kuna kufahamu jinsi ya kusoma data za matokeo ya ukurasa wako ili kufahamu mwenendo wa ukuaji wako mtandaoni.
Wapo watu wanaoweza kukufundisha na ukaepukana na changamoto hii.
B. Uaminifu hasa mwanzoni unapoanza.
Unahitaji kuwa mvumilivu mwanzoni kwasababu ndiyo muda wa kuonyesha unachokifanya na wakati huo hupati wateja kwasababu bado wana kusoma kwanza ili kukufahamu ndipo waanze kuja kununua.
Hatua hii inabidi uwe mvumilivu, weka picha zako ukiwa na wateja wako, weka picha kuonyesha ukiwa na bidhaa zako unazipanga.
Na pia weka shuhuda za wateja ambao umewahudumia.
Hizo njia zitakusaidia kujenga uaminifu mtandaoni hivyo kumuondolea mteja wasiwasi wa kutapeliwa.
C. Inahitaji uvumilivu mwanzoni unapoanza.
Digital marketing ni njia nzuri ila siyo rahisi mwanzoni unapoanza.
Ili kuitambulisha biashara yako mtandaoni mwanzoni Utahitaji kuwa na mpango mkakati mzuri na kufanya kazi kubwa ya kutekeleza.
Inaweza kuchukua kuanzia miezi mitatu kuanza kupata matokeo mazuri ila tu kama utakuwa unapost mara kwa mara katika akaunti yako.
Karibu kwa maswali zaidi kama kuna kipengele hakijaeleweka.