Jinsi ya kuanza biashara ya mafuta kipindi hiki cha mzozo wa Iran vs Israeli-Marekani

Jinsi ya kuanza biashara ya mafuta kipindi hiki cha mzozo wa Iran vs Israeli-Marekani

chai ya rangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2026
Posts
1,042
Reaction score
3,095
Pipa moja la mafuta ghafi linauzwa $70 hadi $90 linakua na ujazo wa lita 159. ukienda kusafisha crude oil unapata petrol, diesel, kerosine, gas na lami. hivi vitu vyote ukivipima ujazo wake unafika lita 170 maana ujazo una expand

garama za kusafisha ni $1 kwa lita, cha kuganya ili kumaximize profit nenda moja kwa moja hadi kwenye mlango bahari wa hormouz, kwasababu saivi Iran wanaufunga huo mlango bahari lakini wanaufunga kwaajili ya marekani, kwakua wewe sio mmarekani utawaambia ni m Tz na wao hawana shida na Tz na watakuuzia mafuta kwa bei ya kawaida, kipindi hiki watakuuzia jwa bei ya chini zaidi labda $40 hadi $50 kwa pipa kwasababu maoipa mengi yamezuiliwa hayana pakwenda

baada ya kusafisha kwa kufanya refinery ujazo huongezeka kama nilivosema kutoka 159 hadi 170 au zaidi hapo utapata vitu mbalimbali, hamna kinachotupwa hata kimoja vyote vipo juu kwenye bei

kwa bei ya sasa ya tz petroli kuuzwa 4000th wewe utauza 3500 tsh kwaiyo kwenye lita 170 utapata 595000, kumbuka wewe ulinunua kwa $40 hadi 50 ambayo ni sawa na laki au laki na 25 hivi kwa tsh. faida yako kwa kila pipa ni 495,000tsh
 
Unaweza kupiga dili na wale askari walinzi pia pipa wanaweza kukuvushia hadi kwa $ 10-20 ila uwe makini mana sio njia salama sanaa
 
Naona kama hesabu zimewahi kutangulia kuliko uhalisia wa jambo lenyewe
 
Kwanini usitangulie hapo Tanga usubirie mafuta ghafi kutoka Uganda,pale ukiwapiga walinzi mlungula unajichotea tu, kusafisha ndio sijui utasafishia wapi

Mimi nadhani Tanzania tungekuwa na viongozi kweli, mafuta ya Uganda tungesafisha wenyewe halafu tuuze soko lote la East and Central badala ya kuacha yakasafishwe sijui wapi huko ndio tuletewe mafuta
 
Kwanini usitangulie hapo Tanga usubirie mafuta ghafi kutoka Uganda,pale ukiwapiga walinzi mlungula unajichotea tu, kusafisha ndio sijui utasafishia wapi
Akiingia AliExpress au Temu atakutana na kampuni za Wachina zinauza mitambo midogo ya kusafisha mafuta ghafi (mini-refinery) kwa bei rahisi mapipa 1,000-20,000 kwa siku
 
Akiingia AliExpress au Temu atakutana na kampuni za Wachina zinauza mitambo midogo ya kusafisha mafuta ghafi (mini-refinery) kwa bei rahisi mapipa 1,000-20,000 kwa siku
Hii mbona nzuri sana, wenye hela wanakwama wapi
 
Back
Top Bottom