Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Nimemsikia ndugu yangu ngara23 akilalamika mwezi mzima wa Tisa, na sasa tumeingia mwezi wa Kumi bado anaendelea kulia.
Kariakoo mawinga kabla mteja hajafika tayari wanakuwa na bei wameshakubaliana karibu mtaa mzima.
Mfano, umeenda kununua fridge aina ya Hisense lita 160, watakubaliana labda laki sita na tisini.
Ukifika, atakayekupokea atakuambia laki saba na nusu, kisha atajifanya anakupunguzia mpaka 690k. Hapo atasisitiza kuwa hapunguzi kwani amepunguza vya kutosha.
Wakati huo fridge bei yake ni 570k hadi 620k. Hivyo, ukijichanganya si ajabu ukapigwa zaidi ya laki moja.
Sasa ili usipigwe zingatia mambo yafuatayo:
Acha nipumzike sasa.

- Kusanya taarifa za kitu unachotaka kununua kabla ya kwenda Kariakoo. Ikiwa tayari una pesa au unatarajia kuwa nazo wiki moja ijayo, fanya utafiti mtandaoni na tembelea maduka Kariakoo ukiwa huna pesa ili ufanye upelelezi vizuri. Kisha weka wastani wa bei baada ya kufanya upelelezi. Mfano wastani wa Hisense ni 670k.
- Usiingie kwenye maduka yenye mtaji mdogo. Kadiri mtaji unavyokuwa mkubwa, ndivyo uwezekano wa kupata bidhaa za bei nafuu unavyokuwa mkubwa.
- Epuka maduka yaliyopo mbele ya barabara. Ikiwa mbele ya barabara, basi loweka kwenye ghorofa. Mtaji mdogo + mbele ya barabara = bei za juu. Zunguka upande wa nyuma, kisha angalia duka lenye mtaji mkubwa, hapo kuna nafasi ya kupata bei nzuri.
- Usiingie dukani na kununua kwenye maduka yenye wauzaji wengi, hasa wale watakaokurukia. Duka lenye vijana wengi kupigwa ni rahisi zaidi. Hautakuwa na uhuru wa kufikiri vizuri kwani watakuzonga sana.
- Hakikisha unamtambua mwenye biashara au msimamizi wa duka. Hawa mara nyingi hawatakupokea na huwa ndani wakishughulikia shughuli za duka kama hesabu. Ukiona mtu anajifanya yupo busy, mfuate huyo na uliza bei.
- Usiwe mwepesi kuuliza bei. Zunguka dukani kama unashangaa bidhaa kabla hawajajua unataka kununua nini. Baada ya muda utajua mazingira ya duka na kiongozi wa duka ni nani, kisha uliza bei ya bidhaa unayotaka.
- Tekni za kupunguza bei (bargain price techniques). Ikiwa amekutajia bei ya kuanzia laki tatu hadi laki tano unusu, punguza laki moja na hamsini. Mfano, fridge bei yake laki 7, mwambie una laki tano hamsini hadi sabini. Ukimfuata mwenye duka, punguza kidogo kidogo hadi mfikie bei unayoitaka.
Acha nipumzike sasa.