Labda jibu langu hili ni General zaidi ya swali lako, lakini nimesema ngoja nilitoe tu.
Gari yoyote ya 4WD au AWD huwa inandikwa pale nyuma. 4WD ni nzuri kuliko magari yote kwani unaweza kuitumia kama 2WD na vile vile kama 4WD ukihitaji hasa kwenye utelezi, na kwa magari kama Jeep, una uhuru wa kuweka part-time 4WD kuwa iwapo barabara itakuwa na utelezi basi gari linajiingiza 4WD automatically na baada ya hapo linarudi 2WD. AWD inakuwa kwenye 4WD muda wote na huenda hali hiyo haihitajiki kwenye barabara za kawaida, na hiyo inaweza kuwa inakula mafuta mengi bure, na vile vile imbalance ndogo tu inaweza kusababisha gari kuwa linatikisika sana.
Soma nyuma ya gari pale kutakuwa na alama ama 4WD au AWD, magari mengine huweza pia kuonyesha 2WD lakini hiyo ndiyo standard, kwa hiyo wasipoonyesa inakuwa na maana kuwa ni 2WD. Halafu pia uwe makini, kuna magari mengine kwa mfano Ford F150 ambayo ili uliweke kwenye 4WD lazima ukaze nati fulani kwenye matairi ya mbele, jambo ambalo linaweza kuwa kero sana ukiwa barabarani, na hivyo unaweza kujikuta unaliendesha katika AWD ingawa halikuwa lengo lako.