Jinsi ya kufahamu ist with 4WD na isiyo na 4WD .

Jinsi ya kufahamu ist with 4WD na isiyo na 4WD .

M2flan

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2013
Posts
584
Reaction score
293
Habari wakuu, nahitaji kununua hii gari Toyota(ist)nafahamu kuna za cc1200 na cc1400, lakin nimeambiwa niwe makini hiz za cc1400 nyingi ni zina option ya 4WD na baadhi hazina, so naomba msaada nitumie vigezo vipi kufahamu yenye 4WD na isiyo na 4WD maana nahitaji ya cc1400 isiyo na 4WD .
 
4wd no bra zaidi kwani inanguvu Mara duty yakawaida, haitegemei front wheel ketembea hats ikiua cv joint
 
Habari wakuu, nahitaji kununua hii gari Toyota(ist)nafahamu kuna za cc1200 na cc1400, lakin nimeambiwa niwe makini hiz za cc1400 nyingi ni zina option ya 4WD na baadhi hazina, so naomba msaada nitumie vigezo vipi kufahamu yenye 4WD na isiyo na 4WD maana nahitaji ya cc1400 isiyo na 4WD .
gari unaagiza japan ? au unanuna kwa mtu ?

Kama ni Japan website zina details zote za gari husika na pia IST yenye 4wd inakua na sticker nyuma na ukiangalia chini utaona ina diff pia exchaust yake iko tofauti na ist za kawaida sababu inaiipisha diff ikae vizuri
 
4WD kwny ka IST ni ujinga tu,hakuna kitu katafanya.
Wewe ndio mjinga unayeishi kwa assumptions. Ulishawahi kuwa nayo?

Mdau unayetaka kununua IST, mimi nakushauri nunua yenye 4WD kama unaishi maeneo yenye miinuko yenye utelezi au mchanga. Mimi nina site yangu Kibaha Misugusugu, nina Hilux Single Cabin inashindwa kupita kufika kwenye kiwanja lakini IST ndio naitegemea sababu ya mchanga
 
Tofauti yake kubwa nikuwa IST ambayo ina 4WD lile bomba lake la kutolea Moshi (Lakupumulia) huwa lipo upande wa Kushoto na IST ambayo haina 4WD bomba lake la kutolea moshi (Lakupumulia) huwepo upande wa kulia.
 
Wewe ndio mjinga unayeishi kwa assumptions. Ulishawahi kuwa nayo?

Mdau unayetaka kununua IST, mimi nakushauri nunua yenye 4WD kama unaishi maeneo yenye miinuko yenye utelezi au mchanga. Mimi nina site yangu Kibaha Misugusugu, nina Hilux Single Cabin inashindwa kupita kufika kwenye kiwanja lakini IST ndio naitegemea sababu ya mchanga

Sawa taahira mwenye Hilux ambayo 4wd yake inashindwa kupita lkn IST 4WD inapita.
 
Labda jibu langu hili ni General zaidi ya swali lako, lakini nimesema ngoja nilitoe tu.

Gari yoyote ya 4WD au AWD huwa inandikwa pale nyuma. 4WD ni nzuri kuliko magari yote kwani unaweza kuitumia kama 2WD na vile vile kama 4WD ukihitaji hasa kwenye utelezi, na kwa magari kama Jeep, una uhuru wa kuweka part-time 4WD kuwa iwapo barabara itakuwa na utelezi basi gari linajiingiza 4WD automatically na baada ya hapo linarudi 2WD. AWD inakuwa kwenye 4WD muda wote na huenda hali hiyo haihitajiki kwenye barabara za kawaida, na hiyo inaweza kuwa inakula mafuta mengi bure, na vile vile imbalance ndogo tu inaweza kusababisha gari kuwa linatikisika sana.

Soma nyuma ya gari pale kutakuwa na alama ama 4WD au AWD, magari mengine huweza pia kuonyesha 2WD lakini hiyo ndiyo standard, kwa hiyo wasipoonyesa inakuwa na maana kuwa ni 2WD. Halafu pia uwe makini, kuna magari mengine kwa mfano Ford F150 ambayo ili uliweke kwenye 4WD lazima ukaze nati fulani kwenye matairi ya mbele, jambo ambalo linaweza kuwa kero sana ukiwa barabarani, na hivyo unaweza kujikuta unaliendesha katika AWD ingawa halikuwa lengo lako.
 
Back
Top Bottom