Jinsi ya kufahamu ist with 4WD na isiyo na 4WD .

Bila shaka hio Hilux itakua na shida au mbovu..mimi natumia Hilux Surf napita sehemu yoyote ile na wala situmiagi 4WD yani nikishusha gia kwenye L au 2 napita popote pale...siangalii hapa pana mchanga, utelezi au nini
 
una gari inaweza tembea kama imeua cv joint?
 
Bila shaka hio Hilux itakua na shida au mbovu..mimi natumia Hilux Surf napita sehemu yoyote ile na wala situmiagi 4WD yani nikishusha gia kwenye L au 2 napita popote pale...siangalii hapa pana mchanga, utelezi au nini
Unaongea kitoto toto kama nilivyokuwa mdogo wakati gari zote nilikuwa naziita 'PIJO' Eti unapita popote! Hakuna gari yenye uwezo wa kupita popote na ndio maana mengine yamewekwa 4WD kuyaongezea uwezo. Hizo ni porojo za watu ambao hata gari lenyewe hawajui kuendesha, hiyo moja.

Mbili, kuna tofauti kubwa sana kati ya Hilux Surf (SUV) na Hilux Pick Up kwa namna zitakavyoperform kwenye rough roads. Pick Up ni nyepesi sana nyuma kiasi kwamba haikwami kwenye mchanga tu, hata kwenye surface iliyo uneven, kitendo tu cha tairi moja ya nyuma kutokugusa chini unaweza kulazimika kurudi nyuma kidogo upite kwa kasi. Ni kwa sababu hii Kirikuu zimewekwa four wheel sababu zenyewe ni nyepesi zaidi.

Tatu, gari langu si bovu japo ni la zamani sana (1991) na halina L na 2 kwa sababu ni manual. Kama unakaa mjini basi mara moja moja tembea nje ya mji uzijue changamoto za njia na barabara za nchi yetu. Yapo maeneo kule Kilema hata gari zenye four wheel zinanasa kwenye tope.
 
Gari zote hizo(hilux na hilix surf) zina engine moja kama ni 2L,3L na 1KZ chassis moja hata kama ni nyepesi hio hilux tofauti yake ni 200Kg kwaio kiuhalisia hakuna sehemu itakayo kua na mchanga mkubwa kuishinda hizo gari mbili yani sehemu ikwame Hilux ije ipite IST
 
Ndio maana nikakushauri uwe mtafiti kuliko muongeaji. Haya magari mawili yameachana mbali sana. Labda unakurupuka kurupuka tu hata usijue ni hilux ipi naizungumzia. Hii pickup kaiingize pale Coco Beach wanakocheza mpira ndio utajua mziki wake. Unaendesha gari mjini lkn unajiapiza HAKUNA SEHEMU ITAKAYOKUWA NA MCHANGA MKUBWA KUISHINDA KUPITA, unazungumzia mchanga huu unaofagiliwa kwenye lami au unasikia tu mchanga huuelewi?




Pengine suala la kuambiwa kuwa IST yenye fourwheel drive inaperform vizuri kwenye mchanga ndio linakutesa kwa namna unavyoiunderestimate IST. The thing is, size ya gari sio issue, issued ni mechanism. Canter ya 5tonnes na 3490cc itakwama kwenye mchanga ambao Kirikuu yenye fourwheel drive itapita.

Mimi nazungumzia experience ya magari mawili ambayo yote ninayo na ninafanya kazi kwenye mazingira ya michanga, wewe unazungumzia assumption. Hiyo pick up tairi za nyuma ndio zinasukuma at the same time nyuma uzito ni mdogo, ikikutana na mchanga mwingi, tairi za mbele kwa kuwa zenyewe zinasukumwa tu, zinatend kuzama ndani ya mchanga na kwa kuwa uzito mkubwa upo mbele kwenye engine tairi za nyuma zinapata extra load ya kuzikwamua za mbele kwenye mchanga, hapo ndio utajua maana gari imekalia.

Sina hakika kama umeshaendesha gari
 
Kama nilivyokuambia hata hio Hilux uliyoiweka na IST hio tofauti yake ni 200kg swala sio kukurupuka wewe ndo uliyekua huelewi umetaja Hilux bila kusema ni ipi hivyo vidogo au zile kubwa mwisho wa siku nasema hivi hakuna sehemu inase Hilux ije kupita IST
 

My Nissan Dualis ni 4WD lakini haijaandikwa nyuma labda hayo ma toyota yenu
 
My Nissan Dualis ni 4WD lakini haijaandikwa nyuma labda hayo ma toyota yenu
Tumia lugha nzuri mzee wangu; kwanza tambua kuwa Toyota ni gari zuri kuliko Nissan by all standards, ndiyo maana Nissan ilishindwa kuhimilia mikiki ya soko ikanunuliwa na makampuni ya Ulaya Renault na Daimler, wakati Toyota iko pale pale. Binafsi nilishafanya kazi pale Toyota Nagoya na Nissan Sendai mwanzoni mwa miaka ya tisini nikiwa training, najua culture yao na sifa zao.

Kuna magari ambayo huwa hayaonyeshi iwapo ni AWD au 4WD hasa yale yanayotengenezwa kwa ajili ya soko la offroad; kwa hiyo inawezekana Nissan yako umenunua used lakini ilikuwa ni kwa ajili ya soko la offroad kama Australia Outback au kwa matumizi ya Farmers. Hata hivyo kitabu chake kitakuwa kinaonyesha hivyo, au kwenye dashboard yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…