Jinsi ya kufanya miujiza (Education is power)


Tatizo kila mtu anamuona mwenzie ndiyo kamezesheswha halafu yeye ndiyo ana mawazo huru,sasa uwanja huu ndiyo ungeamua ni yupi kamezeshwa na yupi hajamezeshwa.
 
Nimekupata. Kumbe wewe ni mfuasi wa biblia!. Mimi naongelea fikra huru isiyo kwenye kifungo cha dini. Nilazima tufunguliwe kutoka kwenye vifungo vya dini.

Kwa mantiki hiyo wewe ni yote katika yote?

Huna aliyekuumba wala anayekupa pumzi ya kila siku?

Unaposema fikra huru una maana gani? Je hayo mawazo/fikra itakayokupa ku-conclude usahihi wa jambo fulani unaipata toka kwa nani?
 

Kwanza kabisa mie sio mkristo,na huwa najiuliza sana kwanini wakanaji mungu wengi wa humu wanaonekana walikuwa wakristo!

Ujue tatizo humu ni kwamba wanaokana mungu wanajiona ndiyo wenye mawazo huru kwa huko kukana mungu,yani kupinga kile wanachokiamini wenzenu ndiyo hali hiyo mnaona mna uhuru wa mawazo. Suala la Mungu ni suala linalohitaji kuamini kwa sababu haonekani, hivyo suala la wewe au nyie kukana mungu si jambo la ajabu hapa kwa sababu haonekani huyo huyo mungu.

Kwahiyo suala hapa ni kuangalia ni ishara na hoja zipi kuonesha uwepo wake mungu na hoja zipi za kuonesha kuwa hakuna mungu,lakini tatizo lenu nyie muda wote mnapinga tu. Sie hatuwezi kuwalazimisha nyie muamini tunavyoamini sie na wala nyie hamuwezi kulazimisha tuamini mnavyoamini nyie,hivyo mmoja anapomwambia mwenziye imani yake si sahihi basi anapaswa aeleze pia usahihi wa imani yake ni upi sio kuishia kuponda imani ya mwenzio.
 
Kwa mantiki hiyo wewe ni yote katika yote?

Huna aliyekuumba wala anayekupa pumzi ya kila siku?

Unaposema fikra huru una maana gani? Je hayo mawazo/fikra itakayokupa ku-conclude usahihi wa jambo fulani unaipata toka kwa nani?

unajua mkuu huu ulimwengu wa vitabu vya mafundisho mbalimbali unateka akili za watu kwa kasi kiasi kila mtu anataka kuwa mjasiriamali siku hizi!siyo kila elimu inaelimisha nyingine zinapotosha.
 
yote kayamaliza Yesu"hata ningekuwa na imani ya kuhamisha milima kama sinao upendo mimi si kitu kabisa"maana nafsi iliyo huru inatakiwa kujazwa na upendo wa kimungu kabla ya yote hayo,maana hiyo miujiza sijui kufufua wafu,uponyaji yanawezekana kwa mwanadamu,ila nafsi ya mwanadamu kuwa na hadhi ya kimungu siyo hiyo miujiza,ni upendo ufananao na Mungu usio na mipaka!
 
Kwa mantiki hiyo wewe ni yote katika yote?

Huna aliyekuumba wala anayekupa pumzi ya kila siku?

Unaposema fikra huru una maana gani? Je hayo mawazo/fikra itakayokupa ku-conclude usahihi wa jambo fulani unaipata toka kwa nani?
Kuna thread hapa nitaileta inaongelea kabla ya kuzaliwa hapa duniani mtu alikuwa yukoje na baada ya kufa hapa duniani anakuwa yupoje. Nadani katika hiyo thread nitajibu maswali yako yote. Maana ni somo lefu na lina practicals zake.
 
Unaongelea mungu yupi huyo mwenye upendo? mungu gani huyo unayemwongelea anawaacha watu wa africa ya kusini kuuwa wenzao. Upendo gani huo anasema eti atawahukumu watu milele wakati maisha ya kuishi duniani ni chini ya miaka mia. Huoni kuwa ni kipindi kidogo sana cha kuishi?
mungu unayemtaja hapa hayupo ni elimu uliyolishwa na waleeee ili wakutawale vizuri.
 

Hakuna cha meditation, muujiza huitaji imani yako kwa yule aliyekuahidi kuutenda.
Miujiza huonyesha yenye unayemtumikia anaishi, na yupo katika utawala, ni muhimu kwa kumthibitisha mpakwa mafuta wa Mungu, kikubwa ni lazima itanguliwe na habari njema ya Kristo, angalizo :sikusema neno la Mungu, kwa sababu huwezi hubiri torati ya Musa unategemea miujiza, utakesha.
Luka 7: 19 aliwatuma kwa Bwana wamwulize: "Wewe ndiye yule
ajaye, au tumtazamie mwingine?" 20 Wale wanafunzi walipomfikia
Yesu wakamwambia, "Yohane Mbatizaji ametutuma kwako
tukuulize: Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?"
21 Wakati huohuo, Yesu alikuwa anawaponya watu wengi
waliokuwa wanateseka kwa magonjwa na waliopagawa na pepo
wabaya, akawawezesha vipofu wengi kuona tena. 22 Basi, Yesu
akawajibu, "Nendeni mkamwambie Yohane yale mliyojionea na
kuyasikia: vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma
wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini
wanahubiriwa Habari njema. 23 Heri mtu yule ambaye hana
mashaka nami!"
 
Ninaheshimu dini ya mtu yeyote. Lakini ukweli lazima tuuseme (Hakuna kitu kinachoitwa mungu wala shetani).
Unajua kifungo cha dini ni kibaya sana kuliko vifungo vyote. Ningekuomba uwe na fikra huru.

Mkuu unataka kusema hufaham chochote kuhusu shetani?
Jini jee?
 
Kuna thread hapa nitaileta inaongelea kabla ya kuzaliwa hapa duniani mtu alikuwa yukoje na baada ya kufa hapa duniani anakuwa yupoje. Nadani katika hiyo thread nitajibu maswali yako yote. Maana ni somo lefu na lina practicals zake.


Uniite plz utaitoa lini?
 

ingekuwa Mungu anawapangia watu ya kufanya,basi binadamu tungefanana na malaika na waovu wangeangamizwa,ila dunia ina mchanganyiko wa watu waovu na wema na wote wanaishi katika viwango vyote vya maisha(kuna waovu maskini na wanyonge pia wapo waovu matajiri,kuna wema matajiri na wapo wema hao hao maskini) mwanadamu kaumbwa kwa nafsi huru ambayo yeye mwenyewe huamua kuijaza na kipi aidha kuijaza na takataka kama hizo zako za kutenda miujiza,kujitukuzia uungu kwa kutenda makuu,au nafsi hiyo ikaamua kufungamana na Mwenyezi Mungu,kwamba taswira ya utukufu wa Mwenyezi Mungu ikaonekana katika maisha yetu hapa duniani,wananchi wa s.africa kuuana hilo ni kusudio la nafsi zao la kiburi na majivuno,Mwenyezi Mungu wa kweli siyo Mungu wa fujo,huonesha utukufu wake kwa kusudio maalum la kuwakumbusha wanadaam kuwa yeye ndiye wa kweli na wa pekee,rejea pale pote ambapo Mungu alijidhihirisha kwa wanadamu kwenye maandiko,alipowasaidia waisrael katika vita,alipowatoa utumwani misri na kwingine pote,kusudio ni kuwaonesha wanadamu kuwa ni yeye wa pekee,lakini hakumlazimisha mtu kumuabudu,bali kila mmoja kwa matashi yake amwabudu kwa upendo usiopimika,naomba niishie hapo,nachoka kuandika kwa kutumia simu.i
 
Mkuu unataka kusema hufaham chochote kuhusu shetani?
Jini jee?
Kweli kuna roho zipo katika ulimwengu wa roho. Lakini kwa jinsi vinavyotajwa hapa duniani wakati mwingine ni hadith. Nimeahidi katika thread inayokuja nitaongelea baada ya kufa mtu anaenda katika evolution ipi kulingana na sababu ambazo nitakuja kuzieleza na kutoa practical ili tuweze kujaribu.
 
Hahahahahaaaaaaa! :tape:

So unataka kusema wakiristo ni tatizo ila biblia iko sahihi?

Na ikiwa biblia ndio chanzo cha hayo matatizo kwanini unaitumia kama reference kusapoti madai yako????

Ivi unaichukuliaje biblia?

Ndugu maswali mazuri sana,mtoa mada anaweweseka hajui ganachokisema kama ulishasema kitu hakifahi iweje leo ukilink na mambo yako ya Education power link mambo yako na Wakina Plato,Alistoto and Newton.Hacha kutoana sisi hatuna uwezo wa kufikiri km meditation Wachina na Wajapani wanafanya sana lakini nothing new on it.Kama wewe si Mkristo na haupendi Ukristo kamwe huwezi ukatumia maandiko yke kutufundisha u west ur time.
 

Hapana hapa UMEKUFURU kabisa. The world is lead by almighty power which is God!! Kama sio hakuna binadamu angeweza kuwa na meditation power. Ulimwengu umaweza ukakuruhusu uingie kwenye ulimwengu wa kiroho kwa meditation ila huwezi fanya makuu ya kubadili maumbile au kuhamisha tungamo. unaweza kukerakera tu. HIVYO KUNA MAMLAKA ILIO JUU ZAIDI
 
Sihitaji kusubiri thread nyingine kupata majibu ya maswali madogo tu kama hayo...

Tafadhali nipatie majibu, nipo jamvini hapa 24/7...

Waiting...

Kuna thread hapa nitaileta inaongelea kabla ya kuzaliwa hapa duniani mtu alikuwa yukoje na baada ya kufa hapa duniani anakuwa yupoje. Nadani katika hiyo thread nitajibu maswali yako yote. Maana ni somo lefu na lina practicals zake.
 
Naomba unifahamishe khs your education background
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…