Jinsi ya kufungua codes za SIRI zilizoandikwa katika kitabu kiitwacho Biblia/ Neno la Mungu

Jinsi ya kufungua codes za SIRI zilizoandikwa katika kitabu kiitwacho Biblia/ Neno la Mungu

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, shalom!!

Utakubaliana na Mimi ya kuwa, ni Rahisi sana kuangalia movie masaa SITA bila kuchoka, pia ni Rahisi sana kusoma au kushinda ukichat siku nzima katika mitandao ya Kijamii ila Si Rahisi kusoma chapter angalau mbili tu katika kitabu kiitwacho BIBLIA, Je ungependa kujua nini Hasa ni sababu ya ugumu katika kusoma na kuelewa NENO lililoandikwa ndani ya kitabu hiki? Fuatana nami utajua ..

Kuanzia Leo, Ukipita Sehemu yoyote na ukasikia watu wakiomba na kunena Kwa lugha, mtu asikudanganye kuwa wale wamechanganyikiwa ,uliyechanganyikiwa ni wewe mbumbumbu ni wewe ambaye umefichwa usijue wanachoomba au kunena.

Lugha unayosikia watu wakinena Si lugha ya duniani, ni lugha ya Mbinguni, na lugha hiyo ni Siri, kuifahamu ni Hadi ufunuliwe au usaidiwe.

Najua umezoea kusikia watu wakinena Kwa lugha, lakini pia ujue kuwa lugha hiyo inayonenwa, inaandikika na kusomeka na inaweza kutafsiriwa pia.

BIBLIA yoyote iliyoandikwa na kutafsiriwa Kwa lugha mbalimbali za WANADAMU Bado haijaweza kuwa Rahisi kusomeka kueleweka kirahisi na kuandikika na kutafsiriwa na wanadamu kirahisi sababu kuu ni kuwa, codes ndani ya maandiko haya Bado ni Siri kubwa, neno Moja katika BIBLIA Huwa Ina tafsiri Saba, WANADAMU Kwa kutafuta tafuta na kuomba na kufunuliwa, wanaweza kufungua codes Moja Hadi nne pekee, zilizopaki ni za Mungu, ndio maana unaweza kusoma na ukarudia kusoma BIBLIA mara kumi lakini bado Kila ukirudi kusoma UPYA uTAENDELEA kupata vitu vipya tena na tena,kusoma BIBLIA Kwa akili Yako, jaribu usome kifungu chochote Kisha jaribu kuelewa Kwa akili Yako na kujaaribu kuitafsiri na kufafanua, utajikuta unaripuka na uelewa ambao Kila mtu karibu Yako atabaki kukushangaa, sababu kuu ni kuwa unajaribu kufungua mlango au seal bila Kodes au funguo zilizo juu kuliko ufahamu wako, hutofanikiwa zaidi ya kupotosha.

(Daniel 1: 1-31).

Palikuwa na msomi mmoja, aliyekuwa mfalme wa Babeli aliyeitwa Belshazzar, aliyeelimika Kwa kusoma Elimu uliyokuwa Bora ya wakaldayo na alikuwa na Elimu na Maarifa makubwa sana, na wasaidizi wake pia walimzunguka wenye hekima, Elimu na Maarifa ya Kila namna, na hiyo haikutosha, alizungukwa pia na wasoma nyota waliokuwa na ushirika na Roho na Ulimwengu wa Giza ambao waliweza kupata Maarifa ya kiroho yalioufaa ufalme wake katika kutafuta suluhu ya changamoto zilizoukumba ufalme wake. Hawa wote hawakuweza kusoma na kuelewa tafsiri ya neno la Siri lililoandikwa ukutani, sababu kuu ya kushindwa kufungua codes ni uchafu, dhambi, machukizo waliyonayo, Si Rahisi mzinzi, mlevi ,muazaji mtenda dhambi , mchawi nk nk asome BIBLIA na aielewe, hiyo ni impossible 🤔

Siku Moja Mfalme akayatimba, kachukua vyombo vitakatifu ambavyo vilikaa special hekaluni, Yeye akaitisha party na kuamua kuvitumia vyombo hivyo special katika kuvinywea pombe na wake zake na makahaba wake na Waganga na wachawi Ili kuifurahisha miungu yake, alivichukua Kweli na kuvitumia katika uchafu huo, kilitokea kitu Cha kushangaza kilichokata pombe yote kichwani na kumwacha kinywa wazi!!!

Kilitokea kitanga/ kiganja kilichoandika maneno ukutani na yalisomeka kama ifuatavyo;

MENE MENE TEKEL NA PERESI.

Mfalme alijaribu kusoma na asiekewe maana ya maneno Yale machache na akawaita wasomi na Waganga na wenye hekima wa wakaldayo na hakuna aliyeweza kufungua codes / Siri zile.

Ndipo alipoitwa Daniel na akawezeshwa na Roho mtakatifu kufasiri Siri zile kama ifuatavyo.

MENE MENE TEKEL NA PERESI

1. MENE.

Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha.

2. TEKEL.

Umepimwa katika mizani, nawe umeonekana kupunguza.

3.PERESI.

Ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wanedi na Waajemi.

Utaona neno Moja tu "PERESI" Lakini yametokea maneno mengi katika tafsiri ya neno Hilo.

Utaona neno Moja " MENE" tafsiri yake neno Hilo Moja yametokea maneno mengi sana ambayo Kwa nje usingejua neno Moja limenenwa kumbe limemaanisha maneno mengi ambayo ya aweza kujaza kitabu kizima.

Ndivyo ilivyo katika kusoma BIBLIA, neno au sentesi Moja usomayo, Mungu akikutafsiria, unaweza kupata tafsiri, mafunuo na mafundisho mengi ambayo Si Rahisi kuyajua usingefunuliwa.

Lugha za Mbinguni usikiazo walokole wakinena, ni Siri za Mbinguni, na Ulimwengu wa Roho wa Giza na agent wake ,wachawi wangependa na hutafuta sana kujua tafsiri ya lugha zile watamkazo na wasifahamu.

Tangu Leo ukisoma au ukifungua BIBLIA / Neno la Mungu kulisoma, omba upewe funguo ya kufungua Siri zilizomo na tafsiri zake maana kusoma BIBLIA/ NENO LA MUNGU, Ni kuongea na Mungu ambaye yu sirini, sasa Si Rahisi kumuelewa Yeye aliye ndani ya neno lake Billia.

CODES ZILIZOMO NDANI YA BIBLIA.

Kwa ufupi, Kila unachokihitaji kimo ndani ya BIBLIA, Hata kama huna wazo la Biashara, omba Kisha Fungua BIBLIA soma utakapoongozwa kusoma na utapata mafunuo nini Cha kufanya,

1. Mali na Mbinu za kutajirika kiuchumi zimo ndani ya BIBLIA Yakobo alitumia njia hiyo na kutajirika sana Kwa mifugo kuongezeka sana.

2. Ukitaka kufaulu Masomo, soma sana BIBLIA, Mimi Nina ushuhuda, nilikuwa wa kwanza darasani Kwa kusoma zaidi BIBLIA kuliko masomo ya darasani.

3. Ukitaka kufaulu katika uongozi na siasa, soma kitabu Cha Wafalme, Samuel, Waamuzi nk nk, Utashine kuliko hao wa gizani na hawatokuweza.

Kiufupi Kila kitu kimo ndani ya BIBLIA.

JINSI YA KU UNLOCK CODES ZA BIBLIA.

Tunaona Daniel, Kila alipokutana na codes, Siri alikwenda mbele za Mungu akaomba na akajibiwa na kufunguliwa na kufunuliwa na kupewa tafsiri.

Omba kabla hujasoma BIBLIA, Mwombe MUNGU akupe nguvu, hamu, Ari ya kusoma na kuelewa na kufungua codes za SIRI Ili uwe msaada Kwa wengine.

Mungu awabariki.

Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako, fuatisha Sala ifuatayo;

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU.

Aamen. Karibuni 🙏
 
Kiranga akisoma Bible huwa anaona contradictions tupu.
Bwana Yesu asifiwe Braza Kiranga.
Kusoma atasoma lakini hatofahamu.

BIBLIA kusoma BIBLIA ni sawa tu na kunena Kwa lugha au kuandika Kwa lugha za Mbinguni, wanaokuzunguka lazima waone contradiction au wakuone fyatu,

Bt vice versa is true.

Mungu atusaidie.
 
Salaam, shalom!!

Utakubaliana na Mimi ya kuwa, ni Rahisi sana kuangalia movie masaa SITA bila kuchoka, pia ni Rahisi sana kusoma au kushinda ukichat siku nzima katika mitandao...
Rabbon naomba kujua Belshaza alikufa vipi?

Maana biblia haitwambii....tunaona tu kwamna akafauawa.
 
Rabbon naomba kujua Belshaza alikufa vipi?
Maana biblia haitwambii....tunaona tu kwamna akafauawa.
(Daniel 5:30-31)

Belshazzar alipinduliwa na kuuawa na wamedi na waajemi usiku wa siku Ile Ile alipopewa fasiri ya neno lililoandikwa na kiganja ukutani.

Hawa Wafalme wa Dunia wanatamba na kujikweza Bure tu,

Yupo Mfalme wa Wafalme Yesu Kristo ambaye akiamua, ni siku moja tu unaliwa na chango, na habari inaishia pale.

Mungu atusaidie.
 
Wewe fungua code watanzania wenzako masikini kama wewe mpate hela, acha longolongo
Ndio nyinyi baadae mnaanzisha makanisa halafu mnawakamua haohao masikini wenzenu
cc mwamposa, najua yupo humo
Pole Yako,

Pesa zipo, unazitafuta za nini?

Pesa zinatafutiwa njia zije kwako, anyway ukizipata ndio inakuwaje?

Ukizipata ndio ukanunulie Malaya zikakuue? Ukazilewee Kisha ziibwe?

Huo ni ubatili mtupu na kujilisha upepo,

Mtafute Mungu Ili uwe na Amani.

Mungu akubariki, umpate Mungu na kupata kisichoharibika kidumucho milele na milele, uishi Ulimwengu huu na Ule ujao.

Ubarikiwe 🙏
 
Mkuu Rabbon sijafanya mzaha umeshauriwa Ufungue Code sisi watanzania wenzake tujikomboe kiuchumi umaskini mbaya
Sasa Kila kitu Kiko wazi ndani ya BIBLIA.

Kupata pesa Kwa njia za Mungu, kufanikiwa kiuchumi kwanza uache Ujinga,

Nenda shule pata Maarifa, epuka wizi, wizi huua baraka zako, hutofanikiwa, acha uongo na Hila, pata mtaji wa uaminifu,

Kisha Lipa ZAKA./ Fungu la kumi.

Sasa kupata pesa, kufungua Siri zilizomo ndani ya BIBLIA kupata Uchumi, pesa, utajiri mbona Rahisi sana?

Sasa ni uamuzi wako, uendelee kulalamikia,au uamue kufanikiwa kiuchumi Kwa njia za Mungu na formula ametoa kabisa,kufanya KAZI Kwa bidii, KAZI , Si ajira pekee, Bali KAZI, ni kumjaribu Kwa kulipa ZAKA/ Fungu la kumi.
 
Naamini umepita umande kidogo,

Si BUSARA Kutoka nje ya mada, jikite kwenye mada 🙏
Naona nisikukabe sana hapo, huna jibu la maandiko, unaanza porojo zako binafsi. Maswali yangu yamelenga kukufikirisha vizuri, majibu unayoyapata ukijifikiria si lazima uyaweke wazi.

Yesu alitumwa na nani?
 
Naona nisikukabe sana hapo, huna jibu la maandiko, unaanza porojo zako binafsi. Maswali yangu yamelenga kukufikirisha vizuri, majibu unayoyapata ukijifikiria si lazima uyaweke wazi.

Yesu alitumwa na nani?
Mada ya Leo inajibu swali lako vizuri sana.



( Isaya 6:1 - 10) Says:

1: Katika mwaka Ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona BWANA ameketi katika KITI CHA ENZI kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza HEKALU.

2: Juu yake walisimama maserafi, Kila Mmoja alikuwa na mabawa SITA, Kwa mawili alifunika uso wake, na Kwa mawili alifunika miguu yake, na Kwa mawili aliruka.

3: Wakaitana Kila Mmoja na mwenzake, wakisema Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa Majeshi, Dunia yote imejaa utukufu wake.

4: Na misingi ya vizingiti ikatikisika Kwa sababu ya Ile sauti ya aliyelia, nayo nyumba ikajaa Moshi.

5: Ndipo niliposema, Ole wangu Kwa maana nimepotea, Kwa sababu Mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu, MACHO YANGU YAMEMWONA MFALME, BWANA WA MAJESHI.

6: Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia,naye alikuwa na kaa la moto mikononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa Kwa makoleo Toka juu ya madhabahu.

7: Akanigusa kinywa changu Kwa kaa Hilo akaniambia, tazama, hili nimekugusa midomo Yako na UOVU wako umeondolewa, na DHAMBI Yako imefunikwa.

8: Kisha nikaisikia sauti ya Bwana akisema, NIMTUME NANI, NAYE NI NANI ATAKAYEKWENDA KWA AJILI YETU? Ndipo niliposema Mimi hapa nitumie Mimi.

9: Naye akaniambia, enenda, ukawaambie watu Hawa, FULIZENI KUSIKIA, LAKINI MSIFAHAMU, FULIZENI KUTAZAMA LAKINI MSIONE,

10: UUNONESHE MOYO WA WATU HAWA, UKAYATIE UZITO MASIKIO YAO UKAYAFUMBE MACHO YAO, WASIJE WAKAONA KWA MACHO YAO, NA KUSIKIA KWA MASIKIO YAO, NA KUFAHAMU KWA MIOYO YAO, NA KUREJEA NA KUPONYWA.


Umeelewaje CODES hizo bi faiza foxy?

Unadhani wewe uliyefunga NDOA na Ulimwengu wa Giza unaweza ambulia chochote bila kwanza kukubali kuja nuruni upewe funguo ya kufungua hizo codes?

Mungu yupo Kila Mahali, lakini hapo ameonekana Kwa Mfano wa mtu na ameketi katika KITI Cha enzi.

Na aliyemwona ni mtu, aitwaye Isaya Nabii Kwa macho ya Roho.

Unadhani Yesu utamfahamu kirahisi hivyo?

Mungu akusaidie🙏
 
Back
Top Bottom