Jinsi ya kufungua codes za SIRI zilizoandikwa katika kitabu kiitwacho Biblia/ Neno la Mungu

Sio kwamba kuna code zimefichwa, ila inahitaji utulivu na umakini ili kuelewa vyema, Hakuna sababu ya Mungu kuficha ujumbe wake kwa watu wake
(Zaburi 53:2-3)

"Toka Mbinguni, Mungu aliwachungulia WANADAMU, Ili aone ikiwa yupo mwenye akili amtafutaye Mungu".

Sasa utaona kuwa Mungu yupo sirini, anataka tumtafute.

Pia kumbe kumtafuta Mungu ndio kuwa na " Akili".

Sasa usipomtafuta Mungu utakosa akili ,BUSARA na Maarifa.
 
We mburura kweli kwahiyo andiko hilo ndio linasema Yesu ndio Mungu?

Neno Ili lipatikane lazima awepo aliyelitamka hilo NENO ambaye ndio Mungu muumba wa Kila kitu

Ukisema Yesu ametokana na neno la Mungu ni sawa maana Mungu ameumba vitu vyote Kwa kutumia neno lake

Ukisema labda mimba Yesu imepatikana Kwa neno la Mungu basi tambua kuwa hata mimba ya Isaka ilipatikana pasipo kushiriki tendo la ndoa kati Ibrahim na Sara Mungu tu alisema Sara akapata mimba

Nyinyi wagalatia sijui mnakwama wapi
 
Usitumie hiyo Elimu ya la Saba A kujaribu kufungua codes za Billia, hutoweza zaidi ya kupuyanga. Hata Elimu ya PHD Bado ni ndogo mno kutumika kuzijua Siri ndani ya maandiko.

Isaka alipatikana Kwa njia ya kawaida ya mume na mke Si vinginevyo, maandiko Yako wazi kabisa.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake, Amen
 
Wewe fungua code watanzania wenzako masikini kama wewe mpate hela, acha longolongo
Ndio nyinyi baadae mnaanzisha makanisa halafu mnawakamua haohao masikini wenzenu
cc mwamposa, najua yupo humo
Ukishapata pesa iweje? umeshawah waza, ukiwa na pesa nyingi ndo itakuwaje? utashangaa unawaza uovu tu, uwe na pesa ili uwe na uwezo wa kulala na kila mwanamke unayemtaka
 

Wagalatia 4:21
Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria?
Wagalatia 4:22
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.
Wagalatia 4:23
Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi.

Hata huyo Paulo aliyekuletea dini ya ukristo anajua kuwa Isaka amepatika Kwa neno la Mungu na Wala sio Kwa tendo la ndoa tena hayo Maneno Paulo amenukuu katika Taurati

Sasa yawezekana wewe unajua zaidi kuliko Paulo aliyekuletea dini ya ukristo

Weka hilo andiko hapa linalosema Isaka amepatikana Kwa tendo la ndoa kati ya Ibrahim na Sara

Ili tuone kuwa mmepotea Kwa sababu bibilia Ina code au mmepotea Kwa ujinga wenu wenyewe
 
Asante nakubaliana na karibia vyote ulivyosema ila kunena kwa lugha na lazima kuwe na mtafsiri, sasa walokole wamefanya fasheni kila mtu anajinenea maneno ambayo hakuna anayeweza kutafsiri


Ukimuuliza umeongea nini hajui, sasa kuna haja gani ya kuongea lugha ambayo mnaita ya kimbingu ilhali haimfikii yule msikilizaji

Haya msingi wa kushuka kwa roho mtakatifu siku ya pentekoste na kunena kwa lugha ilikuwa kwenda kuhubiri injili sehemu ambazo hawazijui lugha yao na wakaweza kunena bila kufundishwa yani leo uende kwa wayao hukijui lakini ukizungumza wanasikia kiyao pure

Tukirudi kwa Daniel aliweza kutafsiri maneno yaliyoandikwa ukutani kwa uweza wa roho mtakatifu, ni kweli.

Vipi nyie walokole wa leo??? Mnasema kunena kwa lugha ni mpaka ushushiwe sio kila mtu ananena ila ukifikia kiwango fulani cha imani unashushiwa

Mbona mlioshushiwa na mnaweza kunena kwa lugha hamuwezi kutafsiri anachonena mwenzenu ilhali wote mna uwezo huo???

Ndio ujue sio kweli, na ndio maana baadhi ya Makanisa mfano Sabato hawana masuala ya kunena kwa lugha sababu wanatambua mibaraka hiyo ipo na kweli kwa uweza wa Roho mtakatifu unaweza kushushiwa karama hiyo lakini ni lazima uweze kutafsiri unachoongea

Na sio kupiga kelele kama chizi
 
Shalom
Kuna kitu aidha umeruka au umesahau....jaribu kufuatilia Codex Vaticanus ( C.325 _350 )
 
Mimi ninachojua huwez kumjua Mungu zaid vile yeye amekupangia kumjua. Hata katika levels za manabii mitume nk kila mtu anamjua Mungu katika ile level ya Mungu aliyoruhusu wewe umjue. Ndio maana unasikia Mungu wa Eliya nk. So maandiko yametoa mwanga kwamba tafuteni mtapata bisheni mtafunguliwa na ombeni mtapata. Kila kitu kiko juu yako kanuni yoyote unayotumia hapo juu kwa kudhamiria utafanikisha hitaji lako. Lakini pia Mungu anasema anitafutae kwa bidii ataniona hii inamaana chochote unachotaka ukiweka bidii utafanikiwa iwe ni mbingu pesa au chochote ni wewe tu udhamirie kukata sharing. Halafu la msingi kujua ni kuwa huyu Mwenyezi Mungu tunaemzungumzia tunamjua kwa asilimia ndogo sana tena sana mno. Tumepewa tu siri kidogo kuhusu Mungu na mbingu yake lakin ukweli ni kama hatumjui kabisa tunamjua kidogo sana. Ndio maana tumekariri watu wanaoweza kutufundisha kumhusu Mungu ni viongoz wa dini. Ukweli ni kwamba hekima ya Mungu haichunguziki anaweza kumtumia hata malaya kukuletea habar njema ya ufalme so kikubwa biblia inatuambia tuwe tayar muda wote tusali na kufunga na kuwasaidia wengine wasio na msaada. Kumbuka nimekuambia kanuni ni tatu tu. Tafuten mtapata
Bisheni mtafunguliwa
Na ombeni mtapewa. Hii kanuni ni kwa binadamu yeyote. Unaweza kujiuliza hiv wale wenye uhai wanne walioketi na Mungu kwenye kiti cha enzi ni akina nani maana hatujaambiwa ni malaika wala binadamu. So ukijiuliza hili swali ndio utajua Mungu tunaemzungumzia ni zaid ya tumjuavyo. Kuna viumbe wengi tu na kama vile Yesu alivyotuambia kwa Baba yake kuna makao mengi ingekuwa sivyo angetujulisha so tukazane kuombe na kujichunga na dunia pasipo mawaa. Ni suala la kufa na kupona.
 
Mungu ni Neno+Mungu ni roho= Neno ni Roho ...huwezi kuelewa vya rohoni kama haupo kiroho, bila uwezesho wa Roho Mtakatifu Biblia nikama kitabu cha stor tu

Kuna tofauti ya Biblia na Biblia takatifu. Kila mtu anaweza kusoma Biblia, hata waganga sikuhizi wanakiwa nazo, hata wanaobishana wanazo...lakini sio kila mtu anaweza kusoma Biblia Takatifu
 
Ikiwa Yesu ni Mungu. Je? Nabii Adam au( Adamu) atakuwa nani?Wakati ndio kiumbe cha mwanzo kuja duniani na Hawa. Yesu Alikuwa wapi.?Mwenyezi Mungu wetu sisi Waislamu hakuzaa wala hakuzaliwa yupo hayi wala hafi (ALLAH)
 
(Mwanzo 15:4).
Ndipo neno la BWANA lilipomjia " Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, Bali mwana atakayetoka KATIKA VIUNO VYAKO mwenyewe ndiye atakuwa mrithi wako.

Karibu🙏
 
(Waebrania 11:11).

Kwa Imani hata Sara mwenyewe ALIPOKEA UWEZO WA KUWA NA MIMBA alipokuwa amepita wakati wake, Kwa kuwa alimheaabu Yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.
 
Ikiwa Yesu ni Mungu. Je? Nabii Adam au( Adamu) atakuwa nani?Wakati ndio kiumbe cha mwanzo kuja duniani na Hawa. Yesu Alikuwa wapi.?Mwenyezi Mungu wetu sisi Waislamu hakuzaa wala hakuzaliwa yupo hayi wala hafi (ALLAH)
Hata Yesu Hana baba wa mwili Wala mama. Alijiumba ndani ya tumbo la Mariamu akawa kama mwanadamu.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake.

Amen
 
Nipe code za utajir wavuv campu wanikome
 
Ni Kweli, HEKIMA za Mungu hazichunguziki,

Pia Mungu ametutaka tumtafute na kumjua Kwa bidii Kwa kusoma neno na kulitafakari mchana na usiku.

Asemapo hachunguziki, amaanisha kumchunguza na kumtafuta Kwa kutumia akili za kibinadamu bila kuomba kufundishwa na Yeye mwenyewe kupitia Roho mtakatifu.

Ubarikiwe 🙏
 
Nipe code za utajir wavuv campu wanikome
Takasa mwili wako kwanza,

Jitenge na zinaa, acha ulevi, uongo wizi na Kila machukizo,mdomo wako unene Kweli.

Mpokee Yesu kuwa BWANA na MWOKOZI WA MAISHA Yako, akupe uwezo wa kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu.

Hatua inayofuata, Lipa ZAKA Fungu la kumi katika mapato Yako, ukifanya hivyo utapokea ulinzi wa pesa Yako na mifuko iliyotoboka itazibwa, magonjwa, HASARA vitaondoshwa.

Na kuanzia hapo HUTAPUNGUKIWA.

Ubarikiwe 🙏
 
Kwako ni Rahisi kumuamini mganga anapoongea na Mizimu Kwa lugha ya kipepo au Mizimu,

Lakini ukiambiwa walokole hunena Kwa lugha ya Mbinguni unakataa.

Ingekuwa na Maarifa kidogo, ungefanya Utafiti Si kubisha usichokijua.

Pole sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…