Nimeshuhudia ASAS Djibouti, KMC na hata JKT wote wakicheza mpira unaofanana walipocheza na Yanga ambao umesababisha wakaadhibiwa vibaya. Leo nitatoa maoni yangu kwa timu zingine zitakazokuja kucheza na Yanga siku, wiki na miezi inayokuja nini wanatakiwa wafanye ili wapate matokeo.
Kwanza punguzeni pasi za kurudisha mipira nyuma (backpasses). Yanga ni timu ambayo sasa hivi inazingatia sana kukaba sana na wanakaba kwa ile filosofia ambayo kocha wa Simba Robertinho amekuwa anaiongelea sana, kukabia kutokea juu. Maana yake timu pinzani zinapata ugumu wa kufikisha mipira hata katikati ya dimba. Tumeshuhudia KMC hawakupiga shuti hata moja on target wala off target langoni kwa Yanga kwa dakika zote 90. Sasa cha kushangaza pamoja na ugumu huu, timu zote hizi zilizofungwa zilikuwa na tabia wanaweza kufika katikati ya uwanja au kunyang'anya mpira kutoka kwa mchezaji wa Yanga, ila badala ya kuongeza pressure kwenda mbele wanarudi nyuma, matokeo yake unashindwa tena kufika hata kati kabla ya kupokonywa mipira. Jana JKT kila walivyokuwa wanarudisha mpira nyuma nilikuwa nasema hawataweza tena kuufikisha tena kati kabla ya kuupoteza na kweli ilikuwa hivyo. Ukiangalia ASAS walipojaribu kupress mwishoni mwa kipindi cha kwanza kama nakumbuka vizuri, kidogo walionekana kusumbua ila hawakuwa na muendelezo huo wakaishia kufanya hayo niliyosema hapo juu. Hili nalisisitiza sana maana ndiyo tatizo sugu.
Pili, acheni kucheza vipasipasi visivyo na maana mkiwa eneo lenu la ulinzi. Focus kwenda mbele haraka inavyowezekana. Afadhali uoshe halafu mpira upotee kwenye final third ya mpinzani kuliko upotee kwenye eneo lenu la ulinzi. Jambo rahisi kulielewa lakini inashangaza timu nyingi zinashindwa kulitekeleza.
Tatu, labda kama timu yako ina wachezaji kama Denis Kibu wanaoweza kupambania mipira mirefu ya juu na kuishinda, epuka kucheza mipira mirefu ya kugombania. Asilimia 98 ya mipira yote mirefu ya JKT ilikuwa inapotea. Cheza mpira wa chini wa kwenda mbele ukzingatia jambo la kwanza nililosema. Kwa kiasi kikubwa inavyowezekana mipira mirefu ya juu labda iwe ya kona, krosi au faulo. Kwa viwanja vya mikoani vyenye milima na mabonde, timu zote mbili zinapata shida kucheza mpira wa chini kwa hiyo mipira mirefu inaweza kutumika.
Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, wiki 2 kabla ya mechi nyang'anya simu wachezaji wenu au kama kuna uwezo monitor mawasiliano yao yote. Kinga ni bora kuliko tiba.
Ila najua haya mawazo wala hayatazingatiwa maana hivi vitimu wala havijitambui. Hivi wewe mchezaji wa Jeshi la Kujenga Taifa unasukumwa na mtu kama Musonda halafu unanyong'onyea?