[emoji23][emoji23]Ukitaka kuifunga Yanga msimu huu,hakikisha unaanza mechi DAKIKA 45 kabla ya muda kamili..
Yaani mechi ikianza saa moja jion wewe Anza mechi saa 12 cheza peke Yako funga magoli ya kutosha...mechi ikianza uwe unaongoza GOLI 5 hivi
Wamefika sana eneo la ulinzi la yangaJana JKT walikuwa na shot on target 1, acha kupotesha eti dk zote 90 hamna short on target.
Swali, kwann kwenye mechi ya Ngao huyo Robertinho alishindwa kuikabia Yanga juu? Muda wote team ikawa nyuma inazuia??Nimeshuhudia ASAS Djibouti, KMC na hata JKT wote wakicheza mpira unaofanana walipocheza na Yanga ambao umesababisha wakaadhibiwa vibaya. Leo nitatoa maoni yangu kwa timu zingine zitakazokuja kucheza na Yanga siku, wiki na miezi inayokuja nini wanatakiwa wafanye ili wapate matokeo.
Kwanza punguzeni pasi za kurudisha mipira nyuma (backpasses). Yanga ni timu ambayo sasa hivi inazingatia sana kukaba sana na wanakaba kwa ile filosofia ambayo kocha wa Simba Robertinho amekuwa anaiongelea sana, kukabia kutokea juu. Maana yake timu pinzani zinapata ugumu wa kufikisha mipira hata katikati ya dimba. Tumeshuhudia KMC hawakupiga shuti hata moja on target wala off target langoni kwa Yanga kwa dakika zote 90. Sasa cha kushangaza pamoja na ugumu huu, timu zote hizi zilizofungwa zilikuwa na tabia wanaweza kufika katikati ya uwanja au kunyang'anya mpira kutoka kwa mchezaji wa Yanga, ila badala ya kuongeza pressure kwenda mbele wanarudi nyuma, matokeo yake unashindwa tena kufika hata kati kabla ya kupokonywa mipira. Jana JKT kila walivyokuwa wanarudisha mpira nyuma nilikuwa nasema hawataweza tena kuufikisha tena kati kabla ya kuupoteza na kweli ilikuwa hivyo. Ukiangalia ASAS walipojaribu kupress mwishoni mwa kipindi cha kwanza kama nakumbuka vizuri, kidogo walionekana kusumbua ila hawakuwa na muendelezo huo wakaishia kufanya hayo niliyosema hapo juu. Hili nalisisitiza sana maana ndiyo tatizo sugu.
Pili, acheni kucheza vipasipasi visivyo na maana mkiwa eneo lenu la ulinzi. Focus kwenda mbele haraka inavyowezekana. Afadhali uoshe halafu mpira upotee kwenye final third ya mpinzani kuliko upotee kwenye eneo lenu la ulinzi. Jambo rahisi kulielewa lakini inashangaza timu nyingi zinashindwa kulitekeleza.
Tatu, labda kama timu yako ina wachezaji kama Denis Kibu wanaoweza kupambania mipira mirefu ya juu na kuishinda, epuka kucheza mipira mirefu ya kugombania. Asilimia 98 ya mipira yote mirefu ya JKT ilikuwa inapotea. Cheza mpira wa chini wa kwenda mbele ukzingatia jambo la kwanza nililosema. Kwa kiasi kikubwa inavyowezekana mipira mirefu ya juu labda iwe ya kona, krosi au faulo. Kwa viwanja vya mikoani vyenye milima na mabonde, timu zote mbili zinapata shida kucheza mpira wa chini kwa hiyo mipira mirefu inaweza kutumika.
Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, wiki 2 kabla ya mechi nyang'anya simu wachezaji wenu au kama kuna uwezo monitor mawasiliano yao yote. Kinga ni bora kuliko tiba.
Ila najua haya mawazo wala hayatazingatiwa maana hivi vitimu wala havijitambui. Hivi wewe mchezaji wa Jeshi la Kujenga Taifa unasukumwa na mtu kama Musonda halafu unanyong'onyea?
Sina uhakika kama unalosema ni sahihi ila wakati mwingine kocha anaamua kutumia mbinu tofauti na unayoitegemea. Ni sehemu ya kumvuruga mpinzani wako.Swali, kwann kwenye mechi ya Ngao huyo Robertinho alishindwa kuikabia Yanga juu? Muda wote team ikawa nyuma inazuia??
Hesabu zako zimekaa kama zile za kuuza matikiti ili uwe bilionea.Hii ni ela kwako ndugu mchambuzi, nenda kwa kila klabu waambie kuwa una mbinu ya kuifunga Yanga. Kisha kwenye mechi dhidi ya Yanga wewe ndio uwe sehemu ya mtengeneza mipango ya ushindi na uwaambie kabisa ukishinda wakupe nini na ukifungwa wakufanye nini. Kuna mechi 30 zitakazochezwa dhidi ya Yanga, kama kila mechi utalipwa 200,000 mfano basi kwa mechi 30 una 6,000,000/= nenda kaombe kibarua cha kukabiliana na Yanga. Kama unaona mpira ni kama hesabu za kuhesabu na vidole.
Kuepuka hujma zozote zinazoweza kufanyika. Kama nilivyomalizia "kinga ni bora kuliko tiba"Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, wiki 2 kabla ya mechi nyang'anya simu wachezaji wenu au kama kuna uwezo monitor mawasiliano yao yote. Kinga ni bora kuliko tiba.
Ndugu mtoa post naomba ufafanuzi kidogo kwenye hayo maelezo yako hapo juu. Kwanini wachezaji wachukuliwe simu zao tena wiki mbili kabla ya kucheza na Yanga?
Point nzuri nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa ila hizi timu hazikukaa nyuma kihivyo. Wangepaki basi tusingeona Yanga wakiwa na uhuru vile kupenya katika ngome zao. JKT walikuwa wanacheza mpira wa wazi ila wa kukamia.Yanga ni timu inayopenda kushambulia, Ina mabeki was pembeni wenye Kasi na wanaopenda kupanda na kuanzisha mashambulizi. Kmc na Jkt wore walicheza mchezo unaofanana yaani kukaa nyuma. Madhara ya mchezo huo ni kuruhusu muda wore mpira kuchezwa golini kwako.
Unawazuiaje, njia pekee ni kuhakikisha unakuwa na mawinfa wenye Kasi na kushambulia ilu usiwape nafasi mabeki wao kupanda na kuanzisha mashambulizi.
Maanake haujiamini kuhusu mbinu yako. Kama unajiamini jilipue kaombe kazi ya ukufunzi wa kuifunga Yanga.Hesabu zako zimekaa kama zile za kuuza matikiti ili uwe bilionea.
Hakika huyu mtu ni [emoji91]Job ni mtu na nusu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ngao imebebwaa.Kuifunga Yanga ya sasa na kuondoka na Ushindi ni jambo gumu sana
Labda itokee katimu kabahatishe kuifunga kwa Penalties kama ilivyotokea kwa Simba na kipa wao wa kutokeza
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na bado mkakosa Ngao. WoiiiihUmeongea vyema. Ila kwa mtizamo wangu, timu inayoshambulia mwanzo mwisho ni ngumu kuihimili kama na ww hauishambulii kurudisha nyuma wingback zake pamoja na viungo.
Kwa style ya uchezaji wa yanga wa sasa itaimudu pekee timu ambayo ni giant yenye wachezaji wazuri ambao wataweza kupishana na yanga bila shida na kuilazimisha yanga kurudi nyuma ikishambulia kwa kwa umakini.
Mfano Azam aliamua kutumia misuli na miguvu bila akili mwishowe akapasuka. Simba nae aliamua kupak bass huku akisukuma counter attack ingawa yanga alishindwa kupata goli.
Ngao mliporwaa juzi tyuuh hapa, 2012 tuliwashona 5 kwa bila, had leo hamjalipaaa.Makolo wajipange sana wakija hovyo wanapigwa 8 otherwise watakula Mkono.
Kwenye makocha waimarishe pia,Gamondi huwezi fananisha na kocha km Jkt Tanzania, Ki mbinu ,ki exposure ,Hayo hayatoshi kama ndani ya uwanja unafanya makosa ya msingi huku kocha amebaki kujikunyata kwenye benchi ameshika kichwa tu
Hapo bila mbinu na uwezo lzm muonekane vibondeUjawaambia wamkabe nani😅
Yaoyao
Pacome
Max
Key
Mudathiri
Aucho
Musonda
Mzinze
Konkoni ..
Utawachagulia wakumkaba afu uwalete wapigwe holaaaa 5