SoC04 Jinsi ya kujenga taifa na jamii yenye maendeleo endelevu bila kuvunja misingi na miiko ya jamii na taifa

SoC04 Jinsi ya kujenga taifa na jamii yenye maendeleo endelevu bila kuvunja misingi na miiko ya jamii na taifa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kesenda

New Member
Joined
May 18, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Kama inavyoaminika katika Taifa lolote lolote misingi ya maendeleo hutokana na uwepo wa rasilimali zilizopo kwenye Taifa hilo,Taifa misingi yake ni Jamii zinazolizunguka taifa hilo, hivyo Uimara wa taifa hutegemea uimara wa jamii zinazolizunguka,Taifa lolote ili liitwe taifa ili liweze kuendelea hutegemea sana matumizi ya rasilimali zake muhimu kama vile watu,maliasiri, taarifa na fedha zinazopatikana kutokana na kodi,hivyo kabla ya ngazi ya taifa siku zote lazima jamii za taifa hilo zijengewe misingi imara,misingi imara ya taifa lazima ifanyiwe marekebesho na marekebisho hayo yasimamiwe ili kuleta tija kwa Taifa,hivyo basi Taifa letu linahitaji mabadiliko katika secta zifuatazo,

Elimu
Elimu,elimu inatafsiliwa kama urithisaji wa maarifa kutoka kizazi hadi kizazi,elimu ni kati ya vipengele muhimu kwa ustawi wa jamii na taifa kwa sababu ni kiini ya watu kujitambua kama taifa linataka kutoa elimu yenye tija kwa maendeleo endelevu lazima elimu iendane na mazingira ya jamii na taifa kwa kuangalia rasilimali zilizopo kwenye taifa, kwa mfano kama taifa ni wazalishaji wa madini elimu ijikite katika madini ili taifa liwe na wataalamu wa ndani kwenye Kipengere cha madini

Elimu ya fedha, Kati ya vitu vinavyosumbua vijana hasa wa taifa hili ni ukosefu wa elimu ya fedha na hii ni kutokana na kutokua na elimu sahihi juu ya utafutaji,matumizi na uhifadhi wa pesa hili linaghalimu taifa kwani vijana hugeuka kuwa tegemezi baadala ya kuwa msaada kwa Taifa,pendekezo langu ni kuwa serikali iangalie namna bora ya utoaji wenye tija kuhusu fedha vijana wengi hupata fedha ila hawana mipango juu ya maisha yajayo,kuwapatia elimu itawajenga watu wenye uelewa kuhusu umiliki wa fedha itatoa fursa kwa taifa kujipatia kodi na kupunguza wategemezi na makundi haramu

Elimu ya uzalendo,bendera ya taifa kama kiwakilishi cha utaifa elimu ya namna bora ya kupambana na rushwa, kwa ujumla ni elimu ya kulitambua na kuthamini taifa letu na watu walione kama zawadi ya kipekee inayopaswa kutunzwa ukizingatia kwamba huna taifa Lingine, hili litasaidia kujenga taifa lenye umoja na mshikamano ambapo ndio msingi wa maendeleo ya kweli elimu hii itawajengea uwezo wa kujitambua kama taifa na kujithamini pamoja na kuthamini vya kwetu.aidha napendekeza elimu hizo zifundishwe kwenye mashule msingi na sekonndari na vyuoni.

2) Vyombo vya Habari
Mabadiliko kwenye Kipengere utoaji na upokeaji taarifa,taarifa ni kiungo muhimu kuanzia ngazi ya familia,taasisi,jamii na taifa katika mienendo ya ujenzi wa jamii imara taarifa ndio huweza kupelekea maendeleo kwani hata taasisi ili iendelee lazima wazingatie taarifa zinazotolewa na kuzifanyia kazi. Pendekezo langu ni kuwa serikali ijenge misingi imara ya utoaji na upokeaji taarifa na ili kujenga taifa imara na endelevu lazima serikali Ijengee vyombo vya Habari misingi ya uhuru ili kuepuka uandishi wa kikasuku ambao hauna tija kwa maendeleo ya taifa misingi imara iitaifanya Jamii kuiamini serikali na kuendelea kudumisha upendo usio na kikomo, ikumbukwe kuwa amani hujengwa na uwazi na kuaminiana hivyo ikiwa misingi ya utoaji na upokeaji taarifa haitakua imara huibua watoa taarifa wasio rasmi wanaoweza kuchafua amani ambayo ndio tunu tuliyonayo.

3)demokrasia na siasa

Kujenga demokrasia ya kweli na kupunguza ukasuku,tunaishi kwenye jamii ambayo utawala unategemea demokrasia ila demokrasia katika nchi za kiafrika imepelekea machafuko katika nchi mbalimbali kutokana na kutotumiwa vyema, baadala yake hutumiwa na watu walafi wa madalakacmckuleta machafuko, ujenzi wa demokrasia ya kweli itapelekea taifa kuwa na usemi mmoja na kuzuia machafuko kutoka kwa watu wenye nia ovu na Taifa letu, kujenga weredi kwa vijana wenye nia njema na uelekeo wa siasa kutasaidia pia kujenga siasa zenye tija na kupunguza siasa za chuki,hali hii itapunguza machafuko ambayo ni chanzo cha uchumi kuporomoka

Kipendele kingine ni katika mihimili ya kiserikali kwa maana ya bunge,Rais,na mahakama kikatiba mihimili hii kila muhimili ni kamilifu na haipaswi kuingiliwa kimamlaka na lengo kubwa la uundwaji ni kusimamiana katika utekelezaji wa maamuzi,hivi leo vyombo hivi havifanyi kazi kikatiba bali kwa matakwa ili kujenga jamii endelevu kama taifa lazima wafanye majukumu yao kwa kufuata katika.

4) UCHUMI, Uchumi ndio kiini cha taifa lolote ikitegemea na muundo ulioowekwa na taifa hilo,ili kujenga uchumi imara ni vyema serikali itengeneze mfumo mzuri wa taifa kujitegemea taifa lazima litengeneze uchumi shirikishi dhidi yake na wananchi pendekezo langu ni kwamba serikali itengeneze ushirikishi katika sehemu zifuatazo, kodi, udhibiti wa mianya ya rushwa hili itatoa mwanya kwa ujenzi wa taifa imara mfano wananchi wengi hasa wafanyabiashara wanalalamika kuhusu kodi kandamizi hivyo hununua bidhaa nje ya nchi kuleta ndani ya nchi huku ni kujenga taifa jingine kama taifa tunapaswa kutengeneza sera rafiki za utozaji kodi ili kutoa fursa kwa wananchi kufanya biashara ndani na kutumia bandari yetu kuleta mizigo

Katika udhibiti wa mianya ya rushwa ushirikishwaji wa wananchi kikamilifu ni muhimu mfano wananchi hununua bidhaa kwa bei ya juu ila risiti za EFD huwa na kiwango kidogo kuliko kilichoannunuliwa hupelekea mapato kupotea kutengeneza mfumo shirikishi utasaidia kuimarisha uchumi

Katika mambo yote ujenzi wa taifa endelevu hutegemea misingi ya utawala bora ikiwemo uwajibikaji,Uwazi,Misingi bora ya demokrasia,na uhuru wa vyombo vya habari
 
Upvote 2
,Taifa misingi yake ni Jamii zinazolizunguka taifa hilo, hivyo Uimara wa taifa hutegemea uimara wa jamii zinazolizunguka
Hakika, umenena mtu mmojammoja na kisha taifa kwa ujumla.

kwa mfano kama taifa ni wazalishaji wa madini elimu ijikite katika madini ili taifa liwe na wataalamu wa ndani kwenye Kipengere cha madini
Sawa.

Elimu ya uzalendo,bendera ya taifa kama kiwakilishi cha utaifa elimu ya namna bora ya kupambana na rushwa, kwa ujumla ni elimu ya kulitambua na kuthamini taifa letu na watu walione kama zawadi ya kipekee inayopaswa kutunzwa ukizingatia kwamba huna taifa Lingine, hili litasaidia kujenga taifa lenye umoja na mshikamano ambapo ndio msingi wa maendeleo ya kweli elimu hii itawajengea uwezo wa kujitambua kama taifa na kujithamini pamoja na kuthamini vya kwetu
Bado ninatafuta ile formula au 'recipe' ya kujenga hiki kitu. Yaani sijui ni media, au tuwe na adui mmoja kama mwamba alivyotutengenezea adui 'Mabeberu'.🤫🤔. Think tank ya taifa ijipange asee itupatie majibu.

serikali Ijengee vyombo vya Habari misingi ya uhuru ili kuepuka uandishi wa kikasuku ambao hauna tija kwa maendeleo ya taifa misingi imara iitaifanya Jamii kuiamini serikali na kuendelea kudumisha upendo usio na kikomo, ikumbukwe kuwa amani hujengwa na uwazi na kuaminiana
Hakika

hununua bidhaa nje ya nchi kuleta ndani ya nchi huku ni kujenga taifa jingine kama taifa tunapaswa kutengeneza sera rafiki
Kuwapa ajira vijana wa nchi nyingine na huku wetu wanalia ajira.

Katika mambo yote ujenzi wa taifa endelevu hutegemea misingi ya utawala bora ikiwemo uwajibikaji,Uwazi,Misingi bora ya demokrasia,na uhuru wa vyombo vya habari
Hakika
 
Back
Top Bottom