Jinsi ya kujitoa Mange Kimambi app

Jinsi ya kujitoa Mange Kimambi app

Ukashangaa nini? Ungeuliza pengine wana sababu za msingi. Hata mimi nilikuwa na hiyo app na nilikuwa nime-subscribe kulipia kila mwezi lakini sasa nimejitoa. Kilichofanya nijiunga ni kum-support Mange mwenyewe kwa kupigana vita vya mtu mmoja, bila woga kipindi cha udikteta wa Magufuli. Na juzi juzi pia alipopinga mama Abdul kumilikisha bandari zetu kwa waarabu. Kwa sasa nimejitoa kwa sababu kaacha kuanika uovu wa viongozi. Akirudia tena na mimi nitajiunga tena.
Ninachoshangaa ni vile wanakuwa nayo halafu wanajifanya hawana, yaani wanajifanya hawamfatilii mange kutwa kumponda. Huo unafiki ndo unanishangaza...otherwise kila mtu afate anachotaka
 
Nyuzi za "Mji Mzito" za Marehemu yule zilikuwa zinatembea ile mbayaa..

Hiyo yote ina maanisha 99% za wana jf wanapenda udaku...

Hata hiyo Mange Kimbambi App 90% humu wanayo, sema publicly wanajibaraguza, BTS wanayo sanaaa, vpn zinawashwa kwa kwenda mbelee..
Niliwahi kusema hii....

Au mtu anakuambia sija'mfollow Mange....Wakati page yake siyo Private..hivyo umfollow usimfollow utaingia na utasoma Udaku wote....
 
Wakuu za asubuhi
Nimejaribu bila mafanikio kujitoa kwenye hii app. Nimewasiliana na wao sipati msaada. Hawana majibu. Benki niliyojisajilia wanasema solution ni.kubadili kadi ya benki. Hivi kweli hadi nibadili kadi?

Kila mwezi nakatwa tsh 2300/- automatically. Sijui nilifanyaje. Nikitaka kufuta akaunti yangu inashindikana. Maelezo niliyopewa kama nilijisajili kupitia app store basi niingie huko nikiona hiyo app ni unsubscribe. Wala sijaiona. Mange mwenyewe hajibu meseji zangu kupitia platform zake. Nia yangu niachane na hiyo app tu kwa sasa. Wazee wa tech tafadhali

Updates
Nimefanikiwa kujitoa kwenye usajili husika. Kwa namna ya pekee napenda kuwashukuru Nobunaga na Dr Restart kwa ushirikiano wao na kuonyesha kujali.

Nimejifunza:
1. Humu JF kuna watu wajinga sana. Nawaombea wasifike hatua ya kuwa wapumbavu
2. Wema bado wapo ila wachache
3. Wengi humu wanapenda mada nyepesi nyepesi wakitumia mgongo wa u great thinker
4. Wengi humu wana stress/msongo. akipata upenyo wa kutoa stress zao wanabwaga tu nyongo. Inajionyesha kwenye post zao

Mwisho, MODS naomba muufute huu uzi. Si lengo langu kuharibu biashara ya mtu bali wao wenyewe walishindwa kutoa mwongozo wenye kueleweka. Hivyo basi Active Boqin BlackBold na wengine tafadhali futeni huu uzi
Aise yani unatoa na hela kabisa kufuatilia umbea maisha ya watu ,halafu inakusaidia nini kuinua maisha yako ukishajua aibu za wenzako
 
Gharama ya umbea kwa 2,300 unalalamika? hapo hutoki ng'oo na tumeboresha mitambo yetu hakuna mtu kutoka, ndio ukome sasa kufuatilia umbea
[emoji16][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom