Maulaga59
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 2,984
- 2,971
Barua imesema "ikiwemo kima cha chini" na sio "ni kwa kimo cha chini" maana yake ni wote, soma paragraph ya kwanzaView attachment 2224480
Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%
Thread starterFumadilu Kalimanzila Start date57 minutes ago Tags asilimia kubeba mapato mishahara ongezeko tanzania
1 of 3
Next
Last
F
Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
57 minutes ago
#1
Ukisoma vizuri kitabu cha WHY NATIONS FAIL ( The Origins of Power,Prosperity & Poverty) cha DARON ACEMOGLU na JAMES A.ROBINSON utajua kwa uhakika ni kwa nini Tanzania yetu ni masikini hivi na itachukua muda mrefu kubadili hali hii.
Kwa ufupi ni kwamba tunacho kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya maendeleo katika Nchi yetu kasoro watu wenye maarifa na taasisi imara.
Hata watu wachache wenye maarifa tulionao pia wana maarifa yaliyopitwa na wakati (obsolete) au waliyo karirishwa tu! Tunaweza kusema maarifa yao hayo ni USELESS KNOWLEDGE tu.
Nchi bila uzalishaji na kuingiza Nguvu kazi kubwa katika uzalishaji ili kuongeza tija ni kazi bure tu.
Viongozi wetu na wachumi wetu waliwasoma akina Adam Smith kwenye THE WEALTH OF NATIONS kwa ajili ya kukariri kujibia mitihani tu!
Watu wetu hata wasomi wakubwa hawajui kutafsiri hata vitu basic kabisa!
Watu wanaambiwa kima cha chini la Mshahara kimeongezeka kwa asilimia 23.3% ,wao wanakimbilia Rais ameongeza Mishahara kwa asilimia 23.3% ( akili za Ki- Mwijaku Mwijaku)!
Jiulize kwanza kama Mishahara itaongezwa kwa asilimia 23.3% yote ,Wage Bill yetu itakuwa Shilingi ngapi?!
Wage Bill ikifika bilioni 900 kwa mwezi na madeni tunayolipa kwa mwezi ni bilioni 900 wakati Mapato yetu kwa mwezi Trilioni 1.5 ( bilioni 1500) Nchi itakwendaje?!
Ukitaka kujua Nchi hii ina tatizo kubwa katika Wealth Creation angalia utitiri wa tozo katika mafuta!
Kwahiyo ukifuatilia sasa mjadala ni asilimia 23.3% ya ongezeko la Mishahara ni kwa kima cha chini pekee au Mishahara yote!