bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,213
- 2,938
JINSI YA KULIFANYA JOKOFU (FRIDGE) LAKO LIDUMU MIAKA 10+
Watu wengi hununua friji na kuliacha tu jikoni hadi pale linapoacha kupoza. Ukweli ni kwamba, friji ni kama gari; lisipopata "service" ndogo ndogo, litakula umeme mwingi na kufa kabla ya muda wake.
Hapa kuna siri 5 za kitaalamu za kutunza jokofu lako:
1. Safisha ile nyavu nyuma ya fridge lako "Condenser Coils" 🧹
Nyuma au chini ya friji yako kuna vyuma kama nyavu (coils). Hivi ndivyo vinavyotoa joto nje. Vikijaa vumbi, friji inabidi ifanye kazi mara mbili zaidi ili kupoza.
* Tip: Tumia brashi au vacuum cleaner kufuta vumbi hapo kila baada ya miezi 6. Hii itapunguza bili yako ya umeme!
2. Hakikisha ule mpira unaozunguka mlango wa friji lako unashika vizuri (Door Seals)
Mpira wa mlangoni (Gasket) ukilegea, hewa ya baridi inatoka nje, hii hupelekea friji lako kutumia nguvu nyingi kutengenza ubaridi mwingi ambao huishia nje, na matokeo yake kula umeme mwingi.
* Test: Chukua noti ya elfu moja, iweke nusu ndani nusu nje kisha funga mlango. Ukivuta noti na ikatoka kirahisi, basi mpira wako umechoka na unahitaji kusafishwa au kubadilishwa.
3. Usijaze Friji Kupita Kiasi (Airflow)
Ili friji ipoze vizuri, hewa inatakiwa izunguke (circulate). Ukijaza vyakula hadi unaziba "vents" za hewa, baadhi ya vyakula vitaharibika na motor (compressor) itachoka haraka. Acha nafasi kidogo kati ya vyombo ili kuruhusu hewa ya ubaridi izunguke vizuri ndani ya friji lako, hii itapunguza na ulaji wa umeme pia.
4. Seti joto Sahihi (The Sweet Spot) 🌡️
Wengi huweka friji kwenye "Max" wakidhani ndio bora.
* Ushauri: Halijoto bora kwa sehemu ya kawaida ni 3°C hadi 4°C, na freezer iwe -18°C. Hii inatosha kuua bakteria bila kulazimisha motor kufanya kazi kupita kiasi.
5. Usiweke Chakula cha Moto 🍲
Ukiweka sufuria ya chakula cha moto moja kwa moja kutoka jikoni, unapandisha joto la ndani ya friji ghafla. Hii inailazimu friji kutumia nguvu kubwa sana kurudisha ubaridi. Acha chakula kipoe kwanza kabla ya kukiingiza.
Pro Tip: Kumbuka kusafisha ndani ya friji kwa maji ya vuguvugu na Baking Soda au magadi au Bicarbonate ili kuondoa harufu mbaya bila kuharibu ladha na usalama wa chakula chako.