Jinsi ya kumfanya Mwanamke akuheshimu pasipo kumshurutisha

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,858
Reaction score
22,729
Kabla ya kulalamika kwamba mke wako hakuheshimu, kwanza jiulize mwenyewe kama unaheshimika.

Heshima ipo kwa wanaostahili, si kwa wanaodai. Jiheshimu kwanza na yeye atakuheshimu. Huwezi kulala na kila mwanamke unayekutana naye na utarajie heshima kutoka kwa mkeo.

Huwezi kumfokea mkeo, kumuaibisha na kumwita majina ya hovyo, na utarajie heshima kutoka kwake.

Ukimuita mshamba au jina lolote baya na yeye atakuita mbwa wewe [emoji23]

Ikiwa una afya na unakataa kufanya kazi, sahau kupewa heshima na mkeo.

Siku zote mwanaume anayejiheshimu yuko salama katika ndoa.

Heshima ni njia mbili, ikiwa unataka kuipata, lazima ujiheshimu kwanza na ndipo utaheshimiwa.

Ikiwa unataka mke wako azungumze nawe vizuri, mtendee vizuri pia.

Acha kupoteza maisha yako kwenye baa. Baada ya kazi tumia wakati wako na mkeo nyumbani

Muogeshe naye atakuogesha. Msaidie kazi za nyumbani kama vile kupika, kutosha vyombo na kufuta chupi zenu pamoja.

Mfanyie Suprise kwa vijizawadi vidogo vidogo hata vya chupi, pedi sindiria nk.

Mpe pongezi kila siku. Tembea naye jioni ukiwa umeshikana naye mikono.

Fanya wakati wake wa kulala uwe wa kukumbukwa kwa kumpelekea moto kisawasawa [emoji7][emoji8].

Mtoe out mkacheze muziki mkiwa mmekumbatiana kwa mahaba mazito kila weekend.

Utapata heshima yako kwa kujiheshimu mwenyewe kwanza na kuwajibika ipasavyo kwa mkeo .

Utaheshimika tu kama unavyoheshimu. Tabia, sio jinsia, ndiyo inayokupa heshima.

Wanaume tuliopo katika ndoa tuamke!

Ubarikiwe.
 
Yote haya inategemea umepata mwanamke wa aina gani. Kama ni mwelewa na mwenye exposure ukimtendea haya aisee mtakuwa washikaji sana na wenye ndoa yenye furaha. Vinginevyo utaishia kuitwa boya tu maana wenzetu hawa hawajawahi kueleweka hasa wanataka nini [emoji16]
 
Vinginevyo utaishia kuitwa boya tu maana wenzetu hawa hawajawahi kueleweka hasa wanataka nini
emoji16.png
Uboya hauwezi kuwepo iwapo tutajiheshimu. Kutieleweka kwa kwa wanawake husababishwa na ujinga fulani waliofanyiwa na wanaume wasiojiheshimu.
 
Mwanaume uwe na hela.sio kila siku sina hela.hata kama utakuwa mzuri kiasi gani amini usiamini kuna heshima hutopata.

Na hata hii si kwa wanaume ndugu yangu.hata Kwa wanawake pia.kama huna kitu mkononi hata mwanaume hakupi heshima anakuona huyu nae atanipiga mizinga tu.umasikini unaumiza,unatenga,hauwezi kusikilizwa,umasikini unatesa vibaya.

Pesa sio kila kitu lakini inaongeza heshima mahali fulani,inakukutanisha na watu fulani na mengineyo.
Kuwa na kitu cha kujiweza wewe mwenyewe kwanza.

Umesikini ulinitesa sana,ulininyong’onyeza,ulinitenga na watu na wengine ni ndugu wa karibu nami,umasikini ni mbaya.
Ila Mungu Kwa kuwa hatokei mkoa wowote hubariki
 
Mwisho kabsa umaskini ni laana tupinge umaskini
 
Kabla ya kulalamika kwamba mke wako hakuheshimu, kwanza jiulize mwenyewe kama unaheshimika.

Heshima ipo kwa wanaostahili, si kwa wanaodai. Jiheshimu kwanza na yeye atakuheshimu. Huwezi kulala na kila mwanamke unayekutana naye na utarajie heshima kutoka kwa mkeo.

Huwezi kumfokea mkeo, kumuaibisha na kumwita majina ya hovyo, na utarajie heshima kutoka kwake.

Ukimuita mshamba au jina lolote baya na yeye atakuita mbwa wewe [emoji23]

Ikiwa una afya na unakataa kufanya kazi, sahau kupewa heshima na mkeo.

Siku zote mwanaume anayejiheshimu yuko salama katika ndoa.

Heshima ni njia mbili, ikiwa unataka kuipata, lazima ujiheshimu kwanza na ndipo utaheshimiwa.

Ikiwa unataka mke wako azungumze nawe vizuri, mtendee vizuri pia.

Acha kupoteza maisha yako kwenye baa. Baada ya kazi tumia wakati wako na mkeo nyumbani

Muogeshe naye atakuogesha. Msaidie kazi za nyumbani kama vile kupika, kutosha vyombo na kufuta chupi zenu pamoja.

Mfanyie Suprise kwa vijizawadi vidogo vidogo hata vya chupi, pedi sindiria nk.

Mpe pongezi kila siku. Tembea naye jioni ukiwa umeshikana naye mikono.

Fanya wakati wake wa kulala uwe wa kukumbukwa kwa kumpelekea moto kisawasawa [emoji7][emoji8].

Mtoe out mkacheze muziki mkiwa mmekumbatiana kwa mahaba mazito kila weekend.

Utapata heshima yako kwa kujiheshimu mwenyewe kwanza na kuwajibika ipasavyo kwa mkeo .

Utaheshimika tu kama unavyoheshimu. Tabia, sio jinsia, ndiyo inayokupa heshima.

Wanaume tuliopo katika ndoa tuamke!

Ubarikiwe.
Huwajui wanawake,hawanaga fomula hao viumbe
 
Tafuta pesa ....

1-Mwanamke hatembezwi barabarani (kulingishia)...mpe gari la sivyo watamt@mb@ tu..
2-Mwanamke akikumis ndipo huongeza upendo siyo kila siku wewe saa moja upo nyumbani...(Hawatabiliki)..
3-Mpe hela na zawadi, Surprise (umepatia hapo)....
4-Mpe muda akuelezee pumba zake na uoneshe kum-support palipo na makosa mrekebishe usiku 😋😋😋😋...

Mwisho "Hakuna mafanikio ya mwanaume bila mkono wa Mama au mke" ila huwa haziivi wakikaa pamoja, kwanini?....next episode is loading....
 
Back
Top Bottom