Jinsi ya kumtongozwa mwanamke na akakubali!

Papa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
1,153
Reaction score
1,359
Mojawapo ya vikwazo tunavyokumbana navyo wanaume tunapokuwa tunammendea mwanamke ni jinsi ya kumuanza mwanamke. Utamuanzaje. Sio siri hapo ndipo huwa kuna mtihani mkubwa sana.

Hivi unakumbuka siku ile ukiwa bar, ukamuona mtoto mkali hatari. Udenda ukakutoka mwanaume. Ukijiuliuza utaanzaje ili angalau upate namba yake. Ili umcheki baadae. Lakini mara tu unapoamua kumfuata, unaona miguu yote inakuwa mizito. Moyo unakwenda mbio, kifua kinakaribia kupasuka. Na hata ukijatahidi sana kwenda kumfuata. Utaishia kumuuliza hivi huko kwenu mvua imenyesha?.

Unapomuona mwanamke unakuwa na hofu na maswali mengine. Unakuwa unafikiri sijui hata vutiwa na mimi, labda ana bwana mwingine, au atanipiga kibuti.

Tatizo lako kubwa ni kwamba hauna confidence. Haujiamini. Fullstop.
Unakuwa unafikiri labda huyu mwanamke atakuona huna sifa anazotaka, hauna gari nzuri, hauna six pack. Ndugu yangu mchawi mkubwa ni wewe mwenyewe.
Ufanye nini sasa
1.Unapomuona mtoto mkali, hakika unakuwa na confidence. Jiamini. Wanawake wote wanapenda wanaume wanaojiamini. Kwa sababu wanajua watuwa salama. Ukibabaika ujue utamkosa huyo mtoto.

2.Unapomuona mtoto mkali tulia, usipapalike, usiongee kama unafukuzwa. Usibane sauti yako. Usiongee kwa kusita sita. Utahitaji kufanya mazoezi ya jinsi ya kutumia sauti yako.

Toka nenda barabarani. Fanya mazoezi. Ukimuona mwanamke mfuate. Msalimie. "Mrembo mambo vipi" endelea. Ongea kwa kujiamini. Ukikwama rudi hapa niambie umekwama wapi.

Kazi ni kwako.
 
Nimekwama maeneo ya posta hapa nimekutana na mtoto mkali kila nikimuongelesha hana time na mm njoo unisaidie
 
Kwani demu anapomuona mwanaume mara ya kwanza anakuwa anajua hana pesa. Kuna jamaa kibao hawana pesa lakini wanachukua watoto wakali. Siri kubwa kujiamini tu
Sijabisha....ndio maana nimesema ni hao wengine, si mimi
 
Tarehe 01/01/2019 Kutakuwa na uzinduzi wa DVD ya jinsi ya kutongoza.
Mleta uzi unakaribishwa Mlimani city saa 12 jioni maana imebainika nawewe ni mwanachama wa domozege company
 
Kwamba we huamini katika mapenzi kabisa? kwamba kwako love is MYTH na Feelings hazina nafasi kwako
Hapana....naamini katika mapenzi ya kweli.
ila siamini katika mapenzi bila pesa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…