Jinsi ya kuona sayari kwa macho

Jinsi ya kuona sayari kwa macho

Steven Sambali

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2008
Posts
364
Reaction score
182
Wengi wameandika kuhusu kuangalia sayari zkuanzia jana ila hawajaweka urahisi wa jinsi ya kuziona kwa macho pale anga likiwa jeupe bila mawingu.

Nitatoa maelezo kidogo ili kuwasaidia wengi waweze kuziona.

Haya maelezo ni kwa wale wapo karibu na Ikweta zaidi. Ukiwa mbali na Ikweta basi utaona picha kidogo tofauti.

1. Tofauti ya NYOTA na SAYARI ni kwamba, mwanga wa nyota unachezacheza na kubadili rangi wakati mwanga wa sayari haubadiliki Kama ilivyo kwa Mwezi.

2. Sayari zote zinapita kwenye mstari ambapo JUA linapita. Hivyo angalia tu kwenye mstari, JUA kwa sasa linapipita. HII pia ni kwa wale ambao hawapo Ikweta.

3. Sayari kubwa au zilizopo karibu na Dunia ndiyo zinaonekana vizuri. Kwa maana hiyo Basi:
I. Sayari ya Venus ndiyo inaonekana kubwa zaidi na kung'aa kupita zote kwa sababu ipo karkbu na Dunia. Ila siyo kubwa kuzidi hizo nyingine.
Ii. Sayari ya Jupiter inafuatia kwa ukubwa kuonekana na kung'aa usiku. Jupiter pia ni moja ya sayari kubwa sana angani.
Iii. Sayari ya Saturn hazipishani na MARS kwa ukubwa. Saturn iko mbali ila ukiongeza na Pete yake, inakuwa kubwa sana na hivyo kuonekana vema usiku.
IV. Sayari ya Mars pia inaonekana vema jioni ya leo. Ukiangalia vizuri utagundua Ina wekundu fulani. Waweza kufumba macho na kufungua haraka ukiangalia utaona RED PLANET. Udongo wake ni mwekundu na hivyo unaweza kuona hiyo rangi.

Kwa kuangalia jua linatoka saa ngapi na ikifika saa fulani litakuwa wapi, nitakuwekeeni Link ili kila Mtu atafute kwa Mkoa au sehemu alipo, Sayari zitatoka saa ngapi na kuzama saa ngapi.

Kwa mfano sayari ikitoka saa 6 Mchana basi unategemea kuwa kwa watu wa Ikweta, ikifika jioni saa 12, sayari itakuwa imefika utosini yaani Kama ni jua ni saa Sita Mchana.

Sayari ikitoka saa 10 jioni basi jua linapozama, sayari inakuwa usawa wa jua la saa mbili asubuhi.
Hii itawasaidia kujua hizo sayari zitakuwa usawa gani.

Kwa kuongeza tu, waweza pia angalia zile nyota tatu zilizopangana kwa urefu Sawa na zinaitwa ORION au Muwindaji.

Hizi utaona pembeni yake kuna nyota mbili kubwa kushoto na kulia na kwa Ikweta, juu yake kuna nyota kubwa inawaka sana inaitwa SIRIUS. Hapo SIRIUS Kuna vinyota viwili vidogo na kengine kadogo zaidi ambako NASA wameshakaona. Kanyota hako ndipo Kabila la Dogoni kutoka nchi ya MALI wanadai wanatoka..
Hii ni habari nyingine ndefu zaidi...

Kujua Link ya sayari kutoka na kuzama nii hapa. Kila Mtu aandike Mkoa alipo ili iwe rahisi kupata usahihi.
Hii chini kwa Mkoa wa Dar es salaam. Kuna sehemu unaandika Mkoa na unabadilisha.


Nyota mbili zinazoonekana kwenye Orion, moja ni inaonekana Nyeupe inaitwa RIGEL na nyingine inaitwa BETELGEUSE. Waweza kuona ukubwa wake ukilinganisha na ukubwa wa Jua. Hizo nyota ni kubwa kuliko Sayari zote na jua letu.

Haya subirini JIONI muone.sayari..
 

Attachments

  • Screenshot_2025-01-25-20-41-27-983_com.noctuasoftware.stellarium_free-edit.jpg
    Screenshot_2025-01-25-20-41-27-983_com.noctuasoftware.stellarium_free-edit.jpg
    238.8 KB · Views: 6
  • Screenshot_2025-01-25-20-26-19-469_com.noctuasoftware.stellarium_free.jpg
    Screenshot_2025-01-25-20-26-19-469_com.noctuasoftware.stellarium_free.jpg
    427.5 KB · Views: 5
  • Screenshot_2025-01-26-11-53-53-106_com.whatsapp-edit.jpg
    Screenshot_2025-01-26-11-53-53-106_com.whatsapp-edit.jpg
    374 KB · Views: 5
  • Screenshot_2025-01-26-11-54-28-604_com.whatsapp-edit.jpg
    Screenshot_2025-01-26-11-54-28-604_com.whatsapp-edit.jpg
    486 KB · Views: 4
Screenshot_2025-01-26-12-33-25-946_com.android.chrome-edit.jpg

Ratiba ya Sayari kutoka na kuzama leo hii kwa wale wa Dar es salaam. Muda wa saa 12 jioni hadi saa mbili na nusu usiku zitaonekana vizuri. Ikikaribia saa tatu usiku, Saturn na Venus zitakuwa magharibi zikisogea kupotea.

Jupiter ipo katikati karibu na zile nyota tatu za ORION.

Mars yeye yupo peke yake mwisho kabisa na nadhani ikifika saa moja jioni ndiyo itakuwa inanyenyuka Mashariki.
 
Binocular yenye specs zipi inafaa kutazamia?
Kwa sayari za Venus, Jupiter, Saturn na Mars unaziona kwa macho na huhitaji kifaa chochote.

Ukitaka kuona vema inabidi uende Dukani wakakupe kabisa na elimu. Ukinunua Darubini, unanunua na Filter yake kwa kila Sayari. Ni ghali kidogo kupata Darubini nzuri hasa Kama wataka kuona Ring ya Saturn.

Vinginevyo waweza tu kununua za kawaida kabisa ila hutapata View nzuri bado. Kumbuka NASA ilibidi warushe TELESCOPE angani ili wapate picha nzuri.
Pia wanaweka Telescope kubwa huko Chile Milimani kwa sababu kuna GIZA sana (Chilean Astronomical Site).
Hivyo inabidi kwenda maeneo yenye Giza tororo na Mwezi usiwepo.

Jaribu kutafuta Camera Zenye Zoom kubwa Kama Nikon p1000.


View: https://youtu.be/BX8JZVtSljM?si=Zwq8Y4YCvQpO2YOG
 
Sijui wangapi mlifanikiwa kuziona Sayari? Leo jioni jua likizama pia zitaonekana pamoja.
Huko angani, Telescope ya NASA ilizinasa zote SITA zikiwa pamoja na kupiga picha ambapo na Mwezi ukaongezewa Pembeni. Telescope hii ipo angani na ndiyo maana Picha ni nzuri sana.

Screenshot_2025-01-27-11-15-28-292_com.facebook.katana-edit.jpg
Screenshot_2025-01-27-11-16-28-950_com.facebook.katana-edit.jpg
 
Zitaonekana Leo Tena?
Leo hadi Mwezi wa tatu mwanzoni zitaonekana vema kabisa Kama anga ni safi.
Tatizo ni moja tu kwamba, kila siku zitazidi kusogea Magharibi kwenda kuzama na kulisogelea jua hivyo jioni itakuwa shida sana kuiona SATURN. Nadhani kuanzia tarehe 10/02 shida itaanza kuwepo kutokana na Program ya Angani.


Ile nyota kubwa Magharibi jioni ni Venus na chini yake utaona hiyo Saturn.
 
Leo hadi Mwezi wa tatu mwanzoni zitaonekana vema kabisa Kama anga ni safi.
Tatizo ni moja tu kwamba, kila siku zitazidi kusogea Magharibi kwenda kuzama na kulisogelea jua hivyo jioni itakuwa shida sana kuiona SATURN. Nadhani kuanzia tarehe 10/02 shida itaanza kuwepo kutokana na Program ya Angani.


Ile nyota kubwa Magharibi jioni ni Venus na chini yake utaona hiyo Saturn.
Hiv zinaonekana magharibi au mashariki?
 
Hiv zinaonekana magharibi au mashariki?
Angalia ujumbe wa kwanza nimetoa maelezo. Maelezo yanafaa wale waliopo karibu na Ikweta. Kama upo mbali na Ikweta angalia Link chini na andika mji uliopo, utajua hizo sayari zinatoka saa ngapi na kuzama saa ngapi. Zikitoka Mashariki zinapita palepale Jua linapopita na hivyo angalia kwenye huo mstari utaziona.

Magharibi jua likizama utaona Saturn na Venus. Juu yako utaona Jupiter na Mashariki utaona Mars na Wekundu wake.

Tafadhali, soma maelezo ya ujumbe wa kwanza.....

 
Huku mawingu yameziba tangu juzi ila huwa naziona Venus na Jupiter kwa muda sasa. Natamani kuona Saturn na Mars.
 
Back
Top Bottom