Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

mkuu, ungeweka na picha ya tumbo lako basi
tuone effect ya hii diet katika kupunguza kitambi. Au waonaje?
Halafu hilo bakuli la ndizi limenitamanisha kweli,
leo lazima nifanye mpango. Asante sana mkuu
mmmh wewe mwali una yako. Ni tumbo tu wataka kuona au?funguka mama
 
Mkuu nakupa big up saaaaana maji ya moto hapo kwangu ndio tatizo, ila ngoja nijaribu
 
maji uyanywe kila siku au kwa muda fulani maana maji ya asubuhi mzeee kama smile vile na jingine huo mtindi uwe umeondolewa mafuta au ule wenye mafuta...
 
Asante mzizimkavu, binafsi nitajaribu ila hata mimi maji ya uvuguvugu nakunywa sana lakini sioni tumbo kupungua wala nini, nitajaribu na hayo mengine, Tumbo linanikosesha raha kwakweli!
 
1. Hapo penye red ndo mzizi mkuu wa mada hiii

2. Changanya na za kwako
 
nashukuru nimeweza kuacha chips,
ila maji ya uvuguvugu yananipa uvivu kunywa, nitaanza sasa........i hope sitakatisha......
 
Je kuna tatizo mtu akinywa tangawizi kwa wingi? Mie napenda sana tangawizi iliyochanganywa na asali, naweza kunywa mugs nne kwa siku. Je naweza kudhurika?
 
mmmh wewe mwali una yako. Ni tumbo tu wataka kuona au?funguka mama
Smile....Hivi mbona unanidhania bure?
Mzizi Mkavu amesha nambia ana mtoto kama mimi, usizushe mengine hapa. Lol
 
Ahsante mkuu kwa ushauri bomba

Matunda yanasaidia sana chakula kusambazwa katika sehemu zote za mwili taratibu na kwa ufanisi pamoja na kusafiri na chakula ambacho hakijameng'enywa kwa njia ya haja kubwa hivyo kupunguza uwezekano wa kupata kitambi. Chakula jamii ya mikunde mikunde inasaidia sana. .(Search Dietary Fiber)

Ila hapo kaka kwenye mayai, yasiwe mengi kwakuwa yana cholesterol na avidin(husababisha vitamin B7 isisambazwe mwilini) hivyo unaweza sababisha matatizo mengine. Mafuta ni muhimu kwakuwa yanasaidia kazi za cell na kulipumzisha ini kutengeneza mafuta mwilini.

Big up mkuu, nina jamaa hapa yeye ulaji wake sio kivile sana sana anapenda mabiscuit, chocolate kwa ufupi kwake kula sio issue lakini tumbo hilo...
 
sasa mzizi umewagusa wanene na wenye vitambi,je na sisi wembamba tule nini tuwe wanene jamani yaan huu mwili hauna shukrani nakula kitu lakin sinenepi kwann?
 
Ukishindwa kunywa Maji ya Uvuguvugu na Asali kijiko kimoja na limau moja kubwa wakati wa asubuhi unapo amka kunywa Glasi moja ya Mtindi kila asubuhi mchana na usiku kwa muda wa miezi 6 utapunguwa huo unene.

Mkuu ahsante kwa darasa lako zuri,
Binafsi nahitaji saana kupungua hususan kitambi, maji kwa asubuhi huweza kunywa isizidi glass moja na hukojoa mara kwa mara. Mtindi nikinywa tumbo hunivuruga haraka saana ambapo hupelekea mchafuko na kuharisha si zaidi ya saa moja tangu nimekunywa mtindi. Muongozo wako inshallah.
 
Kama Mtindi unakufanya uende haja kubwa basi kunywa maji glasi moja ya ya Uvuguvugu yaliyochanganywa na Asali safi kijiko kimoja kikubwa cha kulia wali na ukamulie juu yake limau kubwa moja fanya hivyo kila siku mwili wako utakuwa na Afya na kitambi kitakutoka na unene pia utakutoka utakuwa upo fresh fanya kila siku katika maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…