Nisaidieni dawa ya kupunguza Kitambi ...tumbo langu linazid kuwa kubwa
Pole sana mkuu,
Nakueleza kama mtu ambaye nilikuwa na tatizo kama lako, na kama umeshajishtukia hivyo umefanya vzr sana maana kinachofuata ilikuwa ni kushturiwa na maradhi which is extremely bad!
Mimi nilikuwa na Kg 86 siku moja tu niliamua sitaki kitambi na as am speaking nipo na kg 64.
Nilifanya nini hadi kufikia hapo;
1. Nilipunguza kabisa kula vyakula vya wanga, niliacha kabisa matumizi ya junk food, juice, chips, soda na wali, no beer ldb wine tena mara moja moja sana zingatia pia wingi wa unachokula punguza portion size.
2. Nilianza mazoezi ya kukimbia kwa mwezi nilijiwekea target at least 40kms na nilimudu, to date my running target kwa mwezi ni 200kms na namudu vzr.
3. Nilijiunga na running club maeneo niliyoishi na kushiriki Marathon kadiri niwezavyo ili kuwa challenged na ilinisaidia.
4. Niliacha kabisa kula usiku i only take fruits au mtindi (hii unatakiwa uanze taratibu mwisho utazoea)
5. Nilijifunza kufunga (fasting) ingawa hii bado siimudu kusema za ukweli msema ukweli mpnz wa Mungu.
Lkn kama mdau mmoja alivyosema kukimbia aisee ukiweza hii ni dawa moja nzr mno. Kuna wakati nilijihisi nimekula ovyo napiga ndefu moja 21.1km-42.2km kama mbili hivi nikipima baada ya wiki naona nimekata kg 1-2!
Kwa kweli mwili nilio nao sasa kila mmoja anaupenda.