Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Kuna jamaa yangu alianza program ya kuondoa kitambi, alipunguza mlo na kufanya mazoezi....akaishia kuwa mwembaba lakini kakitambi bado kamechomoza, anakuwa kama ameficha kofia ya Pikipiki tumboni.
Amefanya general exercises badala ya specific parts...kata ABS with different positions haiongopi.
 
Kinaweza Isha kwa wiki1,2au 3 kulingana na tiba lishe utakayo tumia.nilikuwa na kitambi Kama nimebeba pipa ndani ya tumbo baada ya kujilisha tibalishe kiliisha ndani ya wiki mbili TU na Sasa nafurahia maisha ya bila kitambi
Je ngozi ya tumbo ipo na ubora wake, haija pwetapweta??
 
Nisaidieni dawa ya kupunguza Kitambi ...tumbo langu linazid kuwa kubwa
Pole sana mkuu,
Nakueleza kama mtu ambaye nilikuwa na tatizo kama lako, na kama umeshajishtukia hivyo umefanya vzr sana maana kinachofuata ilikuwa ni kushturiwa na maradhi which is extremely bad!

Mimi nilikuwa na Kg 86 siku moja tu niliamua sitaki kitambi na as am speaking nipo na kg 64.

Nilifanya nini hadi kufikia hapo;
1. Nilipunguza kabisa kula vyakula vya wanga, niliacha kabisa matumizi ya junk food, juice, chips, soda na wali, no beer ldb wine tena mara moja moja sana zingatia pia wingi wa unachokula punguza portion size.

2. Nilianza mazoezi ya kukimbia kwa mwezi nilijiwekea target at least 40kms na nilimudu, to date my running target kwa mwezi ni 200kms na namudu vzr.

3. Nilijiunga na running club maeneo niliyoishi na kushiriki Marathon kadiri niwezavyo ili kuwa challenged na ilinisaidia.

4. Niliacha kabisa kula usiku i only take fruits au mtindi (hii unatakiwa uanze taratibu mwisho utazoea)

5. Nilijifunza kufunga (fasting) ingawa hii bado siimudu kusema za ukweli msema ukweli mpnz wa Mungu.

Lkn kama mdau mmoja alivyosema kukimbia aisee ukiweza hii ni dawa moja nzr mno. Kuna wakati nilijihisi nimekula ovyo napiga ndefu moja 21.1km-42.2km kama mbili hivi nikipima baada ya wiki naona nimekata kg 1-2!

Kwa kweli mwili nilio nao sasa kila mmoja anaupenda.
 
Kuna jamaa yangu alianza program ya kuondoa kitambi, alipunguza mlo na kufanya mazoezi....akaishia kuwa mwembaba lakini kakitambi bado kamechomoza, anakuwa kama ameficha kofia ya Pikipiki tumboni.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
 
Je ngozi ya tumbo ipo na ubora wake, haija pwetapweta??
Wale jamaa wa kufanyiwa upasuaji ndio ngozi za tumbo zao huwa hivyo after the procedure. Waeza muona mtu mwembamba freshi lakini huwa amevaa vest flani special inayoshikilia zile ngozi zisicheze, lakini hazina madhara. Mazoezi tu ndio ataendelea nayo ili kujiweka fit always.
 
Kwahiyo wakutumia dawa sijui ma detox ngozi haiwi hivyo maana navyojua mafuta yakitoka ghafla ngozi haiwezi ku-cope change itabaki imepanuka.
 
Kwahiyo wakutumia dawa sijui ma detox ngozi haiwi hivyo maana navyojua mafuta yakitoka ghafla ngozi haiwezi ku-cope change itabaki imepanuka.
Jamaa wa obesity huwa hivyo, ngozi itabaki kuwa hivyo milele. Lakini hakuna mtu anawezajua ukiwa umevalia
 
Kwahiyo wakutumia dawa sijui ma detox ngozi haiwi hivyo maana navyojua mafuta yakitoka ghafla ngozi haiwezi ku-cope change itabaki imepanuka.

Detox ni usafishaji tu wa mwili, huko ndani, kuondoa toxic substances ndani ya mwili, so hiyo hata haitasaidia upande wa hayo manyama.
 
Jamaa wa obesity huwa hivyo, ngozi itabaki kuwa hivyo milele. Lakini hakuna mtu anawezajua ukiwa umevalia
Sijui umeelewa nilichouliza??

Obesity akipunguza tumbo kwa mazoezi ngozi si itafiti
 
Pepsi na mkate?? si nasikia soda zinaongeza mwili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…