Jinsi ya kupika kabichi pekee na yenye mchanganyiko na mboga za aina nyingine

Mkuu kabichi lenye nyanya ukabalansi chumvi vizuri asee mbona unaweza ukajiuma ulimi, huyu mtoa mada anadeka au kamaliza form six
Mkuu nimekulia bush kwenye ugali tembele,ugali,mrenda,ugali mchicha siku mkibadilisha sana mboga ni ugari maharage ,

Lakini sijawahi kuuelewa ugari kabichi toka enzi zile mpaka leo .

Kama shule nimemaliza kitambo tu mkuu hilo usiwe na shaka na ndio maana kila siku niko humu kulisongesha gurudumu aliloliunda Max
 
Safi kabisa, basi kwa kuwa umeumbwa wa kiume, kitu kigumu kwako kula ni mawe, nyaya, misumari na michanga. Ila ukija kupanga familia yako jaribu kuwazoesha kula kila kitu ili waelewe hawatakiwi kuchagua vyakula km baba yao unavyofanya
 
Mleta mada watu wanakula ugali na chumvi sembuse kabichi!!?

Bila shaka utakuwa wa dar wewe.
Mkuu tunakulia shida tu ila Havipandi ngoo .

Mwite huyo anaekula ugali na chunvi muwekee sahani tatu moja ugali na nyama ya pili ugali na kabichi ya tatu ugai na chumvi aliyozoea kuila alafu mpe chaguo muone atachagua wapi mkuu.
 
Ni mapishi tu kama ukute maharage yaliyokolea nazi na dona Tena kuwe na kasamaki ka kukaanga pembeni
Achana na kudublicate mboga wengine kama kabichi ni kabichi tu,kama maharage ni yenyewe tu.
 
Ha ha ha umenikumbusha Mbali mpaka nimecheka Sio siri nimepata tabu sana ha ha ha utotoni yani nilikuwa sipendi kula kabichi na ugali yani Siku nikisia wanapika kabichi nakosa raha, nilikuwa Nakula ugali unazunguka mdomoni hamna radha kama azabu vile,ugali ulikuwa haupandi yani Da ! ! !, Siku hiyo Nakula basi tu ,kweli asee kabichi na ugali sio poa, labda umpate anayejua kuipika hapo sawa alafu iwe na harufu ya kuungua alafu iwe imekaangwa na mafuta mengi hapo kidogo angalau na isiwe na maji
 
Hujui faida za hiyo mboga wewe
Kama mboga zingekuwa ni Walimu basi kabichi ni mwalimu wa Walimu
Chochote ambacho unakitaka kwenye mboga yoyote basi Ukila kabichi unavipata vyote
 
Huko mbali unapopakumbuka mkuu ndio nilikotokea ata mimi ugari unazunguka mdomoni utafikir unafanya mashindano ya ya kapia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…