jooohs
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 2,524
- 10,287
Daa mtoa mada amenikumbusha mbali sana mwaka 2003 nikiwa naanza darasa la kwanza baba aliondoka kwenda kutafuta maisha baada ya ufukara kuzidi hadi leo hajawahi kurudi home.
Mama alikuwa hana kazi nakumbuka mboga tuliokuwa tunakula home ni ugali na chumvi karibia kila siku kwani mama alikuwa hana uwezo wa kununua mboga ya aina yoyote kitu alichokua akituambia mimi na dada yangu nikuwa ugali ndo unanguvu hayo mengine hawezi kununua. nakumbuka nilikula ugali kwa chumvi hadi ulimi ukafa ganzi.
Kuna msimu ulifika mavuno yalikuwa machache mama akashindwa kununua hata kasuku ya mahindi tukakosa kabisa chakula.
Nakumbuka jirani yetu alikuwa amepanda kabichi kwani alikuwa anakisima anamwagilia mimi na dada yangu ilikuwa ikifika usiku wa saa sita watu wamesha lala ndo tunanyatia tunaenda kuiba tena zile changa usiku tunawasha moto kwenye mafiga tunachemsha tunakula pamoja na mchicha .
Yani tulikuwa tukifika shambani sista anafata kabichi mimi mchicha yani nilikuwa nikipeleka mkono nashika rundo la mchicha huyo nakimbia.
Hizo kabichi zilikuwa tamu sana maana mchana wote mmepiga deshi .
Nakumbuka kunasiku tulienda mtembelea mjomba kijiji tofauti tuliletewa uji uliokuwa unasukari sister akagoma kunywa akaanza kumwambia mama anataka ule uji aliozoea kunywa maana toka nazaliwa tulikuwa hatujui kunakitu kinaitwa sukari.