Culture Me
JF-Expert Member
- May 24, 2017
- 10,490
- 21,398
Mwaka flan nilienda Bukoba basi nilivyofika tu wenyeji wakanikaribisha na sahani ya ndizi imechanganywa na samaki, kwa kua nilikua na ubao nikaipiga,kwenye ndizi hapo daaah,
sitaki kupikiwa hata awe fundi vipi staki mtu anipikie ndizi.
Asubuhi nakutana na ndizi zimechanganywa na maharage, mmh nikaipiga kibishi,
Mchana napewa ndizi zimechemshwa rost ya samaki pembeni, nikasema kazi ipo,
Usiku naletewa ndizi zina maharage + Samaki, mmh nikaona hapa nitakufa kwa njaa sababu me ndizi hua sipendi hivyo hata nikila sishibi,
Nilivyomaliza kula nikawaambia ukweli kua ndizi sipendi, walisikitika sana, wakajilaumu kwann hawakuniuliza kabla,
Kesho yake mchana likaangushwa pilau la kuku (my fav, [emoji39][emoji39]) nilikula mpaka nikahisi tumbo linapasuka.