Jinsi ya kupika makange ya samaki bila kutumia viungo vingi

Aaliyyah

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2022
Posts
19,041
Reaction score
46,239
Natumain wazima na weekend inaenda vizuri
Niwaletee recipe ya kupika makange ya samaki
Mahitaji
Samaki aliekaangwa
Kitunguu maji na kitunguu swaumu
nyanya za.kawaida(saga) na nyanya ya pakti,chumvi
Pilpilili hoho na karot ( kata shape upendayo )
Pilipili manga kama utapendelea
Nazi Kama unapendelea pia sio lazima
Mafuta ya kupikia

Jinsi ya kupika
Bandika sufuriq au pan jikoni weka mafuta ya kupikia kias kidogo
Anza kukaangaa kitunguu maji hadi kilainike kisha weka kitunguu swaumu kaanga kidogo
Weka nyanya zikichemka weka pilipili manga acha nyanya ziive kisha ongeza nyanya ya pakti
weka pilipili hoho pamoja na karot acha zilainike zisiive sana ongezea Nazi kidogo changanya na uache Kwa dakika 2 Kisha muweke samaki kwenye pan Changanya na viungo Kisha mgeuze acha dakika 2 makange yatakua tayari
Unaweza kula na wali ugali ndiz hata chips
 
Ahsante kwa darasa

INawezekana kufanikisha pishi hilo pasipo hiyo swaumu na pilipili manga?
 
Ahsante kwa darasa

INawezekana kufanikisha pishi hilo pasipo hiyo swaumu na pilipili manga?
Inawezekana kabisa na ikawa tamu kama kawaida hata Nazi kuongezea tu hata bila Nazi ni poa
 
Kwa style hii ndio uniambie nikonde sijui nibalance diet, siwezi kukuelewa. Pishi kama hili siezi kuacha kula hasirani, wanipeleke mloganzila nikawekewe puto tu.
🀣 tule tu mwananagu
 
Wife Material ndo hawa sasa.

Sio wale makucha marefu hawez hata kufua nguo zake, pumbavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…