Jinsi ya kupika makange ya samaki bila kutumia viungo vingi

Jinsi ya kupika makange ya samaki bila kutumia viungo vingi

Yesssss ila mara moja sana na mpishi mzuri tu .
Ningekuwa somewhere muda huu narudi ningesukuma dona la nguvu 🤣 ila tatizo sasa kulipata huku.
Napenda watu wanaopika sana aisee🤣🤣🤣
 
Asante bestieee naona leo unapika mapemaaaa hutaki shemeji achelewe

Mwenzio sipendagi nyanya kabisaaa naitumia Mara chache hapo ningeweka carot, soya sauce na corn starch na hivyo viungo vingine ningetoa kituuu
Ni kweli Kuna namna nying ya kupika chakula kizuri😍
 
Natumain wazima na weekend inaenda vizuri
Niwaletee recipe ya kupika makange ya samaki
Mahitaji
Samaki aliekaangwa
Kitunguu maji na kitunguu swaumu
nyanya za.kawaida(saga) na nyanya ya pakti,chumvi
Pilpilili hoho na karot ( kata shape upendayo )
Pilipili manga kama utapendelea
Nazi Kama unapendelea pia sio lazima
Mafuta ya kupikia

Jinsi ya kupika
Bandika sufuriq au pan jikoni weka mafuta ya kupikia kias kidogo
Anza kukaangaa kitunguu maji hadi kilainike kisha weka kitunguu swaumu kaanga kidogo
Weka nyanya zikichemka weka pilipili manga acha nyanya ziive kisha ongeza nyanya ya pakti
weka pilipili hoho pamoja na karot acha zilainike zisiive sana ongezea Nazi kidogo changanya na uache Kwa dakika 2 Kisha muweke samaki kwenye pan Changanya na viungo Kisha mgeuze acha dakika 2 makange yatakua tayari
Unaweza kula na wali ugali ndiz hata chips View attachment 2796485
Dah wali samaki alafu awe samaki mkubwa hichi chakula kitanitoa roho mimi.
 
Kucha ni urembo bhana hazimzuii mtu kupika😀
Huwez kuwa efficient kama mm mweny kucha fupi, utakataje nyanya na kucha marefu kama sio utahangaika tuu nyanya moja unakata dakika kumi.

Mi mweny napika ghetto, hao makucha marefu wakijaga wanaanza kujishaua "ooh niache nikupikie", sawa mama pika, bac bhana utacheka yupo slow kinoma makucha yanamsumbua hadi nikamwambia ebu kakae huko niache nipike mwenyew.
 
Back
Top Bottom