Jinsi ya kupika ndizi mzuzu mbivu za nazi

Jinsi ya kupika ndizi mzuzu mbivu za nazi

Attachments

  • IMG_20240920_092017.jpg
    IMG_20240920_092017.jpg
    198.8 KB · Views: 4
Natumaini mkopoa
Wapenz wa ndizi ,Ndizi mzuzu zikiiva msitupe
Leo nimewaletea recipe hii ya kupika ndizi mzuzu zilizoiva za Nazi

MAHITAJI
Naz
Ndiz zilizoiva
Iriki iliyosagwa ama nzima
Sukari kama hupendi tumia chumvi

Hatua ya kwanza
Menya ndizi kata vipande vinne
Kama unatumia Nazi ya kawaida chuja tui la kwanza zito (bubu)na tui la pili weka pekeyake
Kama unatumia ya pakti bas andaa Nazi Yako weka maji kidogo kwakuwa huwa nzito sana

Hatua ya pili
Bandika sufuria ama pan weka ndiz zako Kisha weka tui la Nazi
La pili lile jepes kama unatumia Nazi ya pakti weka maji(maji yasiwe mengi)Kisha weka iriki funika acha ichemke had maji yakikauka

Hatua ya Tatu
Maji yakikauka weka sukari kma hupendi weka chumvi Kisha mimina tui la lile zito tikisa sufuria taratibu had vichanganyike usikoroge koroge na mwiko vitapondeka acha vichemke Kwa dakika 5 zitakuwa tayari View attachment 3099784View attachment 3099785View attachment 3099786
Safi sana kwa wazee wa kigetogeto huu ni msosi mmoja mujarabu sana, naomba mfululizo wa mapishi kama haya simple yaendelee

Yanatufaa wengi sana, maana wengine tumekariri dagaa mchele na ugali tu, tukibadilisha sana Wali wa Pressure cooker na Maharage ya kupima kwa Mama Ntilie😂
 
Karibu
 
Back
Top Bottom