Jinsi ya kupika tambi

Jinsi ya kupika tambi

Mhhhh, yaani njaa imeuma ghafla. Pishi limenitamanisha, nitalijaribu home. Asante mtoa mada.

Tambi ni mmoja ya vyakula ambavyo unaweza kuandaa kwa haraka sana,uandaaji wake hachukua muda mfupi sana.Ni moja vile vyakula ambavyo mimi huandaa nikiwa nimechelewasha chakula au sina muda wa kupika.
Kuna namna na jinsi nyingi sana ya kuandaa tambi.Unaweza andaa tambi kama mlo mkuu,mlo wa pembeni au kuzitumia kwenye salad.
Jana niliandaa tambi kama mlo mkuu kwa ajili ya chakula cha jioni.

Mahitaji

  • Tambi robo paketi(paketi kubwa)
  • Karoti 1 Kubwa
  • Njegere robo kikombe
  • Vitunguu maji 2
  • Hoho 2
  • Soseji 3
  • Carry powder vijiko viwili vya chai
  • Chumvi
  • Salted Butter vijiko 3 vya chakula
Njia
1.Chemsha tambi,chemsha ngegere,chemsha soseji kisha chuja maji yote.weka pembeni
2.Osha na kata mboga zote za majani kwa urefu
3.Katika kikaango weka butter na karoti kisha weka jikoni ukaange kwa moto mdogo ili butter isiungue .Kaanga kwa muda mfupi tu,ili butter iingie kwenye karoti.

4.Ongeza vitunguu na njegere,kisha nyunyuzia carry powder kwa juu,kaanga kwa muda kidogo .
5.Ongeza Tambi na hoho kisha endelea kukaanga na kugeuza ili vichanganyike.
6.Ongeza Soseji zilizokatwa katika vipande vidogo kisha nyunyuzia chmvi na endelea kukaanga kwa muda kidogo tu ili chumvi iive.
7.Kikiwa tayari ,epua na utenge mezani.chakula hiki kinapendeza zaidi kikiliwa chamoto kabla butter haijapoa.


Chakula hiki kinatakiwa kupikwa kwa muda mfupi sana,kuanzia pale unapoanza kuweka mboga za majani kwani lengo ni kutokuivisha sana mboga hizo,zinatakiwa kuiva kwa juu tu.

Unaweza sindikiza chakula hiki na sosi ya aina yoyote ukipenda.Sisi hupenda kula chakula hiki

kama kilivyo bila sosi wala mchuzi wowote,tunafurahia harufu ya butter na carry powder tunapokula hivyo kuweka mchuzi au sosi ni kuaribu ladha na harufu hiyo.

Chakula hiki ni rahisi sana kuandaa ,ni cha haraka na nikitamu sana.


KAZI KWAKO.
 
na vizia siku nimfanyie surprise mke wako. ngoja niikopi kwenye karatasi.
thanks mzizi mkuu.
 
Mrejesho

ImageUploadedByJamiiForums1411322334.777853.jpg

Thanks mkuu,nimepata mlo mwingine wa kupika Kutoka kwako
 
Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua nina haraka au sina muda mrefu wakukaa jikoni. Pishi hili huchukua muda mfupi sana na ni mlo uliokamilika.

Mahitaji


  • Tambi ½ paketi
  • Vitunguu maji 2 vikubwa
  • Karoti 1
  • Hoho 1
  • Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  • Carry powder kijiko 1 cha chai
  • Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
  • Mafuta kwa kiasi upendacho
  • Mayai 2
  • Chumvi kwa ladha upendayo

Njia

1.Chemsha maji ya moto yanayotokota, ongeza chumvi na mafuta kidogo, weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive. Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango, weka mafuta, vitunguu maji, vitunguu swaumu, hoho, karoti na carry powder, kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula

  • Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.

Unaweza kula tambi hizi na mboga yoyote upendayo au laa ukala zikiwa kavu na kufuraiha ladha yake zaidi.

Tollyz kitchen

 

Attachments

  • tambi mayai.jpg
    tambi mayai.jpg
    45.6 KB · Views: 4,434
Back
Top Bottom