Jinsi ya kupika tambi

Jinsi ya kupika tambi

Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua nina haraka au sina muda mrefu wakukaa jikoni. Pishi hili huchukua muda mfupi sana na ni mlo uliokamilika.

Mahitaji

  • Tambi ½ paketi
  • Vitunguu maji 2 vikubwa
  • Karoti 1
  • Hoho 1
  • Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  • Carry powder kijiko 1 cha chai
  • Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
  • Mafuta kwa kiasi upendacho
  • Mayai 2
  • Chumvi kwa ladha upendayo

Njia

1.Chemsha maji ya moto yanayotokota, ongeza chumvi na mafuta kidogo, weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive. Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango, weka mafuta, vitunguu maji, vitunguu swaumu, hoho, karoti na carry powder, kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula

  • Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.

Unaweza kula tambi hizi na mboga yoyote upendayo au laa ukala zikiwa kavu na kufuraiha ladha yake zaidi.

Tollyz kitchen

Shukrani sana mkuu
 
pia kuna style hii, ukichemsha tambi zako unaweka mafuta kwa mbali au unachemsha ukiwa umeweka nazi ya azam/yoyote. Mayai yanachemshwa mda ambao tambi zinachemshwa kisha yakiiva yanakatwa vipande na kuungwa kama mboga (unakaanga vitunguu,karoti,hoho,nyanya kisha unatia vipande vya mayai) italiwa na tambi.
 
Salaam wanajamvi

kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza.
nimekaa huku ndani najskia njaa na mtaani kwangu sehemu ya kula iko mbali kidogo.

nilichonacho ndani ni pakiti za tambi na mchele ila vyote sijui kupika

sasa najiskia kupika tambi naombeni mnielekeze
 
Chukua tambi zako chemsha mpaaka ziwe zimelainika, zitoe na uziweke kwenye chombo kingine na kuziacha zichuje maji, then chukua sufuria nyingine weka jikoni then weka nazi au mafuta kiasi kidogo kama vijiko v3 then chukua hiliki zisage na kuchanganya kiasi kidogo cha sukari weka, then baada huo mchanganyiko kuchemka kidogo ingiza zile tambi zako na kuzichanganya taratibu ili zisivurugike kama dakika 3 zinatosha, ipua pakua kwenye sahani. Hapo tambi zako ziko tayari kuliwa.
 
Back
Top Bottom