Jinsi ya kupika tambi

Jinsi ya kupika tambi

Duuuh sijui ntatoa wap elfu tano ya soseji nipike hvyo
ukiona buku tano inakuwa ngumu mama,,,fanya hivi,nenda kibanda cha chips,nunua chips soseji lkni mwambie hizo sosej ziwe mbichi kabisa ha rudi zako home chipsi tupa kula deal na sosej sasa hahahahahahaha..maana huku tano nyingi joh....
 

Attachments

  • IMG_7644.JPG
    IMG_7644.JPG
    8 KB · Views: 105
Kwann Hzo Tambi Za Santa lucia Imeandikwa Inauzwa Kwa Tanzania Tu?Au Ni Plastiki?Mwenye Jibu Atusaidie
 
Iki kweli kizazi cha nyoka...yani m na mdogo wangu wa darasa la 4 ndo anatupikia...icho chakuka kwake n chepesi sana sasa ugali wa muhogo kweli utaweza ata songa mkuu?..vijana tuamke aya mambo ya marice cooker yanaharibu vijana# plus utozi na usister du# mwingine anasema tambi zinaoshwa my ribs

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Tambi ni mmoja ya vyakula ambavyo unaweza kuandaa kwa haraka sana,uandaaji wake hachukua muda mfupi sana.Ni moja vile vyakula ambavyo mimi huandaa nikiwa nimechelewasha chakula au sina muda wa kupika.


Kuna namna na jinsi nyingi sana ya kuandaa tambi.Unaweza andaa tambi kama mlo mkuu,mlo wa pembeni au kuzitumia kwenye salad.

Jana niliandaa tambi kama mlo mkuu kwa ajili ya chakula cha jioni.


Mahitaji



  • Tambi robo paketi(paketi kubwa)
  • Karoti 1 Kubwa
  • Njegere robo kikombe
  • Vitunguu maji 2
  • Hoho 2
  • Soseji 3
  • Carry powder vijiko viwili vya chai
  • Chumvi
  • Salted Butter vijiko 3 vya chakula

Njia


1.Chemsha tambi,chemsha ngegere,chemsha soseji kisha chuja maji yote.weka pembeni
2.Osha na kata mboga zote za majani kwa urefu
3.Katika kikaango weka butter na karoti kisha weka jikoni ukaange kwa moto mdogo ili butter isiungue. Kaanga kwa muda mfupi tu,ili butter iingie kwenye karoti.



4.Ongeza vitunguu na njegere,kisha nyunyuzia carry powder kwa juu,kaanga kwa muda kidogo .
5.Ongeza Tambi na hoho kisha endelea kukaanga na kugeuza ili vichanganyike.
6.Ongeza Soseji zilizokatwa katika vipande vidogo kisha nyunyuzia chmvi na endelea kukaanga kwa muda kidogo tu ili chumvi iive.
7.Kikiwa tayari ,epua na utenge mezani.chakula hiki kinapendeza zaidi kikiliwa chamoto kabla butter haijapoa.



Chakula hiki kinatakiwa kupikwa kwa muda mfupi sana,kuanzia pale unapoanza kuweka mboga za majani kwani lengo ni kutokuivisha sana mboga hizo,zinatakiwa kuiva kwa juu tu.

Unaweza sindikiza chakula hiki na sosi ya aina yoyote ukipenda.Sisi hupenda kula chakula hiki

kama kilivyo bila sosi wala mchuzi wowote,tunafurahia harufu ya butter na carry powder tunapokula hivyo kuweka mchuzi au sosi ni kuaribu ladha na harufu hiyo.

Chakula hiki ni rahisi sana kuandaa ,ni cha haraka na nikitamu sana.


KAZI KWAKO.
Hii mapishi ni mpya kwangu. Unaanza kukaanga karoti kisha ndo uweke vitunguu??!
 
Oya wazee msaada kwenye Tuta Hapo niko na mwanangu anang'ang'ania Tambi nyama sijawahi pika na sijui wanapika au wanakaanga msaada wandugu

Mtaalamu shusha uzi hapa huenda sio Mimi tu nisojua
 
Back
Top Bottom