Jinsi ya kupika UGALI Fasta Fasta (Full Steps)

Jinsi ya kupika UGALI Fasta Fasta (Full Steps)

Squidward

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2014
Posts
7,828
Reaction score
9,546
Mambo zenu wakuu leo nitafundisha jinsi ya kupika ugali.

Fuata Steps Hizi

MAHITAJI

Maji,unga wa sembe/Dona + Sufuria,Ubanio,Mwiko na jiko la aina yoyote mkaa au umeme au gesi..

Step 1

Sikia Injika sufulia yako jikoni ikiwa na maji yenye unga kidogo. hakikisha maji utayoweka yatakutosha.Pia hakikisha moto unakua sio mwingi ni wastani.

Step 2
Haya anza kukorogea hadi pale maji yatapochemka na kua uji uji unaotokota.

Step 3

Umeshafanikiwa step 2? ,Haya weka unga kiasi kwenye sufuria huku ukianza kuusonga taratiiibu na ubanio. Staili ya kuusonga ni kama unauminya huku unauzungusha kwa mwiko.

Step 4

Utaona mabadiliko ule uji utakua mgumu kila unapoendelea kuusonga.Ukishaona mabadiliko Hayo jua ndo ivo tena ugali umeshaiva.

Step 5 (Mwisho)

Andaa Sahani au hotpot kisha uipue ugali wako.

HONGERA! Nguna ipo tayari kuliwa na mboga yoyote ile uliyoiandaa,inaweza ikawa samaki wa kukaanga or whatever.

Asanteni

index.jpg
 
hahahaha
alafu wewe like ni add umenichekesha sana na ugali wako kama msukuma
Shy land
 
Last edited by a moderator:
Hahhahaha huo na mabujebuje hayo....kwanza inaonekana haushuki hivihivi huu ...
Tatizo ukiukosea mwanzo tu wakati wa kuweka unga,hayo mabuda hayaondok...yaani ukiwa unaweka unga unatakiwa unachanganya fastafasta mkono ukilegea tu unakula mabuda!!!Lakini kuna watu wanapenda ugali wa hivo dia mgumu na wenye muonekano huo!!
 
Tatizo ukiukosea mwanzo tu wakati wa kuweka unga,hayo mabuda hayaondok...yaani ukiwa unaweka unga unatakiwa unachanganya fastafasta mkono ukilegea tu unakula mabuda!!!Lakini kuna watu wanapenda ugali wa hivo dia mgumu na wenye muonekano huo!!

Yakiwa mabuga vuruga kwa handmixer ya keki lol sijawahi kujaribu lakini ila ndio nnayochanganyia chapati za maji
 
Print hii weka pembeni tayari kwa kuifanyia kazi ili nawe uwe mahiri kwenye idara hii pia.

Hahahaha ule ugari wa juzi nlifanya ujanja huo mana me ugari upishi wake nababaisha tu sinaga ujuzi
 
Back
Top Bottom