Jinsi ya kupika Visheti

Jinsi ya kupika Visheti

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
IMG_4772-590x393.jpg

Upishi wa Visheti

Vipimo

1.Unga 2 Vikombe

2.Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu


3.Maziwa ¾ Kikombe


4.Iliki Kiasi


5.Mafuta ya kukarangia Kiasi


6.Shira


7.Sukari 1 Kikombe


8.Maji ¾ Kikombe


9.Vanila ½ Kijiko cha chai


10.Zafarani (ukipenda) Kiasi


Namna ya kutayarisha na kupika

Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.

1. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.


2. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.


3. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha.


4. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.


5. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.


6. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.

 
Umenikumbusha siku za eid bongo...Mama mkubwa akipika kisheti lazima atumie ungo kuviunda hivi
visheti.jpg
 
Asante sana mkuu, nitajifunza niwe nawapikia wanangu huko badae
 
Hamira hutakiwi kuweka au baking powder je???

Pia nilijaribu kupika lkn sukari ndo majanga namna ya kuifanya igande ktk visheti,,mweeee mapishi haya ni fumbo kubwa mno.
Sio mbaya nikipewa ufafanuzi ktk maswal yangu.
 
Hamira hutakiwi kuweka au baking powder je???
Kwa ufahamu wangu huweki hamira wala baking powder, unakanda unga tu kama ilivyoelekezwa, labda kama kuna mwenye ufahamu mwingine maana mapishi yanatofautiana.
 
Pia nilijaribu kupika lkn sukari ndo majanga namna ya kuifanya igande ktk visheti,,mweeee mapishi haya ni fumbo kubwa mno.
Sio mbaya nikipewa ufafanuzi ktk maswal yangu.
Hapo kwenye sukari napo si pagumu ukipazoea. Ninachojua unachemsha maji na sukari mpaka inapokuwa kama inanata, ila angalia isiungue, ndipo unatia visheti vyako na kuvichanganya. Jinsi unavyoendelea kuchanganya sukari inaganda kwenye visheti hadi inakaukia humo yote.
 
Mbona vinakuwa vigumu tofauti na vile vya mtaani vinakuwa lainii na sukari yake hadi raha sema vinavutika km mpira.

Msinichoke mpishi mm
 
Mshanitamanisha visheti vile namba 8 vilokolea hiliki
 
Sukari unaweka wakati gani? Kwenye matayarisho sijaona sukari.
 
Shila ikoje hiyo

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mmmmh mkwe ungejua nnavyotamani visheti acha tu tena zile vya namba nane....

Mrs Kharusy nije kwako utanipikia visheti?

Mmmhu. Mi juzi juzi nlimpigia mtu usiku nkamuulizia visheti vya namba nane. Mie huita masheti. Nashkuru siku ya pili asubuhi kaniletea.

Sijui hata kavinunua wapi, havikua vizuri sana
 
Last edited by a moderator:
Shila ikoje hiyo

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Ni ule uji au mchanganyiko wa sukari na maji kiasi unaoandaliwa kwa ajiri ya kuungia visheti vikishaiva ili vipate sukari ile unayoionaga inagandia juu ya visheti.
Ngoja waje wenye maelezo mazuri utaelewa tu.
 
Back
Top Bottom