realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Vitumbua ni aina nyingine ya Chakula kinachopendwa zaidi katika maeneo mbalimbali nchini.
Vitumbua vina aina mbalimbali ya Mapishi, kuna Vitumbua vya Nazi, Mayai, Nyama na aina nyinginezo.
Vifaa vya kupikia vinapatikana Sokoni kwa Gharama nafuu inategemea na ukubwa unaoutaka.
Ni vizuri kupika nyumbani kuliko kununua, kwani usalama wake ni wa uhakika zaidi.
Ni rahisi kuandaa na kupikia pia.
Mahitaji.
Unga wa Mchele Nusu/ Kilomoja.
Unga wa Ngano (Robo)
Tui la Nazi (Nazi nzima)
Maji ya Uvugu vugu.(Lita Moja)
Hiriki.(Kijiko kikubwa cha Chai)
Sukari.(Robo)
Hamira. (kijiko kikubwa cha Chakula)
Mafuta ya Kuchomea.
Kikaangio cha Vitumbua
Jinsi ya Kuandaa.
Changanya Mchanganyiko wako Vizuri kabisa usiwe mlaini sana Wala Mzito sana.
Hakikisha kila kitu umeweka katika Vipimo sahihi ili Vitumbua vyako viwe vitamu sana.
Baada ya Kuchanganya acha Mchanganyiko wako kwa muda wa Nusu saa au Saa nzima ili uumuke vizuri. Na muda huu ni kulingana na hali ya hewa ya sehemu ulipo.
Utaweka kikaangio chako kwenye Moto hadi kipate Moto kidogo kisha weka mafuta kidogo yakichemka vizuri Chota Unga wako na kuweka kidogo kigogo.
Pika hadi Vitumbua vigeuke rangi na kuwa vya kahawia. Kisha toa kwenye kikaangio.
Vitumbua huliwa wakati wote na Chai, Soda,Juice na kahawa.