Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa lengo la maboreshoYanaonekana matamu.. ☺
Mumeo anafaidi
Per 1 kg hivi vitu ni gram 20 tu. Na maandazi si unatoa dough? Ukitoa dough moja ili ulikate Kate hapo cha mwisho kutia ni maji baada ya kuweka mafuta.Mpendwa mpishi kazi ya hivi vitu kwenye maandazi ni nini?? Na kipi kinatumika wakati gani kwa kipimo gani? Au unaweza weka vyote pwaaa....
1: Chapa maandashi(zi)
2:Baking powder
3:Baking soda (bicarbonate)
Cc Kalaga Baho Nongwa
😂😂😂Subiri nimtumie demu wake hii recipe, kuna siku alinipikia maandazi yakatoka bapa kama biscuit.
Kwa ajili ya mapenzi nikajifanya kusifia mazuri, toka siku hiyo kila weekend ananiletea tubiskuti twake kwa jina la maandazi.
hivi vyote hufanya kazi moja ya kuumua Maandazi, Cake, Biskuit na vitu vingine kama hivyo.Mpendwa mpishi kazi ya hivi vitu kwenye maandazi ni nini?? Na kipi kinatumika wakati gani kwa kipimo gani? Au unaweza weka vyote pwaaa....
1: Chapa maandashi(zi)
2:Baking powder
3:Baking soda (bicarbonate)
Cc Kalaga Baho Nongwa
Sijawah kujaribu nitapika siku mojaAsante baby 🙏
Kwahiyo nachagua kimoja tu cha kuweka sio vyotehivi vyote hufanya kazi moja ya kuumua Maandazi, Cake, Biskuit na vitu vingine kama hivyo.
Kwenye Maandazi tumia Baking Powder ndo yanaumuka na kuachana kama hivo.Kwahiyo nachagua kimoja tu cha kuweka sio vyote
Ngoja nikuletee matumiz sahihi soon tu nitasreenshot 😀Kwahiyo nachagua kimoja tu cha kuweka sio vyote
Vinatumikaje? Vyote at per? Au nikiweka kipi kipi siwekiPer 1 kg hivi vitu ni gram 20 tu. Na maandazi si unatoa dough? Ukitoa dough moja ili ulikate Kate hapo cha mwisho kutia ni maji baada ya kuweka mafuta.
Toka nilipoiona kwa mara ya Kwanza ID yako ilinitosha kujua kuwa wewe ni wife material kabisa .Mimi huwa napenda kupika, kujifunza na kujaribu Mapishi mbalimbali Nyumbani na Familia yangu hufurahia sana ninachokifanya mbali na Shughuli zangu zinazoniingizia Kipato.
kuna siku rafiki yangu alinipatia Maandazi matamu sana na niliyapenda sana.
Ilinibidi nifuatilie na nijue kuwa ametumia nini ili kupata Maandazi matamu kama yale bila hiyana akanielekeza.
Mahitaji.
1. Unga wa Ngano Kilo moja
2.Mafuta ya kupikia
3. Blue Band Vijiko vitatu vikubwa. (Prestige Margarine)
4. Sukari Vijiko Vitatu Vikubwa
5.Hiliki Kijiko Kimoja Kikubwa.
6.Baking Powder Kijiko Kimoja cha Chai.
7. Mayai Mawili Makubwa.
8. Maji ya Vuguvugu.
Maandalizi.
Weka Unga kwenye Bakuli, Yeyusha Blueband kisha weka kwenye Unga wako na uchanganye vizuri.
Weka mayai yako, Sukari, Hiliki, Baking Powder kwenye unga wako Endelea kuchanganya Vizuri.
Weka maji ya Vuguvugu kidogo kidogo kwenye Unga wako kisha endelea kukoroga hadi pale unga wako utakapokuwa tayari.
Hakikisha unga unakuwa Mgumu wastani kama wa kutengenezea Half Cake.
Ukiwa tayari Kata Unga wako na kuanza kupika Maandazi yako Mazuri na ya kunukia vizuri.
Unaweza kutengeneza Mengi kwa ajili ya familia na hata watoto kubeba Shuleni Asubuhi.
Kwa sisi wadada pia unaweza kubeba kwenda nayo kazini.
Yanafaa Kwa Biashara Pia.
Maandazi haya yanafaa kula kwa Chai,Juice, Soda na kahawa.
😋
View attachment 3087473
Ndo hayo matumizi nahitaji kuyajuaKwenye Maandazi tumia Baking Powder ndo yanaumuka na kuachana kama hivo.
Kwenye cake unaweza kutumia vyote.
Itategemea unaandaa nini kwa wakati huo ili upate kitu bora na sahihi ni muhimu kujua kuwa kipi ukitumia kitakupa matokeo chanya.
Yaani una watoto halafu huna tena 😅MuoneToka nilipoiona kwa mara ya Kwanza ID yako ilinitosha kujua kuwa wewe ni wife material kabisa .
Hivi umeolewa dada ,Mimi niko katika uhitaji wa moja kwa moja kuwa na mke ndani .
Umri wangu sio wa kuwa muhuni tena zaidi ya kunywa pombe kidogo kama kipoza uchovu ,njoo uwe wangu tuendeleze maisha .
Nb :niliwahi kuoa nikaachwa ,nina watoto ila walinikataa ,hivyo siwatambui kama watoto wangu hivyo Mimi ni single na pia Sina watoto