Jinsi ya Kutengeneza Maandazi laini na matamu bila kutumia Hamira

Jinsi ya Kutengeneza Maandazi laini na matamu bila kutumia Hamira

Mafano haya ni ya mwanafunzi wake Leo asbuhi
IMG_20240905_094230.jpg
 
Si waliungana na mama yao kunikataa kuwa Mimi sio baba yao ndiyo maana nasema sina watoto kabisa hivyo njoo tuanze moja mama .
Nb :Zuri kuliko Mimi ni mtu nimejaaliwa kuzaa watoto wazuri kuliko kawaida maana uwa wanafanana na Bibi yao
😅😅😅
 
Mandazi hayafai kukaa sana, unapaswa kuyamaliza ndani ya siku tano yakitunzwa vizuri kwa viambata hivyo hivyo.
Mimi wife huwa ananipikia vitumbua kama ugali nilishampiga marufuku kunipikia vitumbua vya na namna hiyo na kumwambia ajifunze....naomba somo la kupika /choma vitumbua
 
Mimi huwa napenda kupika, kujifunza na kujaribu Mapishi mbalimbali Nyumbani na Familia yangu hufurahia sana ninachokifanya mbali na Shughuli zangu zinazoniingizia Kipato.

kuna siku rafiki yangu alinipatia Maandazi matamu sana na niliyapenda sana.

Ilinibidi nifuatilie na nijue kuwa ametumia nini ili kupata Maandazi matamu kama yale bila hiyana akanielekeza.

Mahitaji.
1. Unga wa Ngano Kilo moja
2.Mafuta ya kupikia
3. Blue Band Vijiko vitatu vikubwa. (Prestige Margarine)
4. Sukari Vijiko Vitatu Vikubwa
5.Hiliki Kijiko Kimoja Kikubwa.
6.Baking Powder Kijiko Kimoja cha Chai.
7. Mayai Mawili Makubwa.
8. Maji ya Vuguvugu.

Maandalizi.
Weka Unga kwenye Bakuli, Yeyusha Blueband kisha weka kwenye Unga wako na uchanganye vizuri.

Weka mayai yako, Sukari, Hiliki, Baking Powder kwenye unga wako Endelea kuchanganya Vizuri.

Weka maji ya Vuguvugu kidogo kidogo kwenye Unga wako kisha endelea kukoroga hadi pale unga wako utakapokuwa tayari.

Hakikisha unga unakuwa Mgumu wastani kama wa kutengenezea Half Cake.

Ukiwa tayari Kata Unga wako na kuanza kupika Maandazi yako Mazuri na ya kunukia vizuri.

Unaweza kutengeneza Mengi kwa ajili ya familia na hata watoto kubeba Shuleni Asubuhi.

Kwa sisi wadada pia unaweza kubeba kwenda nayo kazini.

Yanafaa Kwa Biashara Pia.

Maandazi haya yanafaa kula kwa Chai,Juice, Soda na kahawa.

😋

View attachment 3087473
NOted
 
Back
Top Bottom