Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Asante sana kwa uzi huu sioni haja ya kuiga ukisasa maana Gym hazikuwepo aisee
 
Je kuna madhara yoyote ya kuoga maji ya baridi mara tu baada ya kumaliza kufanya mazoezi ??
Ndiyo, nimeshuhudia mtu akidondoka bafuni baada ya kuanza kuoga, ilikua tupo gym tukimenyeka.
Maelezo aliyotoa gym master alisema kua mwili hautakiwi kushtushwa kwa kumwagiwa maji ya baridi ghafla baada ya damu kua inatembea kwa kasi na mwili kua wa moto.

Itapendeza kama tutapata mdau ambaye ni daktari au ana elimu ya hiki ktu ili aendelee kutuelimisha.
 
Muhimu sana hii kitu binafsi baada ya zoezi nilikua nalala chali /kifudifudi kisha mamsapu anatembea juu yangu kuanzia vidole vya mkono mpaka kwenye kwato. Mifupa na joint zote zinanyooka kisha unaunyoosha msuli wa ta.ko umemaliza kazi.
 
Ok thanx,maana hawa mashugamumy nna bahati nao tatizo wananisakama sana!
 
Mpangilio wa chakula uweje haswa kwa mtu wa kufanya mazoez hayo?
 
Je mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 50 atapata matokeo sawa na vijana kama vile kujenga misuli?
 
Nitaleta mrejesho wangu baada ya wiki inshaallah
 
Mpangilio wa chakula uweje haswa kwa mtu wa kufanya mazoez hayo?
Mpangilio uwe kama ukiwa unafanya mazoezi mengine (yaani intake ya calories na protein iwe juu) hii ni kwa siye vimbau mbau au wenye miili ya kawaida. Mnene mlo wake inabidi aukate katika intake ya calories ili aukate mwili.

Mfano asubuhi uji wa ulezi unaweza ukaweka peanut butter, blue band au maziwa. Muda wa kifungua kinywa chapati tatu maziwa, ndizi na samaki/ dagaa/ kuku/ mboga ya majani.

Mchana ugali/ wali, samaki/ dagaa, maharage na mboga ya majani. Tunda.

Usiku wali na mboga za majani.

Hiyo ni vile typical ninavyokula mimi (na nikiwa sijafulia). Pia Siyo lazima vyote viwepo.
Hakikisha unakunywa maji mengi kwa kipindi chote hiki.
 
Je mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 50 atapata matokeo sawa na vijana kama vile kujenga misuli?
Ndiyo, kitakachokupa mwili unaoutaka ni chakula, maji, kupumzika na jinsi utakavyokua makini na mpangilio wako wa mazoezi na siyo umri.
 
Nitaleta mrejesho wangu baada ya wiki inshaallah
Itakua vizuri sana mkuu. Ila hata siku ya kwanza tu unaweza ukatupa mrejesho jinsi mwili ulivyoipokea hii work out.
 
Yaani mm sijafahamu kabisa hio Sparta inakuaje
 
Na ukianza kupiga push up Yale mambo yetu utakuwa unafanya kama kawaida au utasimama kwa muda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…