Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Yeyote ambaye amefanya hii routine tunaomba mrejesho mkuu, ututie moyo wengine.
 
Ni kwa sababu hayo yamelenga misuli ya juu, hata hivyo kwa kadri tutakavyojaliwa muda hata kwenye miguu tutazungumzia.
Mazoezi bila kula ni bure kabisa. Kuna vyakula ukila vizuri mtu anaweza fikiri unaenda gym hata kama huendi.
 
Umeongea ukweli mkuu.
Ila Tukiachilia mbali swala la genetics kwa baadhi ya watu, wengi wetu tukila balanced diet ni kunenepa na mwisho kujipa kitambi.
Acha hilo la kitambi.Namaanisha huwezi kuwa na mwili uliojijenga kama huli vizuri. Pia unaweza kufanya mazoezi na kula vizuri ila msongo wa mawazo ukaunyima mwili kujijenga.
 
Fanya crunches, sit ups, na kama una roller itumie.
Kwa kua unaanza.
Sit ups, Roller na Crunches fanya seti nne, kila seti fanya mara kumi.

Yapo mazoezi mengi ya tumbo naamini kuna wadau watakutajia ila anzia na hayo ukiwa advanced tutazidi kuongeza spices.
Mimi nimenunua roller naona inaniumiza tu
 
Mimi nimenunua roller naona inaniumiza tu
Inakuumiza kwa wapi? Kama ni mgongo jaribu kubadilisha namna unavyofanya.

Ila kama ni maumivu ya tumbo hiyo ni kawaida mkuu, cha kufanya punguza idadi ya seti kwa muda ukishazoea pandisha idadi.
 
Kwa wakaz wa dsm Kuna umbali wa kilomita ngapi kutoka kituo cha daladala mwananchi hadi mabibo hostel ??

na kukimbia umbali wa kati ya hivo vituo viwili ni sawa na kukimbia uwanja wa mpira wa miguu round ngapi ?
 
Samahani siyajui maeneo uliyoyataja hivyo nashindwa kukadiria, lakini ninaweza kukupa wazo jinsi gani unaweza kukimbia uwanja wa mpira na kuongeza kitu.
 
Back
Top Bottom