Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Yeyote ambaye amefanya hii routine tunaomba mrejesho mkuu, ututie moyo wengine.
 
Ni kwa sababu hayo yamelenga misuli ya juu, hata hivyo kwa kadri tutakavyojaliwa muda hata kwenye miguu tutazungumzia.
Mazoezi bila kula ni bure kabisa. Kuna vyakula ukila vizuri mtu anaweza fikiri unaenda gym hata kama huendi.
 
Umeongea ukweli mkuu.
Ila Tukiachilia mbali swala la genetics kwa baadhi ya watu, wengi wetu tukila balanced diet ni kunenepa na mwisho kujipa kitambi.
Acha hilo la kitambi.Namaanisha huwezi kuwa na mwili uliojijenga kama huli vizuri. Pia unaweza kufanya mazoezi na kula vizuri ila msongo wa mawazo ukaunyima mwili kujijenga.
 
Mimi nimenunua roller naona inaniumiza tu
 
Mimi nimenunua roller naona inaniumiza tu
Inakuumiza kwa wapi? Kama ni mgongo jaribu kubadilisha namna unavyofanya.

Ila kama ni maumivu ya tumbo hiyo ni kawaida mkuu, cha kufanya punguza idadi ya seti kwa muda ukishazoea pandisha idadi.
 
Kwa wakaz wa dsm Kuna umbali wa kilomita ngapi kutoka kituo cha daladala mwananchi hadi mabibo hostel ??

na kukimbia umbali wa kati ya hivo vituo viwili ni sawa na kukimbia uwanja wa mpira wa miguu round ngapi ?
 
Samahani siyajui maeneo uliyoyataja hivyo nashindwa kukadiria, lakini ninaweza kukupa wazo jinsi gani unaweza kukimbia uwanja wa mpira na kuongeza kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…