Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Binafsi enzi hizo nilikua napiga kwa sequence maalum.
Kwanza nilianza kwa kupiga push ups za kutanua kifua. Ambazo unapanga matofali mawili kushoto na kulia kwako au vipande vya mbao kisha unakua mikono waiweka juu na kupiga push-ups huku kifua kikiingia katikati.
Nilikua napiga push-ups 50 na nilienda mizunguko 6.
Break ya round na round nilikua na piga squats 100.

Zoezi namba 2 nilikua napiga push-ups za kubana kifua huku mikono nikiibana level ya mabega napo idadi ya push-ups ni kama round one na reps ni sita.

Zoezi namba tatu hapa nilikua naikutanisha mikono kisha natengeneza shepu kama ya kopa.
Nilikua napiga push-ups 3 in 1(yani kila push ups tatu nilizihesabu kama moja) huku kila nikishuka chini kifua kina gusa ile kopa.
Zoezi hili lilikua maalum kwa kujenga msuli wa nyuma ya mkono, kujenga kifua cha juu na kuziba yale matundu ya shingoni,kuujenga mgongo na kua na mwonekano wa kupasuka pasuka.
Nilikua napiga push-up 20 na round 5.

Baada ya hapo nilipiga Zoezi la kujenga shoulders ambalo mara nyingi niliipigia kitandani.
Unachuchumaa kitanda kikiwa nyumba yako kisha mikono una irudisha nyuma na kushika ubao wa kitanda.
Zoezi hili unapiga taratibu na unatakiwa upige push ups hizi 60 *5.

Ukimaliza unaenda mlangoni na kupiga pull ups kwa ajili ya kujenga msuli wa mbele ya mkono.
Pia weza ligeuza kujenga msuli wa nyuma ya mkono.

Baada ya kushughulikia sehemu zote nilikua napiga zoezi la kutengeneza six packs.
Hili zoezi ni gumu kulielezea ila unakaa chini.
Kisha unainyanyua miguu yako unakua kama V. Baada ya hapo unaweka mikono yako kifuani na kuanza kupeleka miguu mbele kama unasukuma kitu bila kuishusha. Unapiga mbele 30,kushoto 30,kulia 30 then unageuka na kupiga push-ups 100 za basketball ili kujenga misuli ya mkono wa chini, zile nyama chini ya kiwiko chako.

Then unahamia kwenye mazoezi ya miguu ukimaliza unajikumbushia kata mbili tatu za wingchun then unapiga sparring na swahiba wako kujiweka fiti tu.
Wewe sio mtu wa kawaida aiseeee
 
hivi gharama za Gym ni sh ngapi kwa anayejua?
Kila gym ina range yake.
Mfano mtaani kwangu kwa mwezi ni elfu kumi kwa siku session moja ni mia tano.

Kuna sehemu ukilipa elfu tano ndiyo haulipi tena.
Ila hizi ni zile local.

Advanced iliyo na kila kitu ni kuanzia elfu hamsini (Gongo la Mboto mwaka jana, sijui mwaka huu) kwa siku elfu tatu kwa session.
Sinza Mapambano elfu mbili kwa session, Home Gym sinza nafikiri ni elfu mbili pia.

Home Gym Kigamboni, elfu ishirini kwa Mwezi na elfu moja kwa siku (ni local usitishike na jina).

Mbeya, Soweto gym ni elfu thelathini kwa mwezi na elfu mbili kwa session (mwaka jana sijui mwaka huu).

So ni wewe tu na eneo ulilopo mkuu.
 
shida yangu moja tu, muendelezo wa mazoezi kwangu ni ngumu sana hakuna yamini ya kufanya mazoezi niweze kuendelea kila siku?
 
Mimi huwa nakimbia hasubuhi,naruka kamba,nafanya abdomen yaani tumbi pia napiga kwa kifupi sufanye mazoezi ya kujenga sehemu ya mwili nnachotaka kila part ya mwili ishughulike je nakosea?
 
Mimi huwa nakimbia hasubuhi,naruka kamba,nafanya abdomen yaani tumbi pia napiga kwa kifupi sufanye mazoezi ya kujenga sehemu ya mwili nnachotaka kila part ya mwili ishughulike je nakosea?
Kwakua target yako ni kila sehemu ishughulike sidhani kama unakosea.
Lakini kama lengo lingekua ni kuujenga mwili hapo ni kweli unakosea.

Mfano, kukimbia na kuruka kamba yote ni mazoezi yatakayokupa pumzi na kukupunguza mwili, tumbo utaliweka tumbo vile unavyotaka.

Sijaona kama unafanya zoezi la kifua au ya kufanania hayo.
 
Maamuzi yaliyo sahihi huja kwa kutafari Bali kunena kusiko tafakari ni upumbavu mbele za watu saafi
 
kwa kwali umeniponza na haya mazoezi yako. saiz kichwa, mbavu, bega moja, mgongo kwa chini, miguu kwa chini nyuma vinauma balaa. yaani najisikia hovyoo
 
Wakuu mimi nataka zoezi la kuimarisha miguu kuanzia kwenye mapaja hadi chini, nifanye zoezi gani kwa matokeo bora zaidi!??
 
kwa kwali umeniponza na haya mazoezi yako. saiz kichwa, mbavu, bega moja, mgongo kwa chini, miguu kwa chini nyuma vinauma balaa. yaani najisikia hovyoo
Pole kwa maumivu mkuu.

Tangu maumivu yaanze ulikua umefanya mazoezi haya kwa siku ngapi? Au ni umeanza tu na haya maumivu yakakuanza?

Umewahi kufanya mazoezi kabla ya kuifuata hii routine? Ulikua ni beginner au advanced?
 
Pole kwa maumivu mkuu.

Tangu maumivu yaanze ulikua umefanya mazoezi haya kwa siku ngapi? Au ni umeanza tu na haya maumivu yakakuanza?

Umewahi kufanya mazoezi kabla ya kuifuata hii routine? Ulikua ni beginner au advanced?

mie ni beginner, nilikuwa nimefanya kwa siku mbili, mazoezi nilikuwa nafanya zamani nikaacha
 
mie ni beginner, nilikuwa nimefanya kwa siku mbili, mazoezi nilikuwa nafanya zamani nikaacha
Nenda pole pole, nimetoa maelezo kwa mtu ambaye ni beginner aanzeje na afanyaje.

Hayo maumivu yanapita soon.
 
Back
Top Bottom