wa mjini
Member
- Dec 4, 2013
- 24
- 5
Naomba msaada wa kuelekezwa utengenezaji wa siagi ya karanga (peanut butter) ntashukulu nikipata msaada wenu.
Mahitaji
1)Karanga kg 1/4
2)Asali kijiko 1.5 cha chakula
3)Peanut oil au mafuta yeyote kijiko 1 na nusu cha chakula
4)Chumvi 1/2 kijiko cha chai (kama peanut zake hazijakua roasted na chumvi)
5)Chupa yenye mfuniko ya kigae (kwa kuhifadhia peanut butter yako)
Namna ya kutayarisha
1)ondoa maganda karanga zako
2)Osha vizuri then weka zikauke vizuri
3)Zioke katika oven dakika 30-35 minutes, moto 350F
4)Subir zipoe kidogo then mimina karanga katika blender ama food processor...saga dakika 1 acha kidogo saga hadi iwe laini
5)Ongeza asali,chumvi na mafuta saga hadi iwe laini...
6)Hifadhi katika chupa yako then weka kwenye friji
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
