Jinsi ya kutengeneza siagi ya karanga

Jinsi ya kutengeneza siagi ya karanga

wa mjini

Member
Joined
Dec 4, 2013
Posts
24
Reaction score
5
Naomba msaada wa kuelekezwa utengenezaji wa siagi ya karanga (peanut butter) ntashukulu nikipata msaada wenu.

Mahitaji

1)Karanga kg 1/4
2)Asali kijiko 1.5 cha chakula
3)Peanut oil au mafuta yeyote kijiko 1 na nusu cha chakula
4)Chumvi 1/2 kijiko cha chai (kama peanut zake hazijakua roasted na chumvi)
5)Chupa yenye mfuniko ya kigae (kwa kuhifadhia peanut butter yako)

Namna ya kutayarisha

1)ondoa maganda karanga zako

2)Osha vizuri then weka zikauke vizuri

3)Zioke katika oven dakika 30-35 minutes, moto 350F

4)Subir zipoe kidogo then mimina karanga katika blender ama food processor...saga dakika 1 acha kidogo saga hadi iwe laini

5)Ongeza asali,chumvi na mafuta saga hadi iwe laini...

6)Hifadhi katika chupa yako then weka kwenye friji

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Kuna dada mtaalamu wa mahunjumati anaitwa farkhina, msubiri
 
Mahitaji

1)Karanga kg 1/4
2)Asali kijiko 1.5 cha chakula
3)Peanut oil au mafuta yeyote kijiko 1 na nusu cha chakula
4)Chumvi 1/2 kijiko cha chai (kama peanut zake hazijakua roasted na chumvi)
5)Chupa yenye mfuniko ya kigae (kwa kuhifadhia peanut butter yako)

Namna ya kutayarisha

1)ondoa maganda karanga zako

2)Osha vizuri then weka zikauke vizuri

3)Zioke katika oven dakika 30-35 minutes, moto 350F

4)Subir zipoe kidogo then mimina karanga katika blender ama food processor...saga dakika 1 acha kidogo saga hadi iwe laini

5)Ongeza asali,chumvi na mafuta saga hadi iwe laini...

6)Hifadhi katika chupa yako then weka kwenye friji

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mahitaji

1)Peanut zenyewe kg 1/4
2)Asali kijiko 1 na nusu cha kulia
3)Peanut oil au mafuta yeyote kijiko 1 na nusu cha kulia
4)Chumvi 1/2 teaspoon (kama peanut zake hazijakua roasted na chumvi)
5)Chupa yenye ufuniko ya kigae (kwa kuhifadhia peanut butter yako)

Namna ya kutaarisha

1)ondoa maganda karanga zako

2)Osha vizuri then weka zikauke vizuri

3)Zibake katika oven dakika 30-35minutes moto 350F

4)Subir zipoe kidogo then mimina karanga katika blender ama food processor...saga dakika 1 acha kidogo saga hadi iwe laini

5)Add asali,chumvi na mafuta saga hadi iwe laini...

6)Hifadhi katika chupa yako ya kigae then weka kwenye friji

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Thanks Farkhina
 
Hata kama huna blender au Oven unaweza kutengeneza hii butter. Badala ya Oven kaanga karanga zako, na badala ya Blender tumia kinu. Twanga mpaka karanga zilainike, zikianza kulainika zinashikana. Hii kitu inafaa kuungia aina yoyote ya mboga hasa zile za asili. Mahitaji fuata mtiririko wa dada Fakhina. Hii kitu alinifundisha Bibi enzi za utoto
 
Nina allerge ya asali...naweza kuweka nini mbadala wake au nikiacha kuweka asali nikaweka sukari ya kawaida inakuaje?
 
hii bana niliiona kwa bibi yangu enzi hizo, karanga zinasiginwa kwenye jiwe laini mpaka zinakuwa laini sana kama butter, hakuna haja ya kuongeza mafuta kwa sababu zenyewe zinatoa mafuta. pia ya ufuta ni nzuri sana. ni nzuri kujitengenezea vitu natural visivyoongezwa kemikali.
 
JINSI YA KUTENGENEZA SIAGI YA KARANGA-PEANUT BUTTER

Utangulizi:
Siagi ya karanga ni uji/laini mzito uliotengenezwa kutokana na karanga zilizokaangwa na kusagwa. Siagi hii inaweza kuongezwa utamu na vitamini. Siagi ya karanga inatumika kwenye mkate, kupikia na kuchanganya na vyakula mbalimbali.

Viambaupishi: Karanga, mafuta yasiyoganda, chumvi, sukari ‘stabilizer’ Lecithin

Vifaa: Mashine ya kusagia, sufuria, jiko la mkaa, mwiko, mzani wa kupimia.

Hatua za uzalishaji:
1. Malighafi
Chagua karanga zilizokomaa, kavu na zenye ukubwa unaofanana. Angalia zisiwe na ukungu kama vile “Aspergillus flavus”. Karanga ziwe na mafuta asilimia

2. Kusafisha na kuchagua
Peta karanga kutoa uchafu na takataka zilizomo- toa karanga mbovu na zile zilizosinyaa au kushambuliwa wadudu/ chembechembe

3. Kaanga.
Kaanga kwa uanglifu kwenye joto la kutosha ili karanga ziive bila kuungua, ha tua hii inazipa karanga rangi ya kikahawia kidogo na kuleta harufu nzuri.

4. Toa ganda
Toa maganda kwenye karanga na kutoa zile zilizoungua
.
5. Saga
Saga karanga mpaka kufikia ulaini unaotakiwa.

6. Changanya
Chemsha siagi kufikia joto la 80[SUP]o[/SUP] [SUB]C[/SUB] – 90[SUP]o [/SUP][SUB]C[/SUB][SUB],[/SUB]changanya na mafuta sukari chumvi asilimiana “stablizer” NB stablizer inawezkuongezwa wakati wa kusaga karanga (wakati wa kurudia).

7. Jaza kwenye chupa
Kwenye chupa safi zilizochemshwa na kukaushwa. Ijazwe huku ikikorogwa ili kutoa hewa. Acha nafasi kidogo juu na funga kabisa hewa isipite. Unaweza ukaweka mafuta sehemu ya juu kwa kiasi kidogo ili kuzuia hewa isiingie kwenye siagi yako.



Imeandaliwa na Mtaalamu wetu wa Chakula. chanzo.ONE CLICK Habari: JINSI YA KUTENGENEZA SIAGI YA KARANGA-PEANUT BUTTER
 
Back
Top Bottom