Guys, mimi nilishawahi kutoka. Sio mara moja au mara mbili but ilikua muda sana. Nakumbuka nikiwa form 3 mwaka 2008 nilijiunga facebook na group moja la dini ya WICCA, hawa watu wanaamini uchawi mweupe yani uchawi usidhuru watu na siunajua tena mambo ya Harry Potter! Nilijikuta napenda sana kujua vingi na kujua kama ni ukweli mtu anaweza kufanya mambo kama niliyokua naona kwenye movies.
Basi kwenye group nilimuuliza admin, mmama mmoja wa USA kuhusu vitu vingi jambo lililofanya tukawa na uhusuano wa karibu kidogo, yaani tulikua tunachat directly inbox hapo ndo alipokua ananieleza vitu vingi sana kuhusu witchcraft na moja wapo ilikua astral projection kama njia nzuri ya kutoka na kukutana.
Aliniambia huwa wanatoka kwenye miili yao na kukutana, pia kuwa kuna watu wengine huwa wanahudhuria tukio la black sabbath kwa njia hiyo. KWA AKILI ZANGU KWANINI NISIJARIBU.
Cha kushangaza kila nilichojarb hakukufanya kazi, kwa miezi na miezi sikuona chochote hadi nikakata tamaa kabisa.
Ila tangu nilipoanza huo mchezo nilikua naona maisha yangu yamebadilika kidogo kwa sahemu yake, Mfano nilikua naota sana ndoto za kutisha au kusikia kama naitwa vile. Moja ya siku sitaisahau niliamka kujiandaa na shule lakini nikaamua nijilaze tena kidogoo, si unajua watu wa kusnooze! Niliota niko njiani kuelekea shule...kwenye kona alitokea mshkaji ambaye ni jirani yangu na classmate pia, kwa sababu sipendagi kuongea naye nikaamua kumkataa kwa kuvuka lami upande wa pili...basi bila kuniona na yeye alivuka lami upande wangu...haikua na namna ilibidi tuongee tu kidogo then mimi nikakazana kumwacha.
Huwezi kuamini niliposhtuka kwenye ndoto nilijiaanda chap nikatoka kuwahi shule, mazingira nliyopita yakanikumbusha ile ndoto ila nikaignore tu....cha kushangaza ni kwamba jamaa alitokeza exactly kwenye ile corner na nikajikuta namkataa vile vile, wakati namkataa ndo nikajua narudia ile ndoto. anyway nikasema jamaa alivuka lami pia ngoja tuone...JAMAA AKAVUKA LAMI VILE VILE...hadi maongezi tuliyoongea nilikua najua atakachokisema kabla hajasema. SITASAHAU HII..
ASTRAL PROJECTION ilivyonitokea.
Nililala zangu mapema sana siku hiyo nadhani saa mbili na nusu usiku. Nikiwa napanda kitandani nilikua nasikia sauti kama nyuki wengi vile, ghafla...najiona kwa chini jinsi nilivyojilaza kitandani...Niliogopa sana na nikajiuliza ni ndoto au ni kweli? nikajaribu hadi kupiga hesabu kichwani ili kujua kama ni ndoto ila kila kitu kilikua real. Nilipata hofu sana na ghafla nikajikuta kitandani tena...
Hii hali ilikua inanitokea mara kwa mara kila nikilala chali alafu ikiwa nimechoka...na ilikua inatokea kabla sijapata usingizi... Ila yule mama wa facebook aliniambia ni hali ya kawaida sana kuogopa, ila nitazoea na nitaweza kufanya vitu vingi zaidi.
Baada ya muda kweli nilizoea hadi nikawa ninaweza kuamua kufanya kitu fulani ambacho nikiamka nitaweza kutest na kuprove. Nilikua naenda sebulen, shuleni na hata mtaani tu...au siku moja niliamua kuangalia mtaa wetu wote kwa juu...ilikua amazing kusema kweli..
Kwa sasa hivi nimekua na kwa experience yangu pamoja na kufanya research mtandaoni nnaweza kukubaliana nakutaliana na baadhi ya comment za watu.(Lakini zingine nimeziweka kidini pia kwa sababu kwenye kutafuta maana nilibidi niangalie pia kwa upande wa kiKristo)
1. Kila mtu anafanya Astral Projection usiku bila kujijua.
Hii nakataa...naamini kila mtu hii hali inaweza kumtokea atleast mara moja maishani mwake lakini sio kila mtu kila siku. Ila Lucid Dreams naamini kila mtu anapata mara kwa mara maishani(Lucid Dream ni zile ndoto ambazo unaota na unajua kuwa unaota). Japo pia mtu anaweza akaota Lucid Dream na kama anajua techniques za Astral Projection akazitumia ili kutoka from Lucid Dreams to Astral projection...huwa ni rahisi kwa hivyo.
2.Astral Projection ni salama.
Hii pia nakataa kabisa...japo wanasema hakuna mtu aliyekufa moja kwa moja kwa kufanya astral projection lakini kwa mimi huwa napata wasiwasi kuamini hili...ukizingatia kuwa ni rahisi kukutana na mtu ambaye yuko kwenye comma kwenye astral plane...hii inanipa wasiwasi kuwa unaweza ukashindwa kurudi kwenye mwili wako na watu wakakukuta kwenye hali ya commatose.
USHAURI WANGU.
Kupractice hivi vitu haviji bure, lazima utapoteza kitu...mfano nilikua very bright shuleni before sijaanza...but nilivyoanza nilinotice nashindwa kuconcentrate darasani...najikuta nawaza kitu ambacho mwenyewe sijui ni nini, it's like everytime nakua kwenye trance state, hata pale ambapo kuna jambo la msingi kama mtihani wa taifa. Nakumbuka mtihani wa mock form 4 nilikua kwenye trance hadi msimamizi anaposema imebaki dak 10, ndo ninaanza kujiuliza huu mtihani vipi mbona hata sijasoma maswali? Ukuzingatia una dak 10 ile panick unashindwa uanze lipi uache lipi na yote yanaenda...simply nlikua nafail kizembe hivyo.
Pia kama mtu niliyeexperience, kuresearch na kuangalia kwa upande wa dini yangu nilifika conclusion moja; Ulimwengu mtu anaoingia wakati wa astral projection (Astral Plane) ni ulimwengu ambao uko kati katikati ya huu ulimwengu na ulimwengu wa vitu visivyoonekana. Kwenye ulimwengu wa vitu visivyoonekana kuna spirits(roho) nyingi chafu, majini wabaya, wachawi kazini, mizimu na na nafsi watu waliokufa. Kitendo cha mtu kuacha mwili wake na kwenda kwenye huu ulimwengu ni jambo ambalo hivi viumbe na roho mbaya vinapenda sana na vinawahi kwenda kuingia kwenye mwili ambao hauna mwenyewe...
Hii ndio ile inasababisha kupagawa/ kuwa possessed by demons. Kwa sababu wiccans wanaamini hivi viumbe huwa vinatamani sana binadamu ambao wana miili, kwa kuwa wenyewe ni roho wanashidwa kuenjoy baadhi ya vitu binadamu hai anaenjoy kama, kula, kulewa, ugomvi, sex, fujo n.k. hii ndio sababu nahsi hata kipindi nilikua kwenye trance nilikua posessed na pengine nilikua nafanya vitu nisivyojua.
Ukizingatia nilikua naenjoy nikiona ugomvi hadi nafeel orgasm, na mtu alikua akinichokoza nilikua nafurahia had mwenyewe najishangaa...coz nilikua napenda ugomvi sana.
Hii kitu sio ya kujaribu, kama mtu anataka kujaribu, mimi nimemwonya...alafu kwenye dunia tuna vitu vingi productive vya kujaribu...Better jifunze lugha nyingine, jisunze skills za kukupa pesa, jifunze self control itakayokusaidia nk....NIMEMALIZA