Mbumbumbu wa mwisho
Member
- Aug 31, 2015
- 80
- 23
Ahsante mkuu umenipa moyo sana na huo ni ushahidi kuwa hii kitu inawezekana. ila jina lako ndo limenikatisha tamaa. so nijuze kama upo serious. ulijiona?
Mkuu hiyo ID isikukatishe tamaa kwani niliamua kuitumia baada ya kujiona mjinga kwa kuto kuyatambua yanitokeayo na kila nikiiona napata hamu ya kujifunza mambo mbalimbali yanihusuyo kama binadamu!!
Hiyo kitu inawezekana kabisa na nimeifanya mara nyingi,lakini bado sijakomaa kwa sababu nilikuwa siijui!
Hapo mwanzo nilipokuwa nikianza kuhisi ganzi,nilikuwa nikiogopa na kudhani labda ndio jinamizi na nilikuwa nakemea kwa jina Yesu hadi nilikuwa nikihisi nawapigia wenzangu kelele!, Ajabu hawakuwahi hata siku moja kusikia nikikemea.
Hapo ndipoanza kujiuliza hii ni nini?
Bahati nzuri wakati napitia JF as a guest member nilikutana na uzi unaohusu ASTRAL PROJECTIO na jinsi inavyokua!
Siku iliyofuata ile hali ya ganzi ilipokuja nili relax na kujaribu kujiinua bila kujitikisa, hapo nilisikia mlio mkali kama wa kengele ya umeme, nilikuwa nikitaka kujiinua ule mlio unazidi huku ukiambatana na kitu kama vibrations zikianzia kichwani na kusambaa mwili mzima.
Ghafla vibration,ganzi na zile kelele zilikoma,hapo nilikuwa huru kuinuka kitandani nikasimama na nilikuwa mwepesi kama vile hakuna gravity.
Nilipo geuka nyuma ndio nilijiona nimelala na nilistuka kweli! nilihisi ndio labda nimekufa!
Nilifumba macho na ghafla nilivutwa kwa nguvu kurudi kitandani(sekunde moja) kama nimevutwa na sumaku na nikaamka hapohapo!!
Hiyo kitu inawezekana na ipo Mkuu Tom jelly!!!!!