Jinsi ya kutoka nje ya mwili (Astral Projection)

Kweli dunia ina maarifa ya kila namna!, Naomba kuuliza ikitokea ndo umeshatoka, upo kwenye misele kukawa na mtu anayekuhitaji aonane na wewe au anashida fulani, au umepigiwa simu huwa inakuaje? Je unaweza kufanya mawasiliano na wale wanaokuhitaji naombeni kidogo ufafanuzi hapa!

akikushitua/kukugusa tu lazima urud...yaan utasensi kinachoendelea kwenye mwili wako
 
Hivi Moving Speed inakuwaje?yaani unaweza kwenda umbali mrefu mf.nje ya nchi kwa muda gani na je hakuna possibility ya kujisahau huko kwa masiku?..katika mambo mengi yanayotuzunguka kuna FAIDA na HASARA.kama zipo ningependa nifahamishwe HASARA
 
IMANI ZA WATU KUHUSU ASTRAL PROJECTION/OUT OF BODY EXPERIENCE(OBE)/KUTOKA NJE YA MWILI.

1: Astral Projection ni nadra sana. ~Ukweli: Astral Projection ni jambo la kawaida sana kwa kweli. asilimia 5% hadi 10% idadi ya watu wote duniani wana uzoefu/ fahamu kutoka nje ya mwili angalau mara moja.

2: Astral Projection ni daima papo kwa papo na Huwezi kujifunza.~ Ukweli: Unaweza kujifunza Astral ili mradi kama umedhamiria kujifunza. Kuna mbinu nyingi sana za kujifunza AP kutegemea na mtu. Kwan kila mtu ni tofauti, hivyo hakuna mbinu fulani iliyo bora kwa kila mtu.

3: Si kila mtu anaweza kujifunza Astral Projection Ni kwa wachache tu.~ Ukweli: Mtu yeyote anaweza kujifunza ili mradi amedhamiria, Astral inahitaji baadhi ya mazoezi, msimamo na uwe open_minded/fikra huru. AP ni kama ilivyo kujifunza kutembea, kuendesha baiskeli au kuogelea, Astral Projection ni ujuzi unahitaji kujifunza/practice.

4:Watu wazima tu ndio wanaweza Astral kwa sababu wao wamekomaa zaidi Ukweli: Umri kamwe sio sababu ya Astral Projection. Ni ukweli kwamba watoto wadogo hufanya zaidi Astral kuliko watu wazima, Sababu ni kwamba watoto hawana hatia na wanaamini kila kitu kinawezekana, hivyo hufikia Astral Projection kwa urahisi zaidi. Sisi watu wazima hatuamini kila kitu kwa urahisi. hivo kitakacho kuwezesha kufanya AP ni kuamini kuwa ni kitu ambacho kinawezekana na pia amini kama unaweza.

5: Astral Projection si salama. Ukweli: Astral Projection ni uzoefu wa asili reportedin kila utamaduni na jamii yeyote duniani kwani Ni salama kwa kila watu maana haifungamani na imani yeyote. lakini mtu yeyote ambaye ana matatizo makubwa ya kisaikolojia lazima kuepuka AP.

6: Ni inachukua miaka kadhaa kufikia kufahamu Astral Projection. Ukweli: Kwa kuwa kila mtu ni tofauti,hakuna mtu anayeweza kuthibitisha muda gani inaweza kuchukua. Baadhi hufikia hilo juu ya kujaribu kwa siku moja na wengine huweza kufanikisha hilo hata katika kipindi cha wiki,mwezi,mwaka na kuendelea!.. lakini ukiwa na nia ya dhati na kufanya majaribio kila siku ndani ya mwezi tu utafanikiwa.

7: Inawezekana usiweze kurudi ndani ya mwili wako tena. Ukweli: Kila usiku wakati wa kulala, AP hufanyika bila ya kujitambua/kujielewa, kwani huwa controlled by subconscious mind, na hii ni kwa kila binadamu, mfano mzuri ni lucid dreams/ndoto ambazo muotaji hukumbuka kila kitu alichoota, lakini AP ni mtu kuidanganya akili yake kuwa amelala ili mwili uweze kutoa DMT/ganzi (ambayo humfanya mtu wakati anaota mfano kama anakimbia ili asiweze kuamka na kuanza kukimbia bali ni akili tu hubaki kufanya kazi, wakati amala) baada ya hapo ndio utaamka katika mfumo wa roho na sio mwili.hivo tofauti ya AP ni kwamba kila kinachofanyika wewe mwenyewe ndio unaamua ufanye nini, uende wapi n.k lakini dream huwa controlled by subconscious mind. Hivyo basi kila mtu anayeota wengi wao kama sio wote wangefia hukohuko/roho zao zisingeweza kurudi tena mwilini. Ikumbukwe kuwa Mtu anavyotoka nje ya mwili kuna kama kamba ya utando mweupe(silver code) ambayo huunganisha mwili mpya na mwili wa kawaida/physical body ambao humfanya mtu arudi ndani ya mwili wake bila ya kupotea, na unaweza pia usiione lakini we amini kama ipo, na pia kukaa nje ya mwili huttokea kwa mda maalum . Hata kama utakuwa hutaki kurudi ila mwili wako utalazimisha urudi tu/na utarudi.

8:Mwili wako ulio uacha au mpya kuingiliwa na mashetani/mizimu/ghosts wakati ukiwa kwenye Astral Projection. Ukweli: Hili ni swali la kawaida sana katika akili ya watu wengi, hakuna kiumbe chochote ambacho kinaweza kuingia katika mwili wako wakati ukiwa kwenye AP, na pia hata mwili wako mpya. Hauwezi kuingiliwa na kiumbe chochote pia, watu wenngi huisi silver cord/utando unaounganisha miili unaweza kukatika lakini sio kweli namaanisha hakuna kiumbe chochote chenye uwezo wa kuikata hii silver cord isipokuwa kama siku yako ya kufa ikifika ndio itakatika namaanisha kuwa silver cord huunganisha mwili wako na roho hivo kukatika kwake inamaanisha mtu kupoteza uhai/ kufa ambapo hutokea wakati wowote siku zako zikifika hata kama ulikuwa hufanyi AP. Na ikumbukwe pia vitu hivi humwingia binadamu wakati mwili na roho vipo pamoja/kuwa katika hali ya kawaida. Zingatia kuwa hii miili imeunganishwa kwa silver cord/utando mweupe hivo chochote kitakacho tokea kwenye mwili wako mfano mtu kukugusa au chochote kile utahisi na kurudi kwenye mwili wako haraka, japo wengine huisi kama ukiguswa utakufa lakini hii sio kweli ila utahisi kuna kitu kinafanyika kwenye mwili wako na utarudi haraka (kumbuka spidi ya roho kutembea ni zaidi+ ya kilomita milion elfu moja kwa sekunde)

9: Astral Projection inabadilisha imani za kidini ya mtu. Ukweli: katika tafiti nyingi zilizofanywa kwa watu wanaofanya AP hazijabadilisha imani zao, ila imechochea watu kukomaa katika ile imani aliyonayo mtu mwenyewe , na hii imeoneka hata kwa wale viongozi wakuu wa kiroho imewasaidia katika imani zao.

10: Huwezi kwenda mbali sana wakati ukiwa nje ya mwili. Ukweli: hakuna umbali maalum ambao mtu huishia, ila kwa sababu uwezo wa kiroho watu wapo tofauti hivo humfanya mtu kwenda umbali unaoendana na uwezo wake wa kiroho. Kumbuka uwezo wa kiroho watu wapo tofauti... hivo uwezo wako wa kiroho ulivyo ndivyo utakapokufikisha.

11:Wakati upo kwenye astral unaweza kukutana na viumbe wa ajabu/kutisha wakakudhuru. Ukweli: Ndiyo_ kwenye ulimwengu wa kiroho kuna wema na waovu, hivo uwezekano wa kukutana na vitu vya kutisha upo lakini kumbuka sio kweli kama viumbe hivyo vinaweza kukudhuru na vingi vyao huwa vya kutengenezwa na watu binafsi, kitakacho kuongoza wewe ni akili yako, kama ikitokea umekutana navyo unaweza kubadili mwelekeo na kwenda sehemu nyingine au kurudi sema kwa sababu vinaogopesha unaweza ukahofu lakini kiukweli havina madhara yeyote. USHAURI... kabla ya kufanya AP hakikisha upo katika mood nzuri na ondoa negativity thoughts/fikra hasi zote hii itakusaidia kutokukutana na viumbe wa ajabu/kutisha... napia hakikisha kabla hujafanya AP unakuwa na lengo mahususi, mfano labda unataka kwenda wapi? Kufanya nini? Kuona nini?kujifunza nini??? Hii itakusaidia kuwa specific na kuepukana na vitu vya ajabu...labda tu kama una lengo la kuviona sawa unaweza kwenda kuviona.
12: Huwezi kugusa vitu katika Astral. Ukweli: unaweza kugusa chochote na ukahisi mfano unaweza kula, kucheza,kusex na vyote vile ambavyo unaweza kufanya katika mwili wa kawaida, ila ni kwa vitu tu vilivyo katika mfumo wa astral; lakini kwa vitu vilivyo physical haiwezekani, kwa mfano ukiwa katika astral huwezi kuchukua au kuhisi kitu kilcho kwenye umbo la kawaida mfano labda uwaze kwenda benk kubeba hela, au kwenda kumpiga mtu haitawezekana,, itakua hivi chochote utakacho gusa hakitashikika au kuhisi utaona kama mkono unapitiliza tuu kama ushawahi kusikia mtu anapita ukutani ndio utakuwa mfano huo maana mwili wako utakuwa katika mfumo ambao niseme ni kama hewa.
13: Madawa ya Kulevya kutumika kusaidia kushawishi Astral. Ukweli: Inawezekana ikakusaidia kwenye astral lakini haishauriwi kwa sababu itakufanya kukupunguzia focus katika astral hivo itakufanya uchanganyikiwe na kutokuwa na mwelekeo wowote na kukufanya isiwe na faida yetote kwako.

14: Haiwezekani kukutana na wanadamu wengine wakati wa Astral. Ukweli: Inawezekana kukutana wengine binadamu (wafu au hai) katika 4D, lakini kama unataka kuzungumza nao kikamilifu na kukumbuka kile ambacho walisema, wanapaswa kuwa nao kuwa na ufahamu kamili wakati ukifanya hivyo. Namaanisha kuwa ukiwa katika astra na ukataka kuongea na mtu yeyote inabidi awe katika hali ya kawaida ila kama atakuwa amelala itakuwa ni vigumu maana itakuwa unaongea na mtu aliyelewa au hataeleweka kwa kile anachoongea... ila akiamka anaweza kukumbuka kama uliongea naye ila hatajua ni nini na kwa upande wake ataona ilikuwa ni ndoto tu. ( zingatia kua focus kwa kile unachotaka mfano kama umemfocus john,juma,rashid n.k huyo ndio utamuona)
15: Astral Projection huthibitisha maisha baada ya kifo? Ukweli: hakuna uthibitisho wowote kuhusu kuwa mtu ambaye anafanya AP hata akifa ndio ataenda kuishi maisha hayo... Ila baadhi ya watu wanaofanya astral huamini kuna maisha baada ya kifo, kumbuka kwenye astra kuna kula, kulala,kucheza,sex na vingine vyote ambavyo hufanyika kwenye maisha ya kawaida ... na ndio maana wengine huona kifo ni kitu cha kawaida tu kwao wala hawaogopi.
#»»»»swali/maoni/mchango unakaribishwa««««#
 
Bennie 369..nataka kujua astral body nayo inafeel vitu kama mvua, jua na barid??
 
Last edited by a moderator:
wadau mi natamani sana hii kitu ila nimejaribu almost a week now nimeshindwa kabisa hasa swala la kuconcentrate limekuwa gumu sana naomba msaada wenu nifayeje ili niweze kufanya hii kitu!
 
ndo maana nikasema watu tupo tofaut, ukiona concentration imekushinda tafta nyingine, kila njia inawezekana kwa kila mtu.... jaribu kupitiapitia coments zilizotangulia.
 
kuna zaid ya njia mia kama sio buku.... unaweza pia kuingia google utazipata inayokufaa
 
Mimi nafikiaga ile hali ya kuwa mwili umeshatulia kama nimelala, na wakati huo nikiwa najitambua.
Kinachonikera nashindwa kuachana na mwili wangu wa kawaida.
 
wadau mi natamani sana hii kitu ila nimejaribu almost a week now nimeshindwa kabisa hasa swala la kuconcentrate limekuwa gumu sana naomba msaada wenu nifayeje ili niweze kufanya hii kitu!

Acha kutumia kilevi cha aina yoyote ile. Vilevile punguza na uache kabisa kutumia vyakula vya nyama!
 
Mkuu Bennie 369 ebu naomba ufafanuzi kidogo jana nilikuwa napitia makala flan nikaambiwa kusafir au kupaa masaa marefu kama nchi nyingine au outer space inahitaji utaalam wa hali ya juu kuhusu kucontrol speed, kufocus n.k... Ssa nataka kujua kama mtu huez kupotea coz of silva cord kwann mtu uhofie speed!
Pili nikaona kitu kinaitwa AP sex nahitaj ufafanuz kidogo apo kuwa ni je AP body inaingilia physical body ya mtu au zote ziwe in AP.
 
Last edited by a moderator:
IMANI ZA WATU KUHUSU ASTRAL PROJECTION/OUT OF BODY EXPERIENCE(OBE)/KUTOKA NJE YA MWILI.

1: Astral Projection ni nadra sana. ~Ukweli: Astral Projection ni jambo la kawaida sana kwa kweli. asilimia 5% hadi 10% idadi ya watu wote duniani wana uzoefu/ fahamu kutoka nje ya mwili angalau mara moja.

2: Astral Projection ni daima papo kwa papo na Huwezi kujifunza.~ Ukweli: Unaweza kujifunza Astral ili mradi kama umedhamiria kujifunza. Kuna mbinu nyingi sana za kujifunza AP kutegemea na mtu. Kwan kila mtu ni tofauti, hivyo hakuna mbinu fulani iliyo bora kwa kila mtu.

3: Si kila mtu anaweza kujifunza Astral Projection Ni kwa wachache tu.~ Ukweli: Mtu yeyote anaweza kujifunza ili mradi amedhamiria, Astral inahitaji baadhi ya mazoezi, msimamo na uwe open_minded/fikra huru. AP ni kama ilivyo kujifunza kutembea, kuendesha baiskeli au kuogelea, Astral Projection ni ujuzi unahitaji kujifunza/practice.

4:Watu wazima tu ndio wanaweza Astral kwa sababu wao wamekomaa zaidi Ukweli: Umri kamwe sio sababu ya Astral Projection. Ni ukweli kwamba watoto wadogo hufanya zaidi Astral kuliko watu wazima, Sababu ni kwamba watoto hawana hatia na wanaamini kila kitu kinawezekana, hivyo hufikia Astral Projection kwa urahisi zaidi. Sisi watu wazima hatuamini kila kitu kwa urahisi. hivo kitakacho kuwezesha kufanya AP ni kuamini kuwa ni kitu ambacho kinawezekana na pia amini kama unaweza.

5: Astral Projection si salama. Ukweli: Astral Projection ni uzoefu wa asili reportedin kila utamaduni na jamii yeyote duniani kwani Ni salama kwa kila watu maana haifungamani na imani yeyote. lakini mtu yeyote ambaye ana matatizo makubwa ya kisaikolojia lazima kuepuka AP.

6: Ni inachukua miaka kadhaa kufikia kufahamu Astral Projection. Ukweli: Kwa kuwa kila mtu ni tofauti,hakuna mtu anayeweza kuthibitisha muda gani inaweza kuchukua. Baadhi hufikia hilo juu ya kujaribu kwa siku moja na wengine huweza kufanikisha hilo hata katika kipindi cha wiki,mwezi,mwaka na kuendelea!.. lakini ukiwa na nia ya dhati na kufanya majaribio kila siku ndani ya mwezi tu utafanikiwa.

7: Inawezekana usiweze kurudi ndani ya mwili wako tena. Ukweli: Kila usiku wakati wa kulala, AP hufanyika bila ya kujitambua/kujielewa, kwani huwa controlled by subconscious mind, na hii ni kwa kila binadamu, mfano mzuri ni lucid dreams/ndoto ambazo muotaji hukumbuka kila kitu alichoota, lakini AP ni mtu kuidanganya akili yake kuwa amelala ili mwili uweze kutoa DMT/ganzi (ambayo humfanya mtu wakati anaota mfano kama anakimbia ili asiweze kuamka na kuanza kukimbia bali ni akili tu hubaki kufanya kazi, wakati amala) baada ya hapo ndio utaamka katika mfumo wa roho na sio mwili.hivo tofauti ya AP ni kwamba kila kinachofanyika wewe mwenyewe ndio unaamua ufanye nini, uende wapi n.k lakini dream huwa controlled by subconscious mind. Hivyo basi kila mtu anayeota wengi wao kama sio wote wangefia hukohuko/roho zao zisingeweza kurudi tena mwilini. Ikumbukwe kuwa Mtu anavyotoka nje ya mwili kuna kama kamba ya utando mweupe(silver code) ambayo huunganisha mwili mpya na mwili wa kawaida/physical body ambao humfanya mtu arudi ndani ya mwili wake bila ya kupotea, na unaweza pia usiione lakini we amini kama ipo, na pia kukaa nje ya mwili huttokea kwa mda maalum . Hata kama utakuwa hutaki kurudi ila mwili wako utalazimisha urudi tu/na utarudi.

8:Mwili wako ulio uacha au mpya kuingiliwa na mashetani/mizimu/ghosts wakati ukiwa kwenye Astral Projection. Ukweli: Hili ni swali la kawaida sana katika akili ya watu wengi, hakuna kiumbe chochote ambacho kinaweza kuingia katika mwili wako wakati ukiwa kwenye AP, na pia hata mwili wako mpya. Hauwezi kuingiliwa na kiumbe chochote pia, watu wenngi huisi silver cord/utando unaounganisha miili unaweza kukatika lakini sio kweli namaanisha hakuna kiumbe chochote chenye uwezo wa kuikata hii silver cord isipokuwa kama siku yako ya kufa ikifika ndio itakatika namaanisha kuwa silver cord huunganisha mwili wako na roho hivo kukatika kwake inamaanisha mtu kupoteza uhai/ kufa ambapo hutokea wakati wowote siku zako zikifika hata kama ulikuwa hufanyi AP. Na ikumbukwe pia vitu hivi humwingia binadamu wakati mwili na roho vipo pamoja/kuwa katika hali ya kawaida. Zingatia kuwa hii miili imeunganishwa kwa silver cord/utando mweupe hivo chochote kitakacho tokea kwenye mwili wako mfano mtu kukugusa au chochote kile utahisi na kurudi kwenye mwili wako haraka, japo wengine huisi kama ukiguswa utakufa lakini hii sio kweli ila utahisi kuna kitu kinafanyika kwenye mwili wako na utarudi haraka (kumbuka spidi ya roho kutembea ni zaidi+ ya kilomita milion elfu moja kwa sekunde)

9: Astral Projection inabadilisha imani za kidini ya mtu. Ukweli: katika tafiti nyingi zilizofanywa kwa watu wanaofanya AP hazijabadilisha imani zao, ila imechochea watu kukomaa katika ile imani aliyonayo mtu mwenyewe , na hii imeoneka hata kwa wale viongozi wakuu wa kiroho imewasaidia katika imani zao.

10: Huwezi kwenda mbali sana wakati ukiwa nje ya mwili. Ukweli: hakuna umbali maalum ambao mtu huishia, ila kwa sababu uwezo wa kiroho watu wapo tofauti hivo humfanya mtu kwenda umbali unaoendana na uwezo wake wa kiroho. Kumbuka uwezo wa kiroho watu wapo tofauti... hivo uwezo wako wa kiroho ulivyo ndivyo utakapokufikisha.

11:Wakati upo kwenye astral unaweza kukutana na viumbe wa ajabu/kutisha wakakudhuru. Ukweli: Ndiyo_ kwenye ulimwengu wa kiroho kuna wema na waovu, hivo uwezekano wa kukutana na vitu vya kutisha upo lakini kumbuka sio kweli kama viumbe hivyo vinaweza kukudhuru na vingi vyao huwa vya kutengenezwa na watu binafsi, kitakacho kuongoza wewe ni akili yako, kama ikitokea umekutana navyo unaweza kubadili mwelekeo na kwenda sehemu nyingine au kurudi sema kwa sababu vinaogopesha unaweza ukahofu lakini kiukweli havina madhara yeyote. USHAURI... kabla ya kufanya AP hakikisha upo katika mood nzuri na ondoa negativity thoughts/fikra hasi zote hii itakusaidia kutokukutana na viumbe wa ajabu/kutisha... napia hakikisha kabla hujafanya AP unakuwa na lengo mahususi, mfano labda unataka kwenda wapi? Kufanya nini? Kuona nini?kujifunza nini??? Hii itakusaidia kuwa specific na kuepukana na vitu vya ajabu...labda tu kama una lengo la kuviona sawa unaweza kwenda kuviona.
12: Huwezi kugusa vitu katika Astral. Ukweli: unaweza kugusa chochote na ukahisi mfano unaweza kula, kucheza,kusex na vyote vile ambavyo unaweza kufanya katika mwili wa kawaida, ila ni kwa vitu tu vilivyo katika mfumo wa astral; lakini kwa vitu vilivyo physical haiwezekani, kwa mfano ukiwa katika astral huwezi kuchukua au kuhisi kitu kilcho kwenye umbo la kawaida mfano labda uwaze kwenda benk kubeba hela, au kwenda kumpiga mtu haitawezekana,, itakua hivi chochote utakacho gusa hakitashikika au kuhisi utaona kama mkono unapitiliza tuu kama ushawahi kusikia mtu anapita ukutani ndio utakuwa mfano huo maana mwili wako utakuwa katika mfumo ambao niseme ni kama hewa.
13: Madawa ya Kulevya kutumika kusaidia kushawishi Astral. Ukweli: Inawezekana ikakusaidia kwenye astral lakini haishauriwi kwa sababu itakufanya kukupunguzia focus katika astral hivo itakufanya uchanganyikiwe na kutokuwa na mwelekeo wowote na kukufanya isiwe na faida yetote kwako.

14: Haiwezekani kukutana na wanadamu wengine wakati wa Astral. Ukweli: Inawezekana kukutana wengine binadamu (wafu au hai) katika 4D, lakini kama unataka kuzungumza nao kikamilifu na kukumbuka kile ambacho walisema, wanapaswa kuwa nao kuwa na ufahamu kamili wakati ukifanya hivyo. Namaanisha kuwa ukiwa katika astra na ukataka kuongea na mtu yeyote inabidi awe katika hali ya kawaida ila kama atakuwa amelala itakuwa ni vigumu maana itakuwa unaongea na mtu aliyelewa au hataeleweka kwa kile anachoongea... ila akiamka anaweza kukumbuka kama uliongea naye ila hatajua ni nini na kwa upande wake ataona ilikuwa ni ndoto tu. ( zingatia kua focus kwa kile unachotaka mfano kama umemfocus john,juma,rashid n.k huyo ndio utamuona)
15: Astral Projection huthibitisha maisha baada ya kifo? Ukweli: hakuna uthibitisho wowote kuhusu kuwa mtu ambaye anafanya AP hata akifa ndio ataenda kuishi maisha hayo... Ila baadhi ya watu wanaofanya astral huamini kuna maisha baada ya kifo, kumbuka kwenye astra kuna kula, kulala,kucheza,sex na vingine vyote ambavyo hufanyika kwenye maisha ya kawaida ... na ndio maana wengine huona kifo ni kitu cha kawaida tu kwao wala:thumbup::thumbup: hawaogopi.
#»»»»swali/maoni/mchango unakaribishwa««««#

Heshima kwako kwa maelezo haya rahisi kabisa katika lugha hii ya kibantu maana huko google lugha iliyopo ni ile iliyokuja na meli kwaiyo ni ngumu kwa wengi humu.
 
Practice Practice Practice

Woga tupa kule
 
Heshima kwako kwa maelezo haya rahisi kabisa katika lugha hii ya kibantu maana huko google lugha iliyopo ni ile iliyokuja na meli kwaiyo ni ngumu kwa wengi humu.

teh teh teh eeeh..... lakn mkuu si kuna google translation?
 
Mkuu Bennie 369 ebu naomba ufafanuzi kidogo jana nilikuwa napitia makala flan nikaambiwa kusafir au kupaa masaa marefu kama nchi nyingine au outer space inahitaji utaalam wa hali ya juu kuhusu kucontrol speed, kufocus n.k... Ssa nataka kujua kama mtu huez kupotea coz of silva cord kwann mtu uhofie speed!
Pili nikaona kitu kinaitwa AP sex nahitaj ufafanuz kidogo apo kuwa ni je AP body inaingilia physical body ya mtu au zote ziwe in AP.

Ndio astral sex ipo uwezekana wa ku doo upo, kumbuka vyote unavyofanya katika ulimwengu wa kawaida hata kwenye astral vipo, ila ni astral kwa astral tu, ila astral kwa mwili wa kawaida haiwezekani na nishaelezea kwenye comments zilizotangulia ila inashauriwa unapofanya astral epukana nakufanya sex, unajua ni kwa nini???.... sex upofanya huwa kuna exchange/kubadilishana energy/nguvu kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine, ambazo zinaweza kuwa positive/chanya au negative/hasi. na hiii ipo hata kwenye ulimwengu wetu wa kawaida, unaweza kufanya mapenzi na mtu na ukawa mtu mwenye bahati sana inamaana hapo kakuongezea positive energy/nguvu chanya, na pia unaweza kufanya sex na mtu alafu ukawa ni mtu mwenye mikosi na mabalaa yakakuandama sana ina maana kakupa negative energy/nguvu hasi. na pia hata wewe unaweza kumpa nguvu zako positive akawa na bahati au ukampa negative/hasi akawa na mikosi sana. ndo maana kufanya sex sio mhimu sana maana kuna vitu vingi tu vya kufanya huko ambavyo vinafaida kwako.
Kuhusu ishu ya speed inategemea na vibration yako, ndipo itakapokufikisha na ukumbuke pia uwezo wa kiroho tupo tofaut... ndo maana unashauriwa kupunguza kula red meat/nyama nyekundu au matumizi ya alcohol/pombe/sigara .... hivi ni vitu vinavyofanya uwe na vibration ndogo hivo kukupunguzia focus na speed. na pia acha matendo maovu au upunguze....silver cord haiwe kukatka we elewa ivo na pia huwez kupotea, jaribu kupitia coments zilizo tangulia maana hv vtu vyote vimeelezewa kiundan zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom