Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Watu wengi wanaposikia neno jasusi, mara moja hufikiria bunduki, mavazi ya siri na filamu na riwaya za upelelezi za Watibeli. Lakini katika maisha ya kawaida, ujasusi ni uwezo wa kuona kile ambacho wengine hawakioni, kusikiliza kwa makini, kuchambua taarifa, na kufanya maamuzi sahihi bila papara. Huo ni ujuzi unaoweza kumsaidia mfanyabiashara, mwajiriwa, mwanafunzi, mjasiriamali na hata mzazi.
Kijana anayejifunza ujasusi wa maisha huwa si rahisi kudanganywa, hutambua fursa mapema, huepuka mitego ya watu wenye nia mbaya na hujenga uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi. Hivyo, ujasusi si kwa ajili ya kufanya uhalifu, bali ni sanaa ya kutumia akili, umakini na uchunguzi katika maisha ya kila siku. Ili kujilinda, kujiimarisha na kupata mafanikio.
Nitakupa siri. Siri za kitibeli. Uliwahi kujiuliza kwa nini unamacho mawili na masikio mawili, lakini ulimi Mmoja na pua moja. Unaweza ukasema TaikonMaster unaulizwa swali la kitoto. Nazungumzia milango ya fahamu ambayo huratibiwa kwa sehemu kubwa na Ubongo wako.
Unapojenga nyumba unaweka milango miwili. Hasa entrance na exist doors. Yaani angalau milango miwili. Kuna sababu ya kufanya hivyo.
Unamacho mawili sio ili yote yatatazame kitu kimoja kwa wakati mmoja. Ni fumbo, ni falsafa kwamba macho mawili yanapaswa yaone zaidi ya kile jicho moja lingeona.
Unamasikio mawili ili usikie zaidi ya kile unachokisikia. Yaani zaidi ya ungekuwa na sikio moja. Hiyo ni siri mojawapo ya ujasusi.
Sio unaona taarifa mitandaoni au Habari. Basi wewe unaichukua kama ilivyo. Nope! Lazima uone zaidi ya kile unachokiona. Lazimq ujiulize. Nani mnufaika wa hiki kinachoendelea. Ukishamjua mnufaika utakuwa karibu kujua sababu ya hayo na ukweli wa yote.
Kwa Watibeli. Kila hadithi na simulizi kuna ukweli uliofichwa ambao msimuliaji hataki msikilizaji ausikie. Kazi ya jasusi ni kusikia yale yaliyofichwa sio yale yanayosemwa.
Sitaki nirefushe mambo. Kwa maana kuandika kwa hitaji nguvu, na kusoma sana kunachosha akili.
Zifuatazo ni mbinu ya kijana au mtu yeyote kujifunza yeye mwenyewe ujasusi kwa ajili ya kufanikisha mishe zake;
1. JIFUNZE KUTAZAMA ZAIDI KULIKO KUONGEA.
Niliwahi kukufundisha tofauti ya kutazama na kuona. Hili ni somo pana. Lakini sio siku yake.
Watu wengi huongea sana kiasi kwamba hushindwa kutazama kile wanachoona kinachoendelea mbele yao. Jizoeshe kukaa kimya na kutazama mazingira, mienendo ya watu na mabadiliko madogo yanayotokea. Iwe Sokoni, kazini au kwenye usafiri wa umma, utaanza kugundua mambo ambayo awali hukuwahi kuyatambua.
2. Jenga Kumbukumbu Nzuri.
Lazima ujifunze na uimarishe akili yako iweze kukumbuka vitu ulivyoviona, kusikia na kuviwaza.
Jasusi mzuri hutegemea sana kumbukumbu kuliko maandishi. Jifunze kukumbuka majina ya watu, maeneo, muda wa matukio na mazungumzo muhimu. Ukiwa na kumbukumbu imara, utaunganisha taarifa kwa haraka na kufanya maamuzi yenye usahihi zaidi.
3. Jifunze Kusoma Lugha ya Mwili
Kila kitu unachokiona ni ishara, Alama na lugha inayowasilisha ujumbe fulani. Lugha ni combo cha mawasiliano. Lazima ujifunze lugha ya mazungumzo, hasa upande wa Maana(Semantiki), ujifunze lugha ya mwili ambapo hii ndio muhimu zaidi, kisha lugha ya mazingira na viumbe wanaokuzunguka.
Mtu anaweza kusema "niko sawa" huku mwili wake ukisema tofauti. Angalia mkao, macho, uso, sauti na namna mtu anavyotenda badala ya kutegemea maneno pekee. Ujuzi huu utakusaidia kuelewa hisia na nia za watu katika mazingira ya kawaida kama biashara, kazi au mahusiano.
Hayo yote yanategemea uwezo wako wa kudhibiti hisia zako, kutambua patterns na kuzingufua.
4. Kusanya Taarifa Kutoka Vyanzo Tofauti
Sisi Watibeli hatuko limited. Hatunaga mipaka kwenye kukusanya taarifa.
Sio kwa sababu mimi ni Mkristo basi nisisome Quran na hadithi za waislam. Watibeli hatuko hivyo.
Sio kwa sababu umeamua kuwa mwema basi usichukue taarifa za wahalifu. Watibeli hatuko hivyo. Watibeli tunasomq na kukusanya taarifa mpaka za kuzimu, wachawi, mashoga, wauaji, n.k.
Usiamini taarifa moja bila kuilinganisha na nyingine. Soma vitabu, sikiliza watu wenye mitazamo tofauti na fuatilia yanayotokea katika jamii. Kadiri unavyopanua vyanzo vya taarifa, ndivyo unavyopunguza nafasi ya kupotoshwa.
Zingatia sisi Watibeli, UKWELI ni moja ya nguzo kuu ya utibeli. Na huwezi kuupata ukweli kwa kujifungia kwenye boksi na chanzo kimoja cha taarifa.
Ukiambia Habari za Yesu, na ukawa mfuasi wa Yesu. Haimaanisha usifuatilie Herode na Pilato wao upande wao ukoje. Kwa nini wamuue Yesu.
Ukiambiwa Habari za Shetani kwamba aliasi. Lazima utafute na upande wa Shetani uone yeye anasemaje. Huo ndio Utibeli. Na ndio msingi wa jasusi wote wabovevu duniani.
Ukishajua ukweli. Utaamua uutumie kwa maslahi yapi.
5. Jifunze Kuuliza Maswali Sahihi
Hakunaga Ujasusi bila Maswali.
Swali zuri linaweza kukupa taarifa nyingi kuliko maelezo marefu. Badala ya kuuliza kwa haraka, tafakari kwanza unataka kujua nini hasa. Katika biashara, kazini au kwenye mazungumzo ya kawaida, maswali yenye akili hufungua milango ya maarifa bila kuonekana kama unafanya uchunguzi.
Nitaeleza siku nyingine Sanaa ya maswali. Yaani unauliza kama hujauliza. Hii inamfanya unayemuuliza asijue ameulizwa na kuepuka kuona unamchimba.
6. Dhibiti Hisia Zako
Hasira, hofu na furaha kupita kiasi vinaweza kufanya mtu afanye makosa. Jifunze kutulia hata unapokutana na habari zinazokushtua au zinazokufurahisha. Mtu anayedhibiti hisia zake huwa na uwezo mkubwa wa kuona ukweli kuliko anayesukumwa na kuendeshwa na mihemko.
7. Fanya Uchambuzi Kabla ya Kuchukua Hatua
Usifanye maamuzi kwa sababu tu watu wengi wamefanya hivyo. Au watu wengi au kuna mtu anataka ufanye hivyo. Linganisha faida, hasara na matokeo yanayoweza kutokea kabla ya kuamua. Tabia hii itakuepusha na hasara nyingi katika biashara, ajira na maisha ya kila siku.
8. Linda Siri Zako, Heshimu Siri za Wengine
My friend, hili nalisisitiza kwa mkazo. Epuka kutoa siri zako kwa watu. Unajimaliza. Siri ndio nguvu yako. Udhaifu wako ndio nguvu zako kimedani.
Ubongo ni kiungo laini sana lakini ni dhaifu kuliko kiungo chochote kwenye mwili wako. Na ubongo ndio kiungo nyeti namba moja ndipo vingine vifuate. Kwa udhaifu wa ubongo angalia jinsi fuvu la kichwa lilivyogumu. Ulinzi mkali kulinda ubongo..angalia moyo ulipo. Kuna kifua na mifupa migumu inayozuia shambulio lolote.
Lazima ulinde siri na madhaifu yako na familia yako.
Halikadhalika. Jifunze kutunza siri na heshima za watu wengine. Hata kama unajua kitu gani kutoka kwa watu wengine. Usiropoke ropoke.
Si kila jambo unalolijua linahitaji kutangazwa. Mtu mwenye busara hujua wakati wa kuzungumza na wakati wa kunyamaza. Ukijenga sifa ya kutunza siri, watu watakuamini na utapata taarifa nyingi zaidi kwa njia halali.
9. Jifunze Kutambua Mifumo
Hili niliwahi kulieleza kama mada inayojitegemea.
Mifumo iko mingi sana duniani. Ila mikuu ni Serikali, Dini, Mifumo ya ajira, mifumo ya ndoa.
Isome, itambue, kisha utajua namna ya kuendana nayo.
Elewa mfumo mdogo hauwezi kubadilisha mfumo mkubwa. Ukisoma kwenye concept ya River piracy au River capture.
Mifumo mikuu ndio hutengeneza channels za matukio. Weka hilo akilini.
Matukio mengi hayaji kwa bahati mbaya; mara nyingi hujirudia kwa mfumo fulani. Ukiwa makini utaona tabia za watu, nyakati za biashara kushamiri au kudorora, na sababu za mafanikio au kushindwa. Anayeona mifumo mapema huwa hatua moja mbele ya wengine.
10. Jifunze kuwa Low Key, Low Profile.
Usipende heshima heshima.
Usipende kuzingatiwa zingatiwa. Hayo ni makosa.
Usipende mng'ao mng'ao hasa kwenye mambo nyeti yanayokunufaisha.
Acha wakuone unamaisha magumu.
Acha wakuone huna lolote.
Acha wakupuuzie.
Usipende kujionyesha unavyo hata kama unavyo kweli. Huko ni kualika nzi.
Vaa kawaida.
Tembea kwa utulivu.
Watu wasijue wakati ukiwa na hela na wakati ukiwa hauna hela.
Zingatia; usitake heshima na kuzingatiwa na kila mtu au watu wengi au wote. Ishi kama haupo vile.
Ukiweza kuishi watu wakikupuuza bila mng'ao utakuwa umefanikiwa pakubwa. Hasa kwa kijana mdogo unayeanza maisha.
Oooh! Ndugu wananipigia simu kila round wanataka niwape pesa. Nashindwa kuwanyima. Yaani maisha yananishinda.
Watu hawawezi kukuomba hela kama hawakuona mng'ao.
Nyuki hawawezi kwenda kwenye mti usio na maua. Ficha maua yako uone kama kuna nyuki atakusogelea.
Nimemaliza. Leo sitaki maswali.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam