Jinsi ya kuwa Jasusi kwa kujifunza mwenyewe ili ufanikiwe katika mishe zako

Jinsi ya kuwa Jasusi kwa kujifunza mwenyewe ili ufanikiwe katika mishe zako

Hoja ilishajibiwa muda mrefu sana, anza mwanzo wa reply yangu si mwanzo wa ubishi wake
Neno Jasusi amelitoa kwenye muktadha wa kipolisi/jeshi na kulitafutia sehemu nyingine ikiwa na maana ileile.
Inawezekana hata wewe ukalitumia kwa jinsi unavyotaka na ikaleta maana iliyokusudiwa. Mf Gwajima Jasusi la mbinguni
Messi jasusi la soka, nk.
 
Nafunga mjadala hapa nadhani uelewa wako ndiyo limited. Upelelezi umegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Ukachero na Ujasusi. Inategemea na wigo wa utendaji kazi wake ndiyo hujenga maana hiyo.

Mpelelezi akifanya kazi ndani ya mipaka nchi yake anaitwa Kachero.

Mpelelezi akifanya kazi nje ya mipaka ya nchi na nchi anaitwa Jasusi.

Hata riwaya nyingi za kipelelezi ukiona mhusika anaitwa Jasusi jua ashafanya kazi nje ya mipaka ya nchi au anafanya kotekote ndani na nje. Mfano Willy Gamba, Joram Kiango, Jacob Matata, hao wote waandishi wao waliwaita majasusi na wana operesheni hadi nje. Hakuna kazi inayozungumzia jasusi halafu akawa ni mfanyakazi wa upelelezi wa ndani ya nchi tu. Ukibisha njoo na ushahidi.

Hii itakuwa reply yangu ya mwisho ukiamua kubisha ni juu yako sababu uwezo wako kielimu ni una kikomo cha happ ulipo. Sitajibu reply nyingine yeyote hata ukitumia multiple id

Anhaa!
Sasa nimekuelewa
Kwa hiyo msingi wa hoja yako unaipata kwenye kusoma Riwaya? Ndicho unachojaribu kueleza hapa.

Sio vibaya kusoma riwaya. Na nakupongeza kwa hilo.

Unachoshindwa kuelewa ni kuwa waamdishi wengi wa riwaya hawajawahi kuwa Watu wa ulinzi na usalama. Tena zaidi wengi wao sio wataalamu wa isimu. Hilo fuatilia utagundua.

Kumaanisha huwezi watumia kama sehemu ya kujibu hoja za kitaaluma. Wao wanaandika kwa sababu mbalimbali.

Tukirudi kwenye hoja yako ya jasusi na Kachero.

Kwenye Lugha kuna kitu kinaitwa Sinonimu, synonyms. Yaani visawe. Yaani maneno tofauti yanayorejelea maana ileile.

Kachero, Jasusi, mpelelezi, askari kanzu, na majina mengine.

Kwa hiyo wewe kama upo Tanzania, lakini unapeleleza Iran, kwa kutumia labda teknolojia au kupitia informer wako utaitwa nani? Kachero au Jasusi kulingana na mtazamo wako?

Kila jasusi ni Mpelelezi.
Lakini sio Kila Mpelelezi ni Jasusi.
Hilo weka Akilini.

Mwanzoni nilikuuliza, Nini maana ya ujasusi? Ukinipa maana yake utakuwa umemaliza mjadala
 
Jasusi ni mpelelezi anayefanya kazi nje ya mipaka ya nchi yake. Si kila mpelelezi ni jasusi, ingawa majasusi wote ni wapelelezi.

Kuna kachero, ndiye wa ndani ya mipaka ya nchi itakuwa umemgusia huyo kwenye mishe za kawaida. I

Mama wa Kitibeli:
Kwanza utibeli sio ukamilifu bali kupenda na kutafuta Ukamilifu.

Vigezo au Sifa za kuwa Mama wa Kitibeli;

1. Lazima kila siku ajitahidi ku transform kutoka kuwa Binadamu(Mnyama), kuelekea kuwa Mtu(Uungu).

2. Ajifunze kutumia Baraka alizonazo kwa Akili, haki na upendo. Bila kuumiza wengine. Ataumiza wengine kama itatokea atachokozwa au kushambuliwa.

3. Ajue uzuri wake ni fahari yake na mumewe atakaye muoa. Na sio fahari ya kila mwanaume. Ajitunze na kuwa msafi.

4. Mama anayelinda heshima ya familia yake.
Anaelewa kuwa maneno, matendo na maamuzi yake yanaweza kujenga au kubomoa taswira ya familia yake.

5. Mama anayejua yeye ni kiongozi mwenye jinsia ya Kike. Kwamba uanamke wake hautaathiri maamuzi, na utekelezaji wa majukumu yake ndani na nje ya familia yake.

6. Mama ambaye sio tegemezi. Bali ni nguzo(anayetegemewa) na mumewe, watoto na jamii. Hivyo atashirikiana na mumewe na watoto kulinda urithi wa jamii yake.

7. Mama ambaye hatakubali kunyanyaswa wala kunyanyasa, kudhulumiwa wala kudhulumu haki zake na wengine. Hili ili litokee lazima awe na akili yenye elimu, maarifa, ujuzi na ufahamu sahihi kisha asiwe tegemezi.

Hiyo ni kwa uchache
 
Hassan Mambosasa
Siku hizi elimu ni kama bahari na wewe ni kisiwa. Imekuzunguka pande zote.

Wewe uliza popote.
Je jasusi lazima afanye ujasusi nje ya nchi tuu? Muulize Hata AI kisha urudi hapa.

Hawa GenZ ndio maana wanadharau kaka zao wenye mtazamo na elimu zenye mipaka kama hivi.
 
Kwako ndio hakuna kitu kama hicho Mkuu.

Uko limited sana kwenye mambo ya falsafa na ufahamu.

Ni sawa mtu aseme shingo lazima iwe inayounganisha kiwiliwili na kichwa.
Alafu akasema hakuna shingo ya kizazi.

Kwenye lugha kuna kitu kinaitwa Semantiki. Ukiwa na elimu hiyo. Utajua kwamba unachokijua wewe kwa wengine wanakijua zaidi ya hapo kwa makumi na mama.

Sasa tutafanya huu mjadala uwe mzuri.
Ujasusi ni nini? Unaweza kujibu katika muktadha wowote, wewe unapendelea muktadha wa kipolisi.
Katumia tafsiri ya kamusi 😂
 
Jasusi ni nje ya mipaka ya nchi yako na Kachero ndani ya nchi yako.
Tusibadilishe matumizi kwa namna jina lina sound vipi ktk jamii

Hakuna kitu kama hicho.
Hiyo ni dhana kwa layman.

Kwa hiyo wewe ukiwa Tanzania, lakini unafanya ujasusi Marekani kwa kutumia Teknolojia, au informers wewe ni kachero?

Au ukifanya ujasusi wa Kidijitali uko sayari ya Mars lakini unafanya ujasusi China, Duniani. Unakuwa upo kundi gani?

Vitu kama hamvijui ulizeni, au mbishe kwa hoja.

Kachero ndio huyohuyo jasusi. Ndio huyohuyo mpelelezi. Ndio huyohuyo askarikanzu. Ni visawe.

Kila jasusi ni Mpelelezi.
Lakini sio Kila mpelelezi ni jasusi
 
Mama wa Kitibeli:
Kwanza utibeli sio ukamilifu bali kupenda na kutafuta Ukamilifu.

Vigezo au Sifa za kuwa Mama wa Kitibeli;

1. Lazima kila siku ajitahidi ku transform kutoka kuwa Binadamu(Mnyama), kuelekea kuwa Mtu(Uungu).

2. Ajifunze kutumia Baraka alizonazo kwa Akili, haki na upendo. Bila kuumiza wengine. Ataumiza wengine kama itatokea atachokozwa au kushambuliwa.

3. Ajue uzuri wake ni fahari yake na mumewe atakaye muoa. Na sio fahari ya kila mwanaume. Ajitunze na kuwa msafi.

4. Mama anayelinda heshima ya familia yake.
Anaelewa kuwa maneno, matendo na maamuzi yake yanaweza kujenga au kubomoa taswira ya familia yake.

5. Mama anayejua yeye ni kiongozi mwenye jinsia ya Kike. Kwamba uanamke wake hautaathiri maamuzi, na utekelezaji wa majukumu yake ndani na nje ya familia yake.

6. Mama ambaye sio tegemezi. Bali ni nguzo(anayetegemewa) na mumewe, watoto na jamii. Hivyo atashirikiana na mumewe na watoto kulinda urithi wa jamii yake.

7. Mama ambaye hatakubali kunyanyaswa wala kunyanyasa, kudhulumiwa wala kudhulumu haki zake na wengine. Hili ili litokee lazima awe na akili yenye elimu, maarifa, ujuzi na ufahamu sahihi kisha asiwe tegemezi.

Hiyo ni kwa uchache
Asante sana,nimejiunga rasmi nimefanyia lamination hii comment
 
Back
Top Bottom