Jionee mwenyewe jinsi teknolojia inayotumika Israel kuzuia makombora ilivyoboreshwa, akili iliyotumika kubuni huu mtambo si ya kawaida

Jionee mwenyewe jinsi teknolojia inayotumika Israel kuzuia makombora ilivyoboreshwa, akili iliyotumika kubuni huu mtambo si ya kawaida

Jiulize hao Saudia wangekuwa kwny vita kama ya Israel leo si wangekuwa sw Libyia ? Israel miaka yote yupo kwenye mtanange ila bado anajenga nchi yake , na kazungukwa na maadui , Israel wapewe maua yao , siku wakiachiwa miaka 30 bila chokochoko zozote utaona atakavyowaacha hao Saudia kimiundo mbinu , taifa la juzi 1948 kipind hiko Saudia wapo hatua kadhaa ila leo hii Israel wapo juu kiuchumi
Vita wameitaka wenyewe kuchukua ardhi ya watu kwa nguvu.
Huwezi shindana na mtu anamiliki mafuta au gas, Russia kuzuia gas hapo Ulaya ilikuwa shida, mafuta ni pesa,hao wazee pesa inamiminika kutoka ardhini.
 
Matajiri wengi wa Kiyahudi hawaishi Israeli.Ulaya na America ndiko kuliko na Wayahudi wengi kwenye mfumo wa pesa wa kidunia.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Nakuambiaje mzee hizo ni hekaya, wayahudi wanajua kuwachukua akili na kuwatisha.
US ana support Israel kwa sababu wana kitu common, wote wanataka kuwamaliza nguvu arabs, serikali ya US hata wakerewe na wamasai wapo ukifuatilia koo.

Wenye asili ya Japan, India, China hadi Iran wapo sector zote hapo US.

Jews wapo, in short watu wa mataifa yote wapo pale. Jeshini huko ndiko usiseme hadi wenye asili ya Afghanisan, Pakistan, Lebanese, Palestinians wapo wengine wana vyeo.
 
Waisrael ndio wanashikilia mifumo ya fedha, suala la pesa sio tatizo kwao ila hawasemi hadharani, missle moja ya iron dome kuwa dola elf 50 kwao ni kama kununua mawe ya manati.

Mambo ya fedha hayawaumizi vichwa.
Israel wanapewa dollars billion 3 ($ 3 billion) na US kila mwaka ili kugharamia huo mfumo wa Iron dome.

Kiufupi huo mfumo upo Israel ila unafadhiliwa na kugharamiwa na US.
 
Hakuna nchi inaweza izuia makombora 1000 kwa pamoja. Hata 100 kwa pamoja haipo sababu huwezi jaza batteries kibao sehemu moja, hizo chache zilizopo lazima ziwe overwhelmed na bado kuna reloading time
Kama ndio hivyo zile roketi 150,000 za Hezbollah ni kitisho sana kwa Israel, yaani Kuna hatari miji mingi ya Israel ikawa hatarini mzozo ukigeuka Vita kamili.
 
Nakuambiaje mzee hizo ni hekaya, wayahudi wanajua kuwachukua akili na kuwatisha.
US ana support Israel kwa sababu wana kitu common, wote wanataka kuwamaliza nguvu arabs, serikali ya US hata wakerewe na wamasai wapo ukifuatilia koo.

Wenye asili ya Japan, India, China hadi Iran wapo sector zote hapo US.

Jews wapo, in short watu wa mataifa yote wapo pale. Jeshini huko ndiko usiseme hadi wenye asili ya Afghanisan, Pakistan, Lebanese, Palestinians wapo wengine wana vyeo.
Upo sahihi kabisa kiongozi, US Kuna kila aina ya jamii iliyopo hapa duniani.

Ushirikiano wao na Israel ni wa kimkakati zaidi, ila sana sana wale 'Christian Evangelicals' ambao ndio wengi huko US, wapo mstari wa mbele kuisapoti Israel sababu ya kiimani.
 
Nisiongee sana, hebu tazameni wenyewe kinachoendelea wakati huu.

View attachment 2793664
Ukiambiwa Israelites sio binadam just believe haya majamaa yana nguvu za Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo. Kazi kwako. Yaani jina lao tu maana yake walishindana na Mungu. Je utawaweza? Hapo waarabu wakigusa tu wamenasa na anamtaka mmoja tu Iran
 
Sipo hapa kutetea waarabu wala Israel, vyovyote vile ni sawa, lakini hekaya za kunambia Israel wamekamata mifumo ya fedha sio kweli.

Nikakuambia kuna nchi zina pesa kama hizo za uarabuni, haimaanishi natetea no, lakini nazunumza ukweli, Israel haina uchumi wowote wa kupambana na nchi kama Iran, Russia, China au India. Ni ile mnawapamba sana.

Hii vita tu ya Hamas wameomba msaada dola bilioni 14, Tamir intercepto 1 ya iron dome ni Tshs milioni 125.

Wakai huo Hezbollah wana makombora 150,000 ukijumuisha advanced precision-guided missiles, rockets kiasi hiko hata iron dome haiwezi hilo battle. Thats too much.
Utetei na unaegemea kwa mwarabu Mara Hamas Mara hizbullah Wana makombora 150.000 vipi funguka. Hao wote uliowataja mfadhili wao Ni iran
 
Kama ndio hivyo zile roketi 150,000 za Hezbollah ni kitisho sana kwa Israel, yaani Kuna hatari miji mingi ya Israel ikawa hatarini mzozo ukigeuka Vita kamili.
Hizo 150,000 nyingi ni ndogo kina Katyusha na zenye range ndogo. Zipo maelfu zenye zaidi ya 150km range ila probably haziwezi fyatuliwa kwa kufuatana mpaka ziishe.

Israel haiwezi kubali kupokea maroketi na makombora mengi. Tutaitafutia lawama mapema hii lawama ya Hamas ni ndogo. Hezbollah wanajua hilo, na Iran wanajua. Ikitokea wanapigana Hezbollah itarusha casually ila kutuma salvo mwanzo mwisho Israel itazima vita kwa roho mbaya sana.
Iran hao watabidi wapige military installations, wakipiga civilians wanapewa majibu makali. Na Israel ilivyo ndogo ukitumia missiles na rockets kupiga raia unaipa justification ya kutumia WMD, na ambavyo Iran mara nyingi inatoa chants za death to Israel mtakuja pelekana mahakama za kimataifa baada ya Tehran kufanywa ruined city.
Hakuna vita ambayo Waarabu walipiga miundombinu ya raia wa Israel, wakitumia mbinu hiyo usishangae Israel hadi chemical weapons, biological weapons na nuclear inatumia.

Na hakuna namna Iran itapigana na Israel bila msaada wa jirani, hawapakani. Anatafutwa kiherehere atakayeungana na Iran agawanywe nchi. Ndio maana Israel inashambulia Syria kila mara shipments za Iran zikijulikana. Na Iran inatafuta makundi washirika ndio waisaidie kupigana na Israel sababu wako nchi jirani nayo.
So Israel kupitia Gaza inayahakikishia mataifa yatakayotumiwa na magaidi yatapigwa airstrikes za kutosha.

It's very complicated ila ninachoamini Iran italazimishwa ipigwe haraka sana ili isiharibu zaidi uchumi wa dunia. Strategy yao ni kuharibu uchumi iitwe kwenye mazungumzo, it's either waipige faster ishindwe au waizembee wakae nayo mezani. Some months of hell hapa duniani.
 
Lini Israel imeshindwa Vita vya chini ?

T14 Armata
Israel iliwahi poteza vita moja tu, vita ya propaganda dhidi ya Waislamu na Waarabu. Na hiyo vita inaenda kuwa neutral diplomasia zinafanya kazi.

Hizo nyingine waletwe hao Hezbollah, Hamas, Iran, Islamic Jihad na yeyote tukae miezi michache tuone baada ya vita kuisha ni ardhi ya nchi gani imeongezeka.

Syria wanajua, Jordan hao hata ukiwa gaidi ndani yao ukaitishia Israel wanakupiga alafu wanaitaarifu Israel kwa kuomba msamaha. Sera kwa sasa ni ileile, ukishindwa kumkanya mwanao tutajua unamtuma wewe na tutakuja kumuadhibu wenyewe kwako. Misri hana huo muda, avunje mkataba Sinai ibebwe tena.
 
Kuhusu matumizi mi sifahamu , lakini ukitembea Qatar, UAE au Saudia na ukaenda Israel utaona tofauti kubwa ya kimiundombinu, utaona hao arabs walivyoendelea kuliko Israel.

Lakini ukae ukijua tu kuna nchi tajiri na nchi yenye uchumi, Qatar inaizidi utajiri US, lakini US wanaizidi uchumi Qatar.
Waisraeli na Israel yao sio matajiri ila Wayahudi ni matajiri. Israel haiwezi kuwa tajiri sababu haina resources, ina changamoto za kiusalama, haipo strategically located kama sisi au Singapore. Yani Israel haina lolote la kuifanya iwe nzuri kiuchumi, pale ilipo ni juhudi na akili kubwa yao. Ikitakiwa iwe level za Yemen, wale ndio Middle East wasio na rasilimali kabisa. Usiilinganishe Israel na Qatar nchi ya pili kwa kuchimba gesi duniani. Usiilinganishe na Saudi Arabia inayouza zaidi ya mapipa milioni 2 ya mafuta kila siku.

Wapemba ni matajiri Kariakoo, ila Pemba sio eneo tajiri. Ukiwa Pemba uuze nini ili uwe tajiri? Samaki uuze Tanga, Unguja, Dar ambapo nao wanavua? Ulime kwa ardhi gani iliyopo Pemba?

Sababu mojawapo ya Wayahudi kuchukiwa ni kila wakienda sehemu wanatajirika na kushika sekta nyeti kuliko wazawa. Usingekuwa Uislamu wabongo wangewachukia Waarabu ambao hata Kiswahili hawajui fasaha ila wanamiliki uchumi wa miji. Wahindi hawapendwi wanatajirika kwa hela wakati Wazaramo wanatajirika kwa singeli na vigodoro.
 
, hizo ni hekaya, nchi zenye pesa chafu ni arabuni huko, israel inapokea msaada wa dola bilioni 3 kila mwaka kutoka US, na juzi hapa wameomba wasaidiwe dola bilioni 14 kupambana na Hamas.

Vita ni gharama mzee, wangekuwa wameshikilia mifumo ya pesa wasingeomba msaada.
Waisraeel ndio wanaotengeneza hayo maisha apo marekani. Na wanaotoa izo pesa ni wayahudi wenzao
 
Missile 1 ya iron dome ina cost $50000.
Roketi moja likizuiwa lililotengenezwa kienyeji, almost Tshs milioni 125 imetembea, vita ni gharama sana.
kwa hesabu za haraka hapo ni kama bilioni 5 Tshs zinafika kuzuia hayo maroketi.

Kwa Tech ya Iron Dome Israel ipewe maua yake, nisiwe mnafiki.
Inazuia makombora yaliotengenezwa mitaani ilitakiwa ipimwe Kwa kinzal
 
Back
Top Bottom