Jioni moja miaka mingi iliyopita na Subhash Patel

Jioni moja miaka mingi iliyopita na Subhash Patel

Nasononeka sana nikiona kejeli na mzaha kwa mtu kmaa Mohamed Said.
Nimesoma kitabu chake cha Wakati na Maisha ya Abdulwahid Sykes na ni mtu anayejua anachokiandika.Kitabu kimeandikwa baada ya utafiti mkubwa (kupitia nyaraka katika maktaba za CCM/TANu,kuongea na watu mbalimbali )Si mwandishi wa hadithi.
Tafuta hicho kitabu kisome na utakuja kushangaa kuwa unafanya mzaha kwa mtu ambaye hata akiondoka ataacha kumbukumbu kubwa.
unasahau kuwa ukitaka kumficha mtz kitu wewe andika kwenye kitabu, utamaduni wa kusoma tu hatunao. Huwezi kukuta kijana ana hobby ya kusoma vitabu novels, thubutu rika na kizaz cha kujua kutembea na viredio vya Bluetooth kuimba singeli. Sasa watathamin vipi waandishi il hali hata thamani ya kusoma tu hawaijui.

Nchi za wenzetu maktaba ndio sehemu watu wanapenda kwenda na waandishi ni watu wenye utajiri mkubwa na umaarufu.
leo kijana wa leo muulize tu umesoma novels, au vitabu vingapi hana jibu

watu kama kina James Hadley chase eeh em niambie ukishika kitabu hutaki kubanduka.

nimesoma hicho kitabu The life and Times of Abdulwahid Sykes, very analytical books with details and ushahidi leo watu kama kina J.K Rawlings waloandika Harry Potter wangekua hai wangeshangaa namna vitabu vyao vinavyouza.
 
Ni kutokuzoea tu weznetu Maulaya wana kitu kinaitwa Eulogy misibani kila mtu akipenda anasimama anapewa Mic anasema jinsi alivomjua au chochote kuhusu marehemu hata kama ulitaniana nae just watu kumuenzi. Mwandishi kasema ali encounter na marehemu miaka hio na kitu pekee hasahau alitizama movie ya the message

Kwa miaka hio kwanza uwe na pesa kweli kweli uwe na tv kwako ndio kumbukumbu yake sasa hawezi kusema tulikua tunawasiliana au tunakutana kwenye vikao vya biashara hapana
 
Mzee said heshima yako, vipi unauonaje mwenendo wa taifa letu hasa kwa kipindi hiki ambacho ni 2020-2025 katika nyanja ya uchumi, kijamii na kisiasa!??
Mlatinoh...
Kuna kisa cha mwendawazimu mmoja.

Huyu mwendawazimu alikuwa anafua nguo zake.
Jamaa akapita akamkuta mwendawazimu anafua basi akamuuliza, "Unafua?"

Yule mwendawazimu akamjibu kwa kumuuliza swali akamwambia, "Wewe huyaamini macho yako ndiyo utaamini kauli yangu?"

Uniwie radhi lakini naamini umeelewa.
 
Mlatinoh...
Kuna kisa cha mwendawazimu mmoja.

Huyu mwendawazimu alikuwa anafua nguo zake.
Jamaa akapita akamkuta mwendawazimu anafua basi akamuuliza, "Unafua?"

Yule mwendawazimu akamjibu kwa kumuuliza swali akamwambia, "Wewe huyaamini macho yako ndiyo utaamini kauli yangu?"

Uniwie radhi lakini naamini umeelewa.
Nadhani mzee wangu ulichomaanisha ni kwamba mim nimekuuliza kitu ambacho hata Mimi nakiona na pengine hata kukiishi.

Lakini.
Nadhani ni kwa sababu sijaliweka swali langu direct......naomba ninyumbue maswali yangu na nakuuliza wewe sababu
1. Ni Mtanzania
2. Ni mtu mzima kiumri kuzidi members wengi humu ndani
3. Unaufahamu mkubwa Sana juu ya siasa na muenendo wa nchi yetu katika nyanja mbali mbali nadhani hii ni kutokana na kuishi kwingi na kuona mengi ndani ya nchi yetu.

4. Unayafahamu sana maisha ya Mtanzania na unayaishi mpaka leo.

5. Ni mwelevu na mwenye busara Sanaa

Maswali ni haya.

1. Kuna umuhimu wa kubadilisha au kutengeneza katiba mpya ya nchi itayotokana na mawazo na fikra za Watanzania wenyewe!!??

2. Ni zipi hasara za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na members wa bunge na sekta mbalimbali ambao ni 98.5% kutoka chama tawala!?? Kama hakuna hasara Bali ni faida tupu bs naomba unijuze pia.

3. Ni kwa kiasi gani unadhani serikali inatimiza matarajio au mahitaji ya at least 40% ya Watanzania? Katika maeneo yapi???
 
MZEE ulikusudia KUZUNGUMZIA habari za maisha ya Marehemu Subhash Patel au unataka kuelezea kuhusu UISLAMU???!!!!!


"movie mashuhuri, "The Message," kwa mara ya kwanza. Hii ilikuwa sinema maarufu sana kuhusu maisha ya Mtume Muhammad (SAW). Sinema hii tukiisoma sifa na "reviews," zake kwenye magazeti tu kwani enzi hizo Tanzania ilikuwa hoi na taaban kwa kila kitu"
 
MZEE ulikusudia KUZUNGUMZIA habari za maisha ya Marehemu Subhash Patel au unataka kuelezea kuhusu UISLAMU???!!!!!


"movie mashuhuri, "The Message," kwa mara ya kwanza. Hii ilikuwa sinema maarufu sana kuhusu maisha ya Mtume Muhammad (SAW). Sinema hii tukiisoma sifa na "reviews," zake kwenye magazeti tu kwani enzi hizo Tanzania ilikuwa hoi na taaban kwa kila kitu"
Uzalendo...
Labda nikuulize unatatizwa na lipi baina ya maisha ya Subash au Uislamu?
 
Sina shida na maisha ya Patel ila nina shida na namna unavyochanganya madesa kwa makusudi kwa kuongelea mambo yasiyo na uhusiano wowote na kichwa cha habari.

Habari za wewe kutazama Sinema inayohusu maisha ya Mtume Muhammad imeingiaje hapo kwenye mada yako?!

Unataka kuhusisha maisha yake na Uislamu? Au unakusudia nini hasa Mzee wetu?!



Uzalendo...
Labda nikuulize unatatizwa na lipi baina ya maisha ya Subash au Uislamu?
 
Ungekua ni billionaire angekukumbuka pia
 
Einstein...
Hapana neno kaka sote tumefurahi na kucheka Kijana wa zamani na kijana wa leo.
Huyu mzee Said, ALLAH amlipe hata umuongelee kashfa gani hakujibu kwa utashi wake Bali anatumia hekima na busara ya hali ya juu, hakika una kila dalili ya uislam unavotaka mtu aishi, wewe nishujaa Wangu hapa jukwaani sijaona mtu wahekima na elimu kama wewe hapa jukwaani, ALLAH akulipe duniani na akupe aghera pia
 
Huyu mzee Said, ALLAH amlipe hata umuongelee kashfa Gan hakujibu kwautashi wake Bali a natumia hekma nabusara ya haliyajuu, hakika unakila dalili ya uislam unavotaka mtu aishi, ww nishujaa Wang hapa jukwaan sijaona mtu wahekma na elimu kama ww hapa jukwaan, ALLAH akulipe dunian na akupe aghera pia
Abuu...
Shukurani zote zinamstahikia Allah.
Ahsante ndugu yangu.
 
Sina shida na maisha ya Patel ila nina shida na namna unavyochanganya madesa kwa makusudi kwa kuongelea mambo yasiyo na uhusiano wowote na kichwa cha habari.

Habari za wewe kutazama Sinema inayohusu maisha ya Mtume Muhammad imeingiaje hapo kwenye mada yako?!

Unataka kuhusisha maisha yake na Uislamu? Au unakusudia nini hasa Mzee wetu?!
Uzalendo..
Ile movie "The Message," nilikuwa na hamu kubwa kuiangalia lakini haipatikani Dar es Salaam.

Siku hizo mambo magumu.

Ndipo nikaja kuiona nyumbani kwa Subash.

Ikawa sasa toka siku ile nikimsoma Subash magazetini au nikimuona katika TV ananikumbusha, "The Message."

Jingine kuhusu "kuchanganya," hii ndiyo staili ya uandishi wangu kuwa napenda kumpeleka msomaji katika nchi hajawahi kufika kwa kumchanganyia mambo.

Nimeandika vitabu 10 kwa staili hii na wahariri wamependa na kupasisha vitabu vichapwe.
 
Marehemu Rejnal Abraham Mengi kipindi anamizozano na wa Asia (mafisadi papa na Nyangumi ) walimpa siri ya mafanikio kwa Kumwambia kwamba wao wamekuja na makabrasha ya business plan tu utajiri wote wanaupata hapa kwa iyo kwa maoni yangu mm ni kua sisi hatuna plan Bali tunataka mafanikio kwa haraka bila plan mfano wao wanakuja na recognized certificate ya compuni iliyofunguliwa Asia wakiingia kwenye Taasisi za fedha kupata mkopo kwa urahisi na haraka kama wawekezaji.sisi huko kufungua campuni tu ni kama MTU anaona anapoteza pesa yake bure hatimae tunajikuta tunakwenda kukopa pesa yetu wenyewe kwao wao .Niko radhi kurekebishwa nilipokose .hayo ni mawazo yangu tu si lazima yawe sahihi
 
Hongera sana kwa kutupa story ya jinsi ulivyoonana na Late Subash Patel ila mwaka 1980 alikuwa sio tajiri basi figisu alifanya mpaka akatajirika kwa muda mfupi.
 
Kwa nini Waasia wanafanikiwa zaidi kuliko sisi Watanzania weusi ? Halafu hawaachi utamaduni wao ingawaje wala hawaishi India/Pakistani , ...
Hata wabongo waliofanikiwa na bado hawajaacha utamaduni wao wapo....kuna wanaoabudu mizimu, wenye kufanya matambiko na wenye kushiriki uchawi na ushirikina....

Wapo waliosoma mpaka vyuo vikuu na pamoja na interaction yote na watu wa kutoka mikoa mingine, bado wanashindwa kutofautisha R na L kwa kuelemewa na mother tongue ya lugha zao za asili...
 
Back
Top Bottom