Mwanadome,
Marahaba.
Najua nina staili yangu lakini mimi ukiniuliza ni ipi nitataabika kuieleza mtu aitambue.
Ama kuhusu afya yangu ndiyo kama ilivyo afya ya mtu mzima.
Mara miguu inauma, mara mgongo nk.
Lakini mimi kwa kuwa hili ni tatizo la umri nimechukulia kuwa siumwi kwa sababu nikiijenga fikra yangu kuwa mie mgonjwa kwanza ndiyo nitakuwa mgonjwa siku zote haya hayataniacha hadi wananilaza mwanandani.
Pili nitawashughulisha watoto watakuwa hawapungui kwangu kisa nini baba anaumwa.
Ala kuli hali hali yangu ndiyo hiyo.
Sijambo Alhamdulilah niko na Netflex.
Ningefurahi sana kama utanifahamisha vipi staili yangu ya uandishi imebadilika hadi wewe kuhisi naumwa.