Jioni ya leo nina furaja kukutana na Dada mpika Uji

Jioni ya leo nina furaja kukutana na Dada mpika Uji

Hilo ni tatizo serikali ichukue hatua la sivyo hakuna umuhimu wa kusoma hadi chuo then uje ufanye kazi ambayo ungeweza kuifanya hata baada ya kumaliza form four
Sio jukumu la Serikali pekee ni jukumu pia la mhitimu.

Unategenea kama kwa sasa walimu wa Art wamejaa mashuleni unategemea nini?

Kuwaza nje ya Box

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio jukumu la Serikali pekee ni jukumu pia la mhitimu.

Unategenea kama kwa sasa walimu wa Art wamejaa mashuleni unategemea nini?

Kuwaza nje ya Box

Sent using Jamii Forums mobile app
Yah ni jukumu la kila mtu lakini kumbuka kazi ya serikali ni kusimamia sera zake kama sasa watu wanasoma then wanaishia kuwa wapika uji or wachoma mahindi na waoasha magari hapo sera ya yetu ya elimu ina matatizo na haimuandai muhitimu kuwa na upeo wa kujiajiri katika fani aliyosomea
 
Okay by the way naomba kumuuliza mtoa mada,hizi kazi mnazozishangaa za kuchoma mahindi,kuuza uji na kupiga debe mnataka zifanywe na watu wa aina gan labda?kwa upande wangu naona ni biashara inaweza ikafanywa na tu yeyote haijalishi una kiwango gan cha elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nataka kufundishwa. Nimeelimika na mada. Ni vzr kitu kama unaona hakikufai ukipotezee. Wengine hii elimu inatufaa. Hatufanani.
Na hii mada ipo jukwaa la biashara. Ukitaka aongelee mambo gani?
ina maana mpaka kuuza uji unataka ufundishwe?
ina maana miaka yote ulikuwa umekaa tu haufanyi kazi?
Huyu jamaa ndo amekufundisha ufanye kazi?acha akili za kushikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nataka kufundishwa. Nimeelimika na mada. Ni vzr kitu kama unaona hakikufai ukipotezee. Wengine hii elimu inatufaa. Hatufanani.
Na hii mada ipo jukwaa la biashara. Ukitaka aongelee mambo gani?
Hapo sasa,afadhali umenijibia na mie...kuna watu vilaza sanaa
 
Habari ziwafikie wavaa tai na milegezo
 
Hilo ni tatizo serikali ichukue hatua la sivyo hakuna umuhimu wa kusoma hadi chuo then uje ufanye kazi ambayo ungeweza kuifanya hata baada ya kumaliza form four
Aliyemaliza chuo na aliyemaliza chuo wote wanauza uji ila kuna tofauti katika uuzaji..

love thé love or hâte thé love.....
 
Safi mkuu anza na wewe kiwonder chako cha kutengeneza Uji>
 
Habari za Mida? Wajasiriamali poleni na wale tulio binasifisha muda wetu baada ya sisi kuto kuwa na kazi nao pia poleni.

Jioni hii niko naongea na Dada anaye uza uji baada ya kupita kupata kikombe cha uji. Huyu Dada kasoma Chuo cha Uhasibu Arusha ina baada ya kuhitimu kaamua ajiajiri kwa kupija uji na kuuza.

Anasema kwa siku hipika Themos 15 zile kubwa kabisa za mahotelini. Na kwa sababu ana tumia vikonbe vikubwa basi kila themos hutoa vikombe 8 tu.

Themos 15 x 8 ni vikombe 120.

Vikonbe 120 x 500= 60,000/

Akitoa gharama zote kama Sukari, mkaaa, Siagi, unga, Maji na maziwa basi anaweza tunza faida ya 30,000/

Siku mbaya huwa ni elfu 20 na siku zingine 25.

30,000/ x siku 30= 900,000/

kwa mwezi anaweza pata hiyo pesa.

Mshahara wake kwamwezi anao jilipa ni mkubwa kuliko sisi wavaa tai asubuhi.

NB: Dada kasomea Procurement.

AIBU NA UOGA NDO MUHIMILI WA UMASIKINI WAKO.

Endelea kumuonea aibu Demu wako/Mchumba/mke/Rafiki/jirani yako/wafanyakazi wenzako na kadhalika.



Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hii ni mada nzuri kabisa, wapite wote wanaotaka ajira na wenye kuogopa kufanya maamuzi. Adui mkubwa wa mafanikio kufanya maamuzi, ukiogopa maneno ya watu wengine. Heri yake dada wa uji, alishafanya maamuzi na sasa hana anachoogopa yupo huru, neno lilisema utaijua kweli na kweli itakuweka huru.. Hongera kwa kumleta.
 
Back
Top Bottom